Utafiti: Profesa Janabi yupo sahihi 100%; watu wanajiua wenyewe kwa upumbavu wao

Utafiti: Profesa Janabi yupo sahihi 100%; watu wanajiua wenyewe kwa upumbavu wao

Hata Mayor Jacob biashara yake ya Mayai imeshamiri kutokana na mazingira wezeshi ya Chama cha Mapinduzi
Kwa akili kama hizi, Profesa Janabi anayo kazi ya kutoa elimu kwa mbumbumbu.
 
Population sample ndiyo inathibitisha Janabi yupo sawa 100%?

100% umeipata kwa population sample kivipi? Watanzania 100% wanakufa kwa kula ovyo?

Population sample inathibitisha Janabi hakosei hata neno moja?

Unaelewa 100% ni nini wewe?

Nimekuuliza assumptions zako na margin of error, kwa nini hujajibu?
Kafanye utafiti kama niliofanya mimi mkuu. No research, no right to speak.
 
Unakuta mtu anakula kula zaidi mara tatu kutwa nzima, tumbo lake halijawahi kukosa chakula, hajui njaa mwili umenenepa hafanyi kazi za kutumia karoli kwa wingi mwilini, ni wa kukaa ofisini na kupanda gari tu kumbe angetembea tu hata umbali fulani ingetosha kusambaratisha sukari na mafuta mwilini mwake na mwili ukawa balanced, hiyo haifanyiki. Zamani kula iliendana shuhuli ya kufanya na muda wa kukaa bila kula huku ukiwa kwenye shughuli fulani. Siku hizi kukuta mzee bonge wa miaka 60 na hana changamoto za kiafya mwilini mwake ni nadra sana
 
Kafanye utafiti kama niliofanya mimi mkuu. No research, no right to speak.
Utafiti gani usio na assumptions wala margin of error? Nimekuuliza umekimbia kujibu haya maswali. Utafiti gani huo?

Umefanya utafiti kuhusu nini?

Na Profesa Janabi yuko sahihi 100% kuhusu nini? Unaijua 100% wewe?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Nakumbuka Mwaka ule nilipokuwa nafuatilia au nafanya utafiti usio rasmi. nakumbuka mada zangu nilizokuwa nafanyia kazi

"kwanini watu wanafanya mazoezi ila hawapungui"

nikawa na mada nyingine
"namna ya kupungua"

nikawa na mada nyingine
"namna ya kupungua pasipo kukonda"

Mwaka ule nilisoma nyaraka nyingi na kupitia machapisho mbalimbali sana pia nilikuja kuhitimisha kwa kujua kwann wanga ndio chakula kikuu kwa watanzania wengi na Amerika hasa ya kaskazin na ambako wanasumbuliwa zaidi na obesity.

hitimisho kiujumla ilikuwa ni hivi

1. adui mkubwa wa mwanadamu ni ulaji mwingi wa sukari na wanga.

2. adui mwingine ni ulaji usio na mpangilio. na milo mingi kama kuku mfano kwa siku mtu anamilo takribani mitano

3. elimu potofu. mfano mafuta ya wanyama yanaganda kwenye mishipa ya damu kitu ambacho si kweli wale walowahi shuhudia autopus/post motm watakuwa mashahidi

4. tatizo jingine kutokuwa na ratiba ya chakula. mtu akiamka asubuh ndo anafikiria ale nn. kitu ambacho kinafanya mtu alekile alichokiwaza kwa siku hiyo.

5. elimu potofu ya kunywa dawa za kuharisha ili kuondoa mafuta yaliyo ndani ya tumbo.
hii ni elimu ilojaa uongo mkubwa sana. mafuta hayakai ndani ya utumbo ila nje ya utumbo wa chakula
wale walowahi kufanya au kushuhudia upasuaji. wanafahamu yanapokaa mafuta
yanakaa nje kuzunguka utumbo na organ nyingine za mwili mfano moyo.figo nk.

6. elimu potofu ya maji ya moto.
mtu anamshauri mwenzake anywe maji ya moto ili ayeyushe mafuta yaliyo tumboni.
huu uongo umekaa miongon mwa watu miaka mingi,mafuta yanakaa chini ya ngoz sasa unawezaje yayeyusha na maji yanayokaa kwenye tumbo la chakula ambalo huwa haliwekagi mafutaaa?

