Utafiti Wangu: Watoto wengi hupenda zaidi ndugu upande wa mama kuliko upande wa baba

Utafiti Wangu: Watoto wengi hupenda zaidi ndugu upande wa mama kuliko upande wa baba

Wkt nko skuli ticha alisemaga mambo ya Patrinial na matrineal society....(cjui nmepatia hata spellings na uzee huu) ,akimaanisha muendelezo wa koo na hata ndugu kuelemea upande mmoja wa familia...yaan unakita watoto wanaelemea upande wa mama..kila kitu kitu,.hii iko kwa nyanda za juu kusini....naa kusin kwa Tanzania..(Matrineal).. Na upande wa kaskazin unakuta watoto wanaelemea kwa baba kila kitu,kuanzia majina ya koo hata kufaham ndugu wa baba zaid kuliko wa mama...(Patrineal)
Swadaktaaa.huku kwetu uchagani tunaelewana sana upande wa mababa.
 
Wkt nko skuli ticha alisemaga mambo ya Patrinial na matrineal society....(cjui nmepatia hata spellings na uzee huu) ,akimaanisha muendelezo wa koo na hata ndugu kuelemea upande mmoja wa familia...yaan unakita watoto wanaelemea upande wa mama..kila kitu kitu,.hii iko kwa nyanda za juu kusini....naa kusin kwa Tanzania..(Matrineal)..
Okay mkuu...
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania kulingana na utafiti wangu;

Kwanini katika familia nyingi watoto wengi hupenda zaidi ndugu wa upande wa mama kuliko wale wa upande wa baba zao?

Ni mara chache sana utaona mtoto wa baba mdogo na mkubwa wanasaidiana.

Mimi licha ya umri wangu huu mdogo lakini nimekuwa nikishirikishwa sana katika kutatua changamoto za kifamilia kwa jamaa na marafiki.

Kwa mfano unaweza kukuta mtu anakaa Dar lakini amepata safari ya kwenda kwenye interview ya kazi huko mkoani Iringa ambapo kuna ndugu wa pande zote mbili.

Kuna ndugu upande wa mama (mama mdogo) pamoja na ndugu upande wa baba (baba mdogo). Ila amini usiamini, asilimia 95% ya watoto watakuwa na furaha zaidi kwenda Iringa na kukaa nyumbani kwa mama mdogo kuliko kwa baba mdogo.

Watoto wa baba mdogo na baba mkubwa wengi wanakuwaga na beefs za hapa na pale tofauti kabisa na watoto wa mama mdogo na mama mkubwa.

Unaweza ukakuta watoto wa baba mdogo/mkubwa wanawweza kukaa hata miaka 2 bila hata kutumiama SMS ya kujuliana hali lakini watoto wa mama yake mkubwa ama mama mdogo wanawasiliana kila baada ya mwezi mmoja.

Nilijaribu kwenda mbali zaidi kutaka kujua chanzo ni nini kutokana na mahojiana na watu wengi wazima walionizidi umri.

Wengi walionipa majibu wanasema kwamba chanzo kikubwa ni kuwa akina mama wanapoolewa katika koo za watu wengine wao ndio wanakuwa chanzo cha kuleta kelele ndani ya koo walizoolewamo (bado sina uhakika na tetesi hii)

Kuna baadhi ya wataalam niliohojiana nao walipata kuniambia kwamba tafiti za kisaikoloji inaonesha kwamba mtoto ni rahisi sana kuamini maneno ya mama kuliko ya baba. Yaaani mama akikwambia kuwa yule mke wa baba yako mdogo amenitukana na kuanzia leo msiende kwao, na kweli watoto watatembelea mkoa huo lakini hawataenda nyumbani kwa baba yao mdogo/mkubwa tofauti kabisa akiambiwa na baba yake.

USHAURI KWA WABABA WENZANGU: Msikubali wanawake mliowaoa wavunje undugu wenu kwa maana nyie mmetoka mbali zaidi tangia mpo wadogo huko kwenu kuliko hao wake zenu mliokutana nao ukubwani.

