Utajuaje kama huna nafsi au umeuza nafsi

Reincarnation tena? kaka unajaza madude mengi kichwani ambayo hayana faida.Tumia muda wako wisely.
 
Mkuu tufafanunulie kwanza tofauti ya nafsi na roho.
Roho ni pumzi ya uhai uliyonayo ambayo ikiachana na mwili wako, unakufa yaani unaitwa maiti.

Nafsi ni kile kinachoumiliki mwili wako. Kwa mfano, roho ikishatengana na mwili, unakuwa maiti halafu hiyo maiti inaitwa "mwili wa fulani", huyo fulani anayeumiliki huo mwili, ndiyo nafsi. Najua unaweza kusema hapa kuwa hiyo "fulani" inawakilisha jina la mwenye mwili na hivyo kuanza kufikiria kuwa pengine nafsi ni sawa na jina la mtu; hapana.

Jina ni kiwakilishi tu cha nafsi kama LEBO ya nafsi kwa sababu zipo nyingi kusaidia watu wasichanganye nafsi moja na nyingine kutokana na ukweli kuwa kila mtu ni nafsi. Kwa hiyo ili tuweze kutofautisha nafsi moja na nyingine, tunazipa majina. Kwa hiyo majina ni viwakilishi vya nafsi, vinavyoweza kutusaidia kutoutisha nafsi moja na nyingine. LEBO hizi huwa siyo pamanent na ndiyo maana leo naweza nikaamua niitwe Makanyaga, halafu kesho tena nikaamua niitwe dumbi.

Vile vile LEBO hizi huwa hazina tabia ya kujitambulisha zenyewe kwenye mazingira mageni, ila nafsi yenyewe huwa inajitambulisha popote pale itakapokuwepo bila kujali mazingira kwamba iko uugenini au nyumbani.

Kwa mfano, wewe huko uliko Ulaya muda huu, tuseme ukiamua kusafiri kutoka huko na kurudi huku nyumbani kwenu Tanzania halafu ukafikia Moshi ambako siyo kwenu na watu wa huko Moshi hawakujui, (tuseme labda kwenu ni Mbeya), the moment umefika Moshi watakaokuona wataanza kusema kuwa yule ni MTU, thapa ayari nafsi yako inakuwa imejulikana. Baada ya hapo, itabidi sasa wakuulize JINA lako ambayo ndiyo LEBO YA NAFSI YAKO. Jina unaweza hata ukawadanganya ukawaambia unaitwa JOHN, wakati kumbe wewe ni MICHAEL.

Tofauti na ilivyo kwa nafsi, watu hawahahitaji kukuuliza kwamba wewe ni mtu, huwa inajitambulisha yenyewe na pia huwezi ukawadangaya kama ilivyo kwa jina, kwamba uwaambie kwamba wewe ni kondoo, na si mtu, haiwezekani kwa sababu nafsi ina mamlaka ya kujitambulisha yenyewe, haihitjai wewe uitambulishe. Wewe unayo mamlaka ya kutambulisha LEBO yako tu basi na hiyo ndiyo una uhuru nayo kwamba unaweza hata ukaamua kudanganya juu ya LEBO yako. Tuko wote?
Mifano zaidi:
Mkono wangu unauma-----hii inamaanisha wewe siyo mkono
Kichwa changu---------- inamaanisha wewe siyo kichwa
Mwili wangu-----------------inamaanisha wewe siyo mwili, WEWE NI NAFSI, labda iliyopewa LEBO JOHN, baada ya kuzaliwa!
Ubarikiwe
 
Umetaja Adam, ukataja na Hawa kama creation,swali hapa, ni kivipi uliweza kuwafahamu Adamu na Eva kama si creation theory unayesema kwako si kitu.

Au we mwenzetu Adam na Eva unao wasemea hapa umewapata sehemu gani?
 
Jamaa anazingua kuna vichaa ukiwazingua wanakuzingua hutaamini.
 
Asante sana nimeelewa sana shukrani kwa kuopoteza muda wako kwa hili, maana hakukuwa na jibu linalleleweka hapa umesaidia wengi sana.
 
Fantastic
 
Ebu Ni fafa nulie ao MUNGU wawili kwenye dini izi za ki kristo na uislam please [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hahahahha hebu dadavua hapa maana wenyewe wanaitaga kusafiri😅 af mie nahisi wanga ni meditators wazuri sana maana wanaacha vitanda wanaenda kuingia kwenye manyumba ya watu huko!
Ni story ndefu kidogo lakini kwa kifupi tu ni kuwa nilikuwa nimejilaza kitandani mida ya 7 hivi usiku sina hata usingizi, ndio wazo la kifanya meditation likanijia.

Basi nikaanza ile process ya kuituliza akili, baada ya km dakika kumi hivi nikaanza kuhisi km nimepata huzuni kubwa ya ghafla( ile huzuni unayoipata baada yakupata taarifa kuwa ndugu yako wa karibu amefariki) na kitu km ganzi inapanda kutokea miguuni hadi kichwani na inavyopanda naisikia kabisa inavyopanda.
Nikaanza kupaona pale kitandani apalaliki tena, nikaona km nikishuka kitandani ndio nitapata unafuu, nikashuka kitandani nikawa nazunguka zunguka pale chumbani ila bado haikusaidia, nikahisi km nikitoka nje ndio nitakaa vizuri, nikatoka njee puuu puu km kichaaa lkn wapi amna unafuu ile ganzi bado naisikia na ile huzuni ya moyoni bado ipo nikaanza eti kukemea kwa jina la Yesu kwa jina la Yesu shindwa 😂😂😂 lkn bado; nikahisi labda nikitoka nje ya geti yaani nitoke barabarani kabisa labda ndio nitapoa, nikaanza safari ya kwenda getini lkn nikiwa naelekea getini likanijia wazo kuwa nikanywe maji ya baraka(catholic wanayajua), nikarudi ndani nikaenda kuyanywa, baada ya kuyanywa tu lile wenge la kukimbia kimbia likatulia ikabakia ile huzuni kubwa moyoni na ganzi mwilini ila sasa hivi ilipungua kidogo.

Usiku ule nilifanya au kuhisi vitu vizuri vizuri ili ile huzuni initoke lkn wapi, nikarudi kitandani kulala, kila nikijaribu kufunga jicho nilale naisikia ile ganzi inapanda kutoka miguuni hadi kichwa na km kuna nguvu fulani hivi zinanitoka mwilini, nikasema kwa hali hii nikilala tu nitafia usingizini nikawa najitahidi nisilale. Nikaja kupitiwa na usingizi saa 9 usiku na hata sikulala sana km nusu saa tu nikastuka yaani mwili wote umelowa jasho yaani hadi mashuka hayafai, nikaja kupata usingizi saa 12 kasoro asubuhi.

Ile hali ya huzuni na ganzi mwilini iliendelea kunitesa, yaani amna kitu chochote kilichokuwa kinanipa furaha hata nifanye nini yaani nikawa nahisi kufa kufa tu, nikisikia mtu kafariki nasema afadhali yake kafa kaenda kupumzika nakumbuka ilikuwa ni kipindi kile kingunge amefariki.
Nilikuwa najiepusha sana kukaa karibu na vitu km kisu au mapanga coz nilikuwa najua akili yangu haipo sawa na roho ya mauti ilivyokuwa inaniandama.

Ni vitu vingi vingi vilitokea ndani ya hiyo wiki moja ya huzuni na ganzi mwilini, kilichoniponya niliamua kutafuta faraja kwa kusoma Bible na niliikazia sana zaburi ya 26, niliisoma zaidi ya mara 10 kwa kuirudia rudia nikaanza kuona ile hali inaaondoka saa ile ile na niliweza kurudi kwa hali yangu ya kawaida.

Nakumbuka nilikuja kumuuliza Mshana Jr kuhusu kufanya meditation usiku mkali, akasema sio vizuri kuifanya mida hiyo coz usiku kuna maroho mengi machafu yanaranda randa hovyo.

MEDITATION SIO YA KUICHUKULIA KIRAHISI RAHISI KAMA TUNAVYODHANI
Abigail Nabal
kilwakivinje
 
Ungekunywa chai ya karafuu ungepona haraka sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…