7. mazoezi sana na ulaji sana, mtu amafanya mazoezi vizuri na anazingatia ratiba na lengo lake ni kupungua ila akishamaliza anaenda kula wanga mwingi na sukari ambavyo vinaenda kumeng'enywa na kuwa sukari ambayo inabadilishwa na mwili kuwa mafuta ambayo inahifadhiwa na mwili. mafuta hayo huwa kwenye mfumo wa minyama kiswahili chake sijui. ila tunaweza ita fat tissue.
mafuta haya kadri yanavyozidi kujilundika ndivyo mtu anazid nenepa. na huwezi yaondo kwa mazoezi peke yake. haya mafuta ni akiba ya mwili so mpaka yatumike lazma mwili uwe unaupungufu wa chakula cha kuendesha mwili kwa wakati au siku hizo.

8. Mazoezi ila mtu hajui mazoezi hayo yanamsaidia nn. mfano unakuta mtu ananyanyia vitu vizito ili kukunguza uzito au mwili. Hapa kwenye mazoezi napo panashida yake.

9. watu wanaelimu nyingi ila nyingi hazipo sawa.
ila elimu ya chakula sahihi ipo shule ya msingi nadhani darasa la sita kama sijakose pia shule ya upili.

10. Mtu anakwambia usile nyama ni mbaya. kuku ni mbaya. mayai mabaya. yan karibu kilakitu ni kibaya.
Nyama ni nzuri sana kwa afya ila kilakitu kiasi
mayai ni mazuri sana ila ni mayai gaji na kiasi gani si unakula mayai 10 ya kichemsha peke yako.

11. Wito wangu kwa watanzania wenzangu,tujitahid sana kuepuka wanga na sukari kupita kiasi.
unaweza kula hivi
Asubuhi
supu nyama
na kitafunywa chochote
plus matunda mfano tango au parachichi

mchana
Ugali mboga za majani/samaki/daga/maziwa nk
matunda
maji

usiku
Wali kiasi samaki/mboga za majan za kutosha/samaki
matunda kama parachich
maziwa fresh
nk
maji

huu mpangilio wq chakula ni mgumu kama huna ratiba ila ukiwq na ratiba hiwezi na utaona ni mgumu sana

WATU WA MICHEZO
Mfano
watu wa mpira wa miguu
Ngumi
riadha na micjezo mingine ya kutaka wepesi na uharaka
wanazingatia sana lishe maana ulaji mbaya kwao hasa pombe na wanga kunaongeza uzito ambako kunapunguza ufanisi wao

Bodybuilder
wanakula kiwango kingi cha vyakula vya proteni kwaajil ya kujenga mwili. wanga kwao wanakula kidogo sana maana ukinenepa mwili hauwezi kugawanyika.

******************************************
 
Unakuta mtu anakula kula zaidi mara tatu kutwa nzima, tumbo lake halijawahi kukosa chakula, hajui njaa mwili umenenepa hafanyi kazi za kutumia karoli kwa wingi mwilini, ni wa kukaa ofisini na kupanda gari tu kumbe angetembea tu hata umbali fulani ingetosha kusambaratisha sukari na mafuta mwilini mwake na mwili ukawa balanced, hiyo haifanyiki. Zamani kula iliendana shuhuli ya kufanya na muda wa kukaa bila kula huku ukiwa kwenye shughuli fulani. Siku hizi kukuta mzee bonge wa miaka 60 na hana changamoto za kiafya mwilini mwake ni nadra sana
Mkuu,

Sasa kama hayo ndiyo maisha mtu aliyoyachagua, hata baada ya kuhutubiwa na Janabi, unataka kumlazimisha kwa nguvu asiishi anavyotaka yeye, aishi unavyotaka wewe?

Na yeye akikulazimisha uishi anavyotaka yeye kulakula kila saa bila mazoezi, utafurahi?

Baada ya kutoa elimu, muwaache watu waishi wanavyotaka. Isije kuwa mnawasema kama kwa chuki, kwa sababu tu wameamua kuishi maisha msivyotaka nyie.

Mkiwasema hivyo, itaonekana
kama mnataka kuwa control maisha yao, na kumbadili mtu hivyo ni vigumu sana.

The right to self determination is paramount, and that includes the right to living unhealthy.

Mbona hata hao madaktari wanakunywa pombe, wanavuta sigara, huku wakijua kabisa madhara ya pombe na sigara?
 
Mtu anakuuliza, kwa nini aishi maisha marefu ikiwa vile vitu anavyopenda kufanya, vile ambavyo anaona vinayapa maisha utamu, anakatazwa kufanya?
Mkuu upo serious kweli? Kwa hiyo wewe unashauri mtu akiwa na maisha ya taabu hata ikibidi ajinyonge ni sawa?
 
Utafiti gani usio na assumptions wala margin of error? Nimekuuliza umekimbia kujibu haya maswali. Utafiti gani huo?

Umefanya utafiti kuhusu nini?

