Utafiti binafsi: Ukitegesha alarm usiku lazima uamke muda mfupi kabla ya alarm kulia

Utafiti binafsi: Ukitegesha alarm usiku lazima uamke muda mfupi kabla ya alarm kulia

Uko sahihi,hii mimi pia hua inotokea mara nyingi sana.Hili limenikumbusha kuna kipindi nilitaka kuwanunulia watoto alarm ya kuwasaidia kuamka saa 12 kwenda shule,kwa sababu kuna wakati nakuwa sipo kwa hiyo hakuna wa kuwaamsha,sasa kilichokuwa kikinishangaza wakati najianda kununua kila nikiwa sipo nikipiga simu saa 12 niwaaamshe nakuta tayari wameamka,nikawa najiuliza hawa wanawezaje kujua kuwa saa 12 imefika na sikupata jibu...
 
Conditional reflexes or bioligical clock , ungekuwa umesoma biology usingejitamba kuwa umegundua
Umenikumbusha hii hali ya Classical Conditioning 😅
Classical Conditioning ni hali ambayo hutokea pindi Vichochezi visivyo vya hiari (conditioning stimulus-CS) vinapoungana na vichochezi vya hiari (Unnconditional Stimulus-US). Pindi vichochezi hizi vinapotenganishwa kiumbe akina kichochezi kimojawapo basi anaanza kurespond kama kaona vichochezi viwil.

Halii hii hupelekea muhanga wa jambo hili kua na Tatizo la Low Latent Inhibition....Mtu mwenye Low Latent Inhibition hua anarespond kwenye stimuli/vichochezi za zamani au anavyovifahamu kama anavyorespond kwenye Vichochezi ambavyo ni vipya.

Nikimaanisha kwamba mtu mwenye LLI akiona kitu ambacho ni kigeni ataanza kujiuliza kitu hichi ni kitu gani, kinafanyeje kazi, kwanini ni kipo hapa na maswali mengine kibao. Kutokana na maswali hayo mtu anajiuliza yatapelekea akifahamu kitu hicho kwa undani zaidi.

Hence mtu anakua anajua vitu viiiingi sana sio kwa sababu ni Born-Genius, hasha bali ana ugonjwa wa kutoelewa Kitu kwa mara moja.
That's me.....✌️
 
Hili nimelifanyia utafiti muda mrefu sana toka niko shule

Kila nikitegesha alarm lazima nitashtuka usingizini kabla ya alarm haijaniamsha

Utakuta nimeset alarm ilie saa 10 kamili usiku lakini cha ajabu kwenye saa 10 kasorobo ama saa tisa na dakika 55 nakuwa nimeshtuka kutoka usingizini
Daaaaah
 
Mdogo wangu hii ilinisababishia simu niwe naiweka mbali ili kitendo cha kwenda kuizima alarm basi najua usingizi nishaukimbiza.

Mana nilikuwa na tabia ya kurudi kulala huku naongeza dakika tano tano 😂 hadi siku moja nikachelewa kwa Mdosi. 😂
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Mimi huwa kawaida naweka Alarm 3 zenye interval ya dk 10 kila mmoja, ili ya kwanza nisipoisikia nisikie ya pili au ya tatu. Ajabu sasa nikisikia ya kwanza nitaenda kuzima fast na zingine naweza kuzizima pia😀😀😀, halafu narudi kuuchapa, baadae nikiamka nitaanza kujilaumu kuchelewa.

Siku hizi kuna afadhali kuitikia Alarm maana mwenye jimbo akisikia pia anachochea niamke ila ugomvi unaweza ukazuka pia😀😀.
 
Hata na mimi huwa inanitokea japo siipendagi hiyo hali kwani huwa nadhaniaga bado nina masaa kadhaa mbele kumbe muda ndo umeisha. Aisee.

Nachukiaga sana yaani.
Kwanini mtu uchukie kuamka kutoka usingizini.
 
Autonomic Nervous System (ANS) Ni sehemu ya mfumo wa fahamu ambao huratibu matendo yanayofanyika ukiwa hujitambui au ukiwa umelala, pia huratibu shughuli mbalimbali za mwili kama vile mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula, kutanuka na kusinyaa kwa mboni,hamu ya kufanya mapenzi nk nk.

Ubongo hua unafanya kazi kutokana na vile akili yako itaUkomandi. Pindi unaposeti alarm kuamka saa kumi basi unakua umeusisitiza ubongo wako kwamba saa kumi alarm italia so Inabidi uamke Hence Ubongo wenyewe unakua unajua Inabidi uamke kabla ya saa kumi.

Hakuna uchawi hapo ni Saikolojia tu[emoji3577]
You're what you think....Fikra zako zaweza kujenga au kubomoa
Wabongo wengi hawana ubongo! Muulize Hayo.[emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Inategemea na umuhimu wa jambo linalokufanya uamke muda huo, masaa uliyolala, hali ya uchovu, na mazingira.
Kuna watu wanaweka alarm na bado wanamiss paper. Yaani hapo ni malaika wako tu wanakusaidia kukuamsha
Hii kwenye research huwa tunaita affected variable ambazo tuna Zi draw kutoka kwenye conceptual framework

Sent from my Infinix X682B using JamiiForums mobile app
 
Hili nimelifanyia utafiti muda mrefu sana toka niko shule

Kila nikitegesha alarm lazima nitashtuka usingizini kabla ya alarm haijaniamsha

Utakuta nimeset alarm ilie saa 10 kamili usiku lakini cha ajabu kwenye saa 10 kasorobo ama saa tisa na dakika 55 nakuwa nimeshtuka kutoka usingizini
Biological clock.
 
Naweza nikakuunga mkono mtoa mada kwa kiasi fulani sababu mimi huwa naweka alarm siku ambazo huwa nina Safari asubuhi ila huwa mara zote naamka kabla ya alarm.
 
Back
Top Bottom