Niliwahi kuhudhuria send off ya rafiki yangu mmoja. Eti wakati wa mawaidha mama wa mke anasimama na kusema, "baba tumekupa huyu binti hana alama yoyote ya kipigo mwilini mwake. Ikitokea amekushinda au mmeishana tafadhali usimguse, mrudishe tu nyumbani kama ulivyomchukua." Huu ni ujinga mkubwa na ni pigo kuu kwa ndoa. Mwanamke huingia kwenye ndoa mguu mmoja ndani mmoja nje. Hana cha kupoteza kwenye ndoa no matter what happens.
Sasa mimi nilimwambia jamaa yangu, "ingekuwa mimi ndio naoa, ndoa hii ingeishia hatua hii hii ya send off, basi!!" Jamaa hakunielewa kabisa. Usithubutu kuoa mwanamke ambaye wazazi wake hawako radhi kumwacha huru. Huwezi kamwe kujenga familia imara badala yake itakupasa wewe ndio uwe nafasi ya mke kusudi ndoa idumu. Matokeo yake upande wa mwanamke utakuwa na nguvu kwenye ndoa yenu kwa, sababu bila hivyo mke hakai.
Mke bora kabisa ni yule ambaye maisha yake ameyatoa asilimia 100 kujenga ndoa yake. Mwanzoni roho yake iliambatana na wazazi wake, lakini tangu mwanamume alipomwingilia akamtoa bikra, alipanda ndani yake roho mpya ambayo inakwenda kuziba gap lililokuwa likijazwa na wazazi. Sasa amefungamana na mtu mpya, ndio maana binti kabla ya kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza huripoti kwa wazazi kila tukio linalohusu mapenzi. Ila siku akiingiliwa tu, huanza kuficha kila tendo wazazi wasijue, hakuna tena muunganiko. Anaweza hata kubanwa gheto kwa msela kwa siku kadhaa huku wazazi wakihaha kumtafuta.
Sasa ukioa mwanamke wa aina hii, hawezi kuwa na muunganiko wa kweli na mumewe, achilia mbali ukoo wa mume. Kwake yeye wazazi ni kimbilio pale anapoharibu, kwa sababu rohovyake ishavurugwa na wanaume wengi, hivyo ana emotional blur. HAJUI KUPENDA, anategemea mashosti wa Instagram na semina za akina mauki wamfundishe mapenzi ni nini. Amesahau kuwa alitoroka darasani pale wazazi wake walipokuwa wakifundisha kwa mtaala halisi wa malezi, akakimbilia ukahaba. Sasa akiingia kwenye ndoa ataishi kwa experience ya hao wanaume walio tangulia kuwa naye, atamchukukia mume wa ndoa kama WANAUME WENGINE TU. Kwa mtindo huu kwa nini asiimarishe ukoo wake ndani ya ndoa?
Kosea yote, lakini usikosee kuoa, majuto yake ni makuu.
Asante