Ng'wanamangilingili
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 5,778
- 4,859
Hujui chochote kuhusu simba wewe itakua unaangalia life za simba NatGeo tu ama channels zenu za kiarabu, watu tumechunga maporini misitu minene tena huko huko biharamulo na chato na mnakutana na simba na wanakuja kila leo kuvamia ng'ombe na mbuzi.Na huko watawamaliza Sokwe wote wa Mlima virunga!
Simba Hawaii kwenye Misitu minene kama ya Biharamulo, Gombe au Virunga. Wanaishi sehemu zenye mvua chache, nyasi ndefu na vichaka vya hapa na pale.
Sasa Burigi Chato itakuwaje? ....Mungu tupe Maarifa zaidi ya