Utakatishaji Fedha, Biashara inayoendelea kwa Siri kubwa

Watu wa Sembe wameguswa hapa ..eti hawaelewi alichoandika mtoa mada.
 
Wewe umeshawahi kutakatisha?
WIVU TU
fanya kazi.....acha porojo
 
Wewe umethibitisha ulichoongea maana pia umeandika taka taka na jinsi gani kichwa chako kilivyo na akili mbovu kuwahi kutokea.
 
Umesema vyema ila kuna watu leo hii nchini wanatumika kutakatisha fedha na serikali ipo kimya. Mtu anaonyesha hela kwenye mtandao akidanganya watu yeye ni free madon
 
Mimi nimekuja kufahamu hapa bongo mtu mwenye hela nyingi au mwenye cheo kikubwa hawapendwi bila kusahau watu wenye elimu kubwa nao wanaambiwa elimu yao nifeki na haina maana hawasaidii nchi n.k.
 
Sasa unahitaji taaluma ya ujasusi kweli hapo kubaini kuwa kuna mianya ya kutakatisha pesa za watu wengine? Au hata zake alizotengeneza kwenye Illegal business zake nyingine?
Au hukumuelewa anyway sio wote tunafaa kuchunguza matukio.
Yeye alipowataja tu hao watu nikaona ni kwa namna gani wanatekeleza hilo jambo iwe ni pesa zao au wamepewa !!
 
Mnaosema hamjamuelewa mtoa mada..mko serious kweli au mnatanua mbona hata hahitaji akili kubwa sana:
1.Mtu anajifanya mtumishi wa Mungu: Anasema anapaka pes kwenye sadaka na kuuza maji - na huwezi verify - kumbe anauza madawa ya kulevya..pesa yake ndo anaitaja kama kaipata kwenye sadaka - bila kuwa na kanisa angeshindwa kuhalalisha matumizi makubwa..mfano apeleke bank nillion 3 watamuuliza source ya hizo pesa anasema sadaka na watu wanaona kanisa lipo na watu wanajaa wanakubali.
2.Wafanyabishara: Mtu anakiduka smart cha level ya kawaida mfano anauza simu lkn matumizi yake siyo ya mchezo ukimuuliza anakujibu si ninauza simu..kumbe ile gelesha tu..kipato kinatoka kwingine kabisa.
3.Msanii: Show chache mapesa mengi..kumbe gelesha tu...anajilipa kwa pesa haramu na anaweza kwenda kuzitumbukiza bank -kumbe kapush mzigo...
N.K
 
Kwa lugha rahisi, Unakuta mtu kafungua fremu Mwenge anaweza akagonga mwezi asiingie mteja hata mmoja ndani, Faida 0% ila nyuma ya pazia ni kupoteza maboya tu ana bizness nyengine chafu ili ile ya frem ionekane kama ndo chanzo cha kwanza cha mapato.
 
Drug dealer hatakiwi kuwepo hapa
Bank moja ulaya Hongkong and Shanghai Banking Corporation Limited walipigwa fain ya 1.9 b usd kwa kusindwa kuwazuia CARTEL WAKUBWA WA COLOMBIA NA MEXICO ku launder hela kupitia hiyo benk, KIMSING WAUZA MADAWA WANAONGOZA KWA SHUGHULI YA KUTAKATISHA FEDHA, mleta mada hajakosea wakuu, Top ten money laundering scheme in histori ina Wauza Ngada wengi kuliko watu wengine wowote.
 
Umepata hela chafu unaenda kuinunua nyumba alafu unakaa after sometime unaiuza tena ile nyumba then hii hela inakuwa justifiable hata ukiulizwa umepata wapi pesa unasema uliuza nyumba ilokuwa yako, kuna stail nyingi za kutakatisha fedha. Nakumbuka kuna jamaa alikujaga hapa jukwaani kuuliza namba ya kuvusha dolla laki 9 kama sio M1 kuja tanzania kutoka marekan sababu hawez weka hiyo hela benk na hawez kusafiri nayo akawa anataka apewe mawazo ya namna gani hiyo fedha ataifikisha bongo land kwa namna yeyote, ukisoma ule uzi ndio utajua watu wanavyosafisha fedha aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…