Wanawake wengi hupenda zaidi kuwavuta watoto upande wa ndugu zao tu. Yaaani unakuta likizo mtoto anapelekwa kutembelea kwa mama zake au bibi mzaa mama tu baaaas, na hapa ndio mwanaume anapaswa kuwa kichwa ngumu na kusimama kama baba wa familia.

Kuna baadhi ya wababa huwa wanawachukua watoto wa nguvu na kuwapeleka upande wa ndugu zao pia ili wazoeleke na huko. Baadhi ya mwanaume legelege unakuta hata watoto wakizaliwa hata kama wapo 4 basi majina yote yanatokea ndugu upande wa mkewe.

NINAOMBA KUKOSOLEWA KATIKA UTAFITI HUU KAMA SIPO SAHIHI.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Kiuhalisia hilo jibu ulilopewa hapo juu ndio lina nguvu Sana kwenye hili, wanawake waolewaji hua ni chanzo kikubwa cha migogoro kwenye familia nyingi
 
Shida iko kwa akina Baba. Unakuta baba hakuna hata siku moja anachukua watoto wako wakasalimie ndugu zako na hiyo inafanya siku wakikutana wanakuwa kama strangers hawana relationship yoyote. Kingine kama mume una uwezo ukioa ndugu za mume sometimes wanamchukia mke hivyo kufanya uhusiano wa watoto na ndugu zao uwe mbaya
 
Kabisaaa halafu wao ndio wanajiona wenye mali. Mzazi hajafa hana hata dalili ya kuumwa ila tayari wanawatangazia akiondoka tu wao ndio wasimamizi hapo chuki lazima ianze
Tatzo ndugu wa upande Wa mzazi wa kiume wanavieleele sana hasa mashangaz watataka wakutawale kama vile wamekuzaa wao
 
Zamani ilikua mwanamke akiolewa anaenda kuishi ukweni na anakua karibu na ndugu wa mwanaume. Huyo mwanamke akielewana vizuri na ndugu wa mwanaume ni connection tosha kwa wanae kuelewana na ndugu hao

Sasa ukute mwanamke anaolewa halafu ndugu wa mwanaume wanaleta chuki ambayo itahamia kwa watoto na vizazi vingi

Mali huleta mifarakano,ndugu wengi wa mwanaume wanadhani mali za ndugu yao ni zao hawajali ana mke na watoto wao wanajipachika hapo wakisubiria mifarakano,misiba wapate chao.

Wanaume wengi wapo busy hasa kazi na michepuko wanasahau kuwapeleka watoto wao kusalimia upande wao

Muda mwingi mtoto anashinda na mama,mtoto akiona mama ana ukaribu na huyu anajisikia amani na kuona huyo mtu pia ni wa karibu nae zaidi.
 
Watoto watakuwa karibu na ndugu aliye karibu na familia (hasa mama)...inatokea wengi wanakuwa karibu na ndugu wa mama kwa sababu ndio hao wanawekwa karibu na mama. Nikiri tu wazi kwamba hata mimi nakuwa comfortable zaidi nikienda kwa dada kuliko nikienda kwa kaka
Kwa kaka yako hupapendi au humpendi wifi yako sababu anaringa😂😂😂
 
Zamani ilikua mwanamke akiolewa anaenda kuishi ukweni na anakua karibu na ndugu wa mwanaume. Huyo mwanamke akielewana vizuri na ndugu wa mwanaume ni connection tosha kwa wanae kuelewana na ndugu hao

Sasa ukute mwanamke anaolewa halafu ndugu wa mwanaume wanaleta chuki ambayo itahamia kwa watoto na vizazi vingi

Mali huleta mifarakano,ndugu wengi wa mwanaume wanadhani mali za ndugu yao ni zao hawajali ana mke na watoto wao wanajipachika hapo wakisubiria mifarakano,misiba wapate chao.

