Utaifa wa Tanganyika umeanza kukua kwa kasi, kuna hatari ya kuzuka mgogoro wa Kijamii, Serikali 3 ni sasa

Kwani Imeanza leo ndugu, na kwanini mpka wa subiri tarehe flani? We are powerless, hatuna guts na hakuna chochote tutafanya
Inawezekana hiyo tarehe 7 kusiwepo na hayo maandamano, lakini hizo hamasa lazima zitaleta maandamano soon. Niliianza kuona hamasa za maandamano wakati wa operation ukuta na hayakutokea, lakini hiyo hamasa ilikaa akilini mwa watu. Yakaja ya hamasa ya Mange nayo haya kufanyika baada ya vyombo vya dola kujazana mitaani. Ikafika wakati wa uchaguzi wa 2020 watu wakakosa ujasiri kidogo lakini hayakutikea ila yalikuwa yatokee. Hamasa ile ikabaki akilini mwa watu.

Hatimaye juzi 2025 yakatokea hadi leo hakujakaa sawa, na wananchi taratibu uoga unapungua, na wanaamini maandamano yataleta mabadiliko. Tunza hii post, mama Samia hamalizi miaka yake mitano bila maandamano makubwa, na hapo ndio utakuwa mwisho wa ccm iwapo hakutafanyika mabadiliko ya kweli.
 
Pascal Mayalla
Hapo chini ni moja ya video za Vijana wa Gen-Z kuonyesha moja ya operation zao.

Kijeshi ama kiusalama wanaweza kuitwa "saboteurs or clandestine operatives" kama vyombo vya Usalama vina chambua taarifa na kutoa Ushauri kwa mamlaka husika lazima ziwashauri Kuwa hali ya kisiasa imebadilika sana na ni hatarishi.

Katika hivyo vipeperushi, fikiria wakiamua kubadilisha utaratibu na kufanya operation kimya zaidi, fikiria hivi vipeperushi vimesambazwa na maneno ya kudai uhuru wa Tanganyika na kuwatenga Wazanzibari kwenye maeneo wanayoishi.

Lakini si hili tu la vipeperushi kama hizi organization wanafanya wakitumia mitandao, fikiria mambo wanayoweza kufanya kwenye mtandao wakiamua kwenda mbali zaidi, kama kuprint Drone, Bunduki au kushare blueprint za kuunda silaha, au vilipuzi.

CCM wasipoona hili kwa uzito basi wajue ni sikio la kufa.

Anayepuuzia uwezo wa kizazi hiki kwenye kupanga mipango ni kipofu.

Your browser is not able to display this video.
 
With this, nakubali it will add up with time.
Ila by now we should accept our place.

Hata kipindi cha utumwa kilitumia muda Sana Kuja kuisha
 
Hii taarifa ni nzuri kwa watu wa zanzibar kuliko watu wa bara
 
Zanzibar kuwa na serikali yao siyo tatizo ila Tanganyika kuwa na serikali yao ni tatizo.
Ni swala la muda Tanganyika kurudia hadhi yake ya nchi.
 
Sasa zanzibar inakila kitu hadi raisi wake kwanini isijitenge tu
Maana za chinichini abed alilaimishwa tu na nyerere alikuwa hataki muungano
 
Sijawahi kujua shida iko wapi kama TANGANYIKA kukawa na Serikali yake, very simple kuna kuwa na clear demarcation
 
Ila tuseme kaukweli haka jamani, Tanganyika ina raha yake kuwepo, ni vile tu basi hakuna namna.

Si unajua raha ya kuwa huru bila hofu ya kubaguliwa, kutukanwa kulalamikiwa na majirani mnaopakana mto, au ukuta. unajikuta unanenepa bila kujua.
 
Warudi tu Tanganyika.

Wameenda kuzurura na kuacha mapori, madini yanaibiwa na mbuga za wanyama zinaporwa badala waje tusaidiane kulinda.

Wanabanana tu hapo tarafani unguja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…