Utaifa wa Tanganyika umeanza kukua kwa kasi, kuna hatari ya kuzuka mgogoro wa Kijamii, Serikali 3 ni sasa

Sisi kizazi cha leo hatutakubali ujinga wenu. washenzi kabisa ninyi wazee wachawi.
Mkuu Mnyama, Mnyama wa DM , heshima ni kitu cha bure, uungwana na ustaarabu, tofauti zetu za mitazamo zisikufanye unitukane mjinga, mshenzi na mchawi!, jf tumepoteza members wengi wasio na ngozi ngumu, ambao wanashindwa kuvumilia kutukanwa hivi na wengine usikute ni vitoto au vijukuu!.
P
 
Umesema wako wengi zaidi ya wazanzibar sasa si watawamudu tu.
 
 
Na huo ndio mtego wenyewe ambao mtu mwenye akili timamu anatakiwa aone hatari yake.

Watanganyika wakifanya fujo kwa Wazanzibari na Wazanzibari wakilipa kisasi, faida yote ya muungano inaisha maana.
 
Hakuna maandamano yoyote 7/7 , huu muungano wetu adimu na adhimu, hauvunjikiki, tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
Wewe unaona huu muungano uko sawa kabisa.baadhi ya watanganyika mnaturudisha nyuma kuikomboa Tanganyika inayonyonywa na zanzibar.Nchi kubwa kama uingereza iliamua kujiondoa kwenye umoja wa ulaya baada ya kuona watu wake wananyonywa lakini baadhi ya watanganyika mnajifanya hamuoni matatizo ya huu muungano wa kihuni.
 
Watu wakishaanza kuandamana hakuna namna unaweza kuzuia labda uwape matakwa yao.
Ili ukomeshe labda ua gen z wote if not jambo hilo haliepukiki.
Hawa watu wataandamana tena hata kama sio mwaka huu
 
Serikali iwe moja ama mbili za Ukweli Ukweli! Tatu hapana
 
hakuna jipya,,,, baada ya 2030 hutoona tena hizi kelele.. ni huu mrundikano wa waliovuka maji kwenye nyadhifa nzito za serikali ya Tanganyika ndo inawauma watu..
 
Serikali iwe moja ama mbili za Ukweli Ukweli! Tatu hapana
Serikali 2 hazina tija yoyote, ndiyo zimetufikisha hapo. Suluhu ni Serikali 3 sawa na mapendekezo ya Rasimu ya Katiba ya Warioba, kama hamtaki bora kuvunja
 
hakuna jipya,,,, baada ya 2030 hutoona tena hizi kelele.. ni huu mrundikano wa waliovuka maji kwenye nyadhifa nzito za serikali ya Tanganyika ndo inawauma watu..
Nimetoa Tahadhari ya kiusalama.

Wanaoandamana na kupanga maandamano vijana waliozaliwa mwaka tuliopitisha vyama vingi na kuendelea. Ni kizazi kipya kabisa. Kinachanga moto mpya
 
Nimetoa Tahadhari ya kiusalama.

Wanaoandamana na kupanga maandamano vijana waliozaliwa mwaka tuliopitisha vyama vingi na kuendelea. Ni kizazi kipya kabisa. Kinachanga moto mpya

Hivyo vizazi vipya vimepita vingi mzee,,, hata mfumo nao ni mpya.. mfumo uliomfumua Mrema 1995 na Lowassa 2015 ni tofauti na huu ulitufumua 2025 ila wenye mfumo ni wale wale..

Hao wanaosema wataandamana ni kelele tu,,, waache kusumbua watu watulize mihemuko,,, wajaribu kufikiri zaidi ya screen wanazotazama wauone uhalisia ..
 
Hivi JF mnavyoruhusu threads km hizi mnategemea nini? Futeni nyuzi za kipuuzi km hizi hazina maana yyte ni upumbavu wa mtu moja au watu wachache ambao wengi wako nje ya nchi waliojawa roho za kishetani wasiotaka kuona watu wakitulia kufanya mambo yao ya kimaendeleo
 
Kelele zote hizi zitazimika mara akiingia Rais Mroman, baaas
 
Angalia wanarejelea vurugu, ghasia, uhalifu wa tarehe 29 km vile ni mafanikio kwao, maana yake hawa ndio walioandaa, kuratibu, kufadhili na kutekeleza ule upuuzi. Vyombo vya ulinzi na usalama msilale tena tunataka tuwaone hawa watu, tuwajue wako ndani au nje ya nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…