Na Profesa Janabi yuko sahihi 100% kuhusu nini? Unaijua 100% wewe?

Tuanzie hapo kwanza.
Mkuu wewe ni mtafiti kweli au basi tu? Unajua jinsi ya kufanya sampling?
Huwezi kuhoji watanzania wote. Unachoweza kufanya ni kutafuta population sample kwanza. Then unaenda mbali zaidi unapata target population kutoka kwenye population sample. Hii sample ya mwisho sasa ndio unafanyia utafiti based on your chosen variables.

Sasa mimi katika sample niliyofanyia utafiti, wote wameangukia kwenye obesity. Hii ni sawa na 100% of the target population. Ungekuwa ni wewe ungepunguzaje hiyo asilimia ilmradi isifike 100% na kwanini?
 
Tumia chart hii inayoonyesha uhusiano kati ya uzito (y-axis) na urefu (x-axis) kujua BMI yako inakoangukia ili kujifanyia tathmnini binafsi:
View attachment 2860859
Nina kg 66 na urefu ni ft 6.4

So unataka kusema hapo BMI yangu ni 30+ so niko overweight... Mbona bado me najiona kimbau mbau.
 
Mkuu wewe ni mtafiti kweli au basi tu? Unajua jinsi ya kufanya sampling?
Huwezi kuhoji watanzania wote. Unachoweza kufanya ni kutafuta population sample kwanza. Then unaenda mbali zaidi unapata target population kutoka kwenye population sample. Hii sample ya mwisho sasa ndio unafanyia utafiti based on your chosen variables.

Sasa mimi katika sample niliyofanyia utafiti, wote wameangukia kwenye obesity. Hii ni sawa na 100% of the target population. Ungekuwa ni wewe ungepunguzaje hiyo asilimia ilmradi isifike 100% na kwanini?
Mpaka sasa nakuuliza margin of error na assumptions hujajibu.

Profesa Janabi yuko sawa 100% kwenye nini?

Sample yako ni ya watu wangapi? Umeiwekea control gani? Umepata sample ya watu obese 100% Tanzania?

Unajua kwamba unaweza kutafuta watu wanne walio obese, ukafanya research, ukasema umefanya research Tanzania ukakuta 100% wako obese?

Ume avoid vipi selection bias katika research yako?
 
Mkuu upo sahihi ngoja Tusubiri majibu yake.
 
https://www.nhs.uk/conditions/obesity/causes/#:~:text=It's%20caused%20when%20extra%20calories,in%20the%20body%20as%20fat.Hakuna kitu anachozungumza Professor anachokitoa tu kwenye akili zake.Anayozungumza ni yanayozungumzwa na science ya Afya, Kama unaona Janabi anadanganya basi chukua muda hata upitie tovuti za Vyuo Vikuu vya tiba au hospital kubwa maarufu duniani kuhusu ulaji wa hovyo na madhara yake uone kama professor ni Muongo
Profesa yupo sahihi mkuu. Kama unadhani ni muongo, basi ingia field ufanye utafiti. No research, no right to speak.
 
Hakuna kitu anachozungumza Professor anachokitoa tu kwenye akili zake.Anayozungumza ni yanayozungumzwa na science ya Afya, Kama unaona Janabi anadanganya basi chukua muda hata upitie tovuti za Vyuo Vikuu vya tiba au hospital kubwa maarufu duniani kuhusu ulaji wa hovyo na madhara yake uone kama professor ni Muongo
https://www.nhs.uk/conditions/obesity/causes/#:~:text=It's%20caused%20when%20extra%20calories,in%20the%20body%20as%20fat.
Mkuu hii link uliyobandika hapa umeisoma vizuri kweli? Hebu rudia kusoma:
Obesity is a complex issue with many causes. It's caused when extra calories are stored in the body as fat.
 
Nimetumia probability sampling techniques.
Probability sampling technique kivipi? Kwenye sample ya watu wangapi? Umewachaguaje kuhakikisha huna selection bias? Umetumia control gani? Assumptions zako zilikuwa zipi? Margin of error yako ni ipi?

Mbona hujibu maswali? Mtafiti gani unaogopa maswali?

Umefanya utafiti kweli wewe au unatupa chai tu hapa?

Na ukikuta watu 100% ni obese, hilo linamaanisha Profesa Janabi alikuwa sawa 100%?

Unajua kuna tofauti kati ya wewe kufanya research na kukuta watu 100% obese na Profesa Janabi kuwa sahihi 100% ?

Do you understand this simple logical fact?
 
Cha msingi atupe Margin of errors na Assumptions za study yake kwanza.
 
IMG_6036.jpg

IMG_6035.jpg
 
Back
Top Bottom