Utafutaji wa kiwanja umenifanya nielewe mwanadamu ni hatari sana

Kuna mwanaJF miaka 2014 sijui alitega thread hapa alitapeliwa kiwanja.
Huyu alipelekwa na tapeli hadi serikali ya mtaa ili kijihakikishia uhalali wa umiliki, kumbe hata ile ofisi ya serikali ya mtaa ni feki imewekwa mwonekano wa ofisi kwa hiyo siku tu.
Kuuziana viwanja serikali ya mtaa ni risk sana coz mnaweza mkauziwa hata watu kumi kiwanja kimoja ,
 
Kuna hivi vinavyotangazwa kila kukicha kwenye maredio vinapatikana mlandizi, bagamoyo, sijui kigamboni na inasemwa ni bei ya chini sana, je uhalali wake upo vipi???

Mwenye taarifa au uzoefu na hili atujuze.
Ni kwamba maeneo hayo thamani ya shamba heka moja ni kati ya laki 5 hadi 1.5milion.

Eka moja ina viwanja zaidi ya kumi ila havizidi 12.

Kwa hiyo, muuzaji ananunua/alinunua eka let say laki 5 na akapima viwanja 10+ vya ukubwa wa 20x20 na anauza Tsh 250,000/=.

Kwa harakaharaka 250,000x10=2,500,000. Kwa hiyo ni biashara yenye faida kwao na ni halisi.

Changamoto ni kwamba pako mbali na mji na kama iwapo mtu una pesa na ukapata muuzaji mwaminifu basi unaweza ukanunua shamba tu ambapo laki 7 unapata heka.

Hapa nipo njiani naenda Vigwaza kuchukua hati ya shamba eka 2 nilinunua milion moja (nilikuwa ninalipia kidogo kidogo laki 2.5 kwa mwezi.

Wezi wapo ila pia wa kweli wapo.
 
Acheni ubahili na ujuaji.

Tafuta Wakili, mlipe akufanyie "conveyancing".

Ukishamlipa wakili atahakikisha unanua kiwanja/nyumba ambayo iko salama kwa kuanza kukufanyia 'official search' (upekuzi wa usalama wa ardhi hiyo kwenye masijala ya ardhi katika eneo husika), mpaka kukuandikia mkataba wa mauziano (au kuhakiki mkataba wa mauziano utakaoletewa).

Wengi wenu kwa ubahili au ujuaji, mnajikuta mnanunua ardhi/nyumba ambazo sio mali halali za wauzaji, au ardhi/nyumba ambazo zimekopewa benki n.k

Nikupe mfano, marafiki wawili waliosoma pamoja walitaka kununua nyumba za ghorofa karibu karibu. Nyumba zikapatikana. Mmoja akatafuta wakili akamlipa amfanyie "conveyancing" from stage A to Z, akamlipa 2M.

Wa pili akaona ile 2M ni pesa nyingi, akaenda kununua hivyohivyo. Baada ya kusaini mkataba na kuhamia, akagundua kwamba ule mkataba wa mauziano alioletewa ulikuwa na "exclusion clause", this is a clause limiting liability to the drawer (drafter of the contract).

Baada ya kuhamiwa akaletewa bili ya maji na umeme jumla 3.2M. Alipomfata muuzaji ili alipe akakataa, akasema haikuwa sehemu ya makubaliano. Kwenda kwa Mwanasheria akaambiwa hivyohivyo, kwasababu mkataba uliandikwa "nyumba inauzwa kama ilivyo". Lakini angemlipa Wakili basi angeongeza clause kwamba "madeni yote yanayohusu nyumba hiyo kabla ya mauziano yalipwe na muuzaji".

Kwahiyo acheni ubahili na ujuaji muepuke hasara zisizo za lazima [emoji28]
Wakili wangu aliuziwa kiwanja hewa, na dalali kwa 25m alitaka kunificha ila wakati wakutoa ushahidi akabidi anifungukii ili apata msaada wangu.......kwa ufupi wizi au utapeli wa aridhi hauna mwenyewe ata majaji wanatapeliwa kila ukicha muhimu katika kununua aridhi ni take your time to pay your money, mhemuko acha kama kuna wateja wengine wanata kukichukua wachukue tu hiyo itakua sio ridhiki yako.......tricky madalali wanao tumia kutapeli ni kukuwaisha kulipa kutegeneza mazingira kwamba kuna wateja wengi wanahitaji hiyo sehemu, wewe just ignore them neenda ukafanye sachi yako kwa wakati wako usiwe na haraka.
 
Me Pana mpumbavu aliniuzia kiwanja ubavu wa nyumba yake baada ya kuondoka kurudi nakuta kamuuzia mtu mwingine na keshajenga kabisa na frem,yaani namuangalia huyu Mzee simmalizi sijui nimpe adhabu gani.
Hata pesa za kurejesha Huwa hawana Mimi nataka niuze nyumbani yake.
Hawa wazee wa kiswahili sijui wanaivunia Nini

Kwanini unanunua uswahilini ndugu?unless umejipanga kweli viwanja style hio mtarogana sana
 
Kiwanja kizuri ni kile unaenda kununua karibu na wenyeji wako. Ndugu rafiki etc. Madalali epuka. Hakikisha muhusika anayeuza hayuko mbali na eneo analo uza. Huwa inasaidia sana.

Wekeza kwenye kupata taarifa zaidi.
Madalali ni wa kuepuka sana. Wengi ndio matapeli. Huwa hawatosheki na vipato vyao
 
Acheni ubahili na ujuaji.

Tafuta Wakili, mlipe akufanyie "conveyancing".

Ukishamlipa wakili atahakikisha unanua kiwanja/nyumba ambayo iko salama kwa kuanza kukufanyia 'official search' (upekuzi wa usalama wa ardhi hiyo kwenye masijala ya ardhi katika eneo husika), mpaka kukuandikia mkataba wa mauziano (au kuhakiki mkataba wa mauziano utakaoletewa).

Wengi wenu kwa ubahili au ujuaji, mnajikuta mnanunua ardhi/nyumba ambazo sio mali halali za wauzaji, au ardhi/nyumba ambazo zimekopewa benki n.k

Nikupe mfano, marafiki wawili waliosoma pamoja walitaka kununua nyumba za ghorofa karibu karibu. Nyumba zikapatikana. Mmoja akatafuta wakili akamlipa amfanyie "conveyancing" from stage A to Z, akamlipa 2M.

Wa pili akaona ile 2M ni pesa nyingi, akaenda kununua hivyohivyo. Baada ya kusaini mkataba na kuhamia, akagundua kwamba ule mkataba wa mauziano alioletewa ulikuwa na "exclusion clause", this is a clause limiting liability to the drawer (drafter of the contract).

Baada ya kuhamiwa akaletewa bili ya maji na umeme jumla 3.2M. Alipomfata muuzaji ili alipe akakataa, akasema haikuwa sehemu ya makubaliano. Kwenda kwa Mwanasheria akaambiwa hivyohivyo, kwasababu mkataba uliandikwa "nyumba inauzwa kama ilivyo". Lakini angemlipa Wakili basi angeongeza clause kwamba "madeni yote yanayohusu nyumba hiyo kabla ya mauziano yalipwe na muuzaji".

Kwahiyo acheni ubahili na ujuaji muepuke hasara zisizo za lazima [emoji28]
Samahani mkuu?

Mfano namunua kiwanja cha mil 4

Wakili ili anisimamie nimlipe shingapi? Kiwanja kisicho na hati..
 
Me Pana mpumbavu aliniuzia kiwanja ubavu wa nyumba yake baada ya kuondoka kurudi nakuta kamuuzia mtu mwingine na keshajenga kabisa na frem,yaani namuangalia huyu Mzee simmalizi sijui nimpe adhabu gani.
Hata pesa za kurejesha Huwa hawana Mimi nataka niuze nyumbani yake.
Hawa wazee wa kiswahili sijui wanaivunia Nini
Mm kila nikinunua napiga Uzio wa tofali kesho yake naandika hakiuzwi epuka matapeli
 
Biashara yeyeto ufanyayo na mbongo kuwa makini sana.
We check mfano watendaji wanajua kabisa ili eneo Sio na wanashiriki vizur na muuzaji huku wakijua ili wapate tu asilimia 10.
Nenda kwenye show room za magari usipokuwa makini unauziwa body engine wanachomoa wanaweka ya temeke, ofisin wanadocument zote ukutani kumbe ni feki ingia mkataba uone,

Mswahili katu hawezi endelea udhani ujanja kupiga kumbe anajilaani inaweza isikupate wewe ukashangaa mbona watoto hawaelewiki
 
Acheni ubahili na ujuaji.

Tafuta Wakili, mlipe akufanyie "conveyancing".

Ukishamlipa wakili atahakikisha unanua kiwanja/nyumba ambayo iko salama kwa kuanza kukufanyia 'official search' (upekuzi wa usalama wa ardhi hiyo kwenye masijala ya ardhi katika eneo husika), mpaka kukuandikia mkataba wa mauziano (au kuhakiki mkataba wa mauziano utakaoletewa).

Wengi wenu kwa ubahili au ujuaji, mnajikuta mnanunua ardhi/nyumba ambazo sio mali halali za wauzaji, au ardhi/nyumba ambazo zimekopewa benki n.k

Nikupe mfano, marafiki wawili waliosoma pamoja walitaka kununua nyumba za ghorofa karibu karibu. Nyumba zikapatikana. Mmoja akatafuta wakili akamlipa amfanyie "conveyancing" from stage A to Z, akamlipa 2M.

Wa pili akaona ile 2M ni pesa nyingi, akaenda kununua hivyohivyo. Baada ya kusaini mkataba na kuhamia, akagundua kwamba ule mkataba wa mauziano alioletewa ulikuwa na "exclusion clause", this is a clause limiting liability to the drawer (drafter of the contract).

Baada ya kuhamiwa akaletewa bili ya maji na umeme jumla 3.2M. Alipomfata muuzaji ili alipe akakataa, akasema haikuwa sehemu ya makubaliano. Kwenda kwa Mwanasheria akaambiwa hivyohivyo, kwasababu mkataba uliandikwa "nyumba inauzwa kama ilivyo". Lakini angemlipa Wakili basi angeongeza clause kwamba "madeni yote yanayohusu nyumba hiyo kabla ya mauziano yalipwe na muuzaji".

Kwahiyo acheni ubahili na ujuaji muepuke hasara zisizo za lazima [emoji28]
Akili ya kutafuta viwanja siyo lazima wakili ambaye ni zao la bookish Schools.

Wakili naye anatafuta chakula tena kwa gharama zilizo juu na ufanisi zero
 
Mm kila nikinunua napiga Uzio wa tofali kesho yake naandika hakiuzwi epuka matapeli
Mimi huwa ninapasafisha napanda miti, nachimba mashimo ili mradi mtu akija aone kuna mtu na anakuja muda usiojulikana kwa hiyo hawezi kuuza au kama kina ugomvi utajua tu maana utasikia mtu anakuuliza kwanini unachimba hapo au nani kapanda miti
 
Samahani mkuu?

Mfano namunua kiwanja cha mil 4

Wakili ili anisimamie nimlipe shingapi? Kiwanja kisicho na hati..
Wengi wanachukua kwa asilimia kadhaa , nafikiri yeye ndo anakuambia anataka asilimia ngapi.

Mi mambo ya viwanja nimeachana nayo maana utapeli ni mwingi ,ila nataka kuanzia 700m² maeneno kibada au gezaulole.
 
Back
Top Bottom