Wanaume wengi wapo busy hasa kazi na michepuko wanasahau kuwapeleka watoto wao kusalimia upande wao

Muda mwingi mtoto anashinda na mama,mtoto akiona mama ana ukaribu na huyu anajisikia amani na kuona huyo mtu pia ni wa karibu nae zaidi.
Ni kufeli tu sababu baba ana jukumu la kuwapelekeni watoto kwa ndugu zake pamoja na mke ili watoto mzoeane na mjuane kwa ukaribu.

Mshirikiane katika mambo mbali mbali ila sasa sikuhizi utamaduni umebadilika kutembeleana watu hawafanyi hio biashara na ndio maana ndugu wa mama wanachukuaga nafasi hasa wajomba maana hupenda sana kuja kumsalimia dada yao.

Binafsi mie nilikuwa naenda sana kwa dada yangu weekends enzi yupo bongo which means watoto wake wangenizoea na kuona huyu ndie ndugu yetu tofauti na ndugu wa baba ambao hawaji mara kwa mara.
 
Daaah mi nawapenda sana ndugu wa baba kuliko kwa mama, yaan najihisi nyumbani zaidi nikiwa kwa ndugu wa baba kuliko kwa mama. Ila sema tu wajomba wanajua kudekeza bwana. Unadekezwa kama mfalme
Ukiona hivyo ujue una ndugu waelewa sana...Hawana matabaka wala u much knows! Maana ndugu wengine miyeyusho sana...hasa kama kuna waliokosea kuoa ndio huleta mipasuko.

Unakuta dingi mkubwa yuko freshi ila mkewe mchoyo kichizi kiasi kwamba mkienda mnaona kama mwaenda kumpa tabu tu. Mnaacha kwenda kabisa.
 
Ndugu wa upande wa Baba huwa ni wenye wivu, hawana msaada, wachawi hawana upendo hawapendi uendelee ila ndugu wa upande wa mama wana upendo na hupenda ueendelee.
Hahahah tatizo linakuwa kubwa kama baba yako ndio mwenye uwezo kuliko wengine wote. Hizo pigo hazikwepeki na mara zote mama yenu ndio anaonekan mtu wa kauzibe 😂😂😂!!!

Ni ngumu sana kushirikiana na watu ambao wako against na mama yenu hata akiwaambia msiache kwenda.
 
Baba yao ni yule aliyefunga ndoa na mama yao. Mkuu, ubaba sio suala la DNA. Ngoja umri wako uongezeke ndio utaelewa unaonekana bado mtoto mdogo sana.
Ndio mkuu. Kwa mfani me binafsi toka niko kadogo nimelelewa na dada angu wa kwanza na mumewe kanisomesha mpaka sasa.
Kiukweli ile kauli ya kumuita shem imepotea mdomoni.
Namuita mzee ila nayo inanipotea .Namuita baba nae anaitika kwa starehe huyo [emoji23][emoji23]
Kwa sababu yeye ana mabinti wawili na ni wadogo sana kwangu wako primary na me ndo jibaba.
Huyu mzee abarikiwe saaana.
One day nitafanya wonders kwa ajili yake.
 
[emoji16][emoji16][emoji16] umenikomalia walah
hahahah we sijui kwann humpendi wifi yako mi unaniuzi kinoma.😂 Hivi dadaangu nae akiwa anakutenga tenga utajiskiaje?

Au wifi yako ni mdogo sana kwako mamii?
 
hahahah we sijui kwann humpendi wifi yako mi unaniuzi kinoma.[emoji23] Hivi dadaangu nae akiwa anakutenga tenga utajiskiaje?

Au wifi yako ni mdogo sana kwako mamii?
Ninao wawili, mmoja ni mkubwa sana kwangu na mwingine ni mdogo sana...ila huyu mdogo hanaga shida sema tu hatujazoeana kiviile
 
Back
Top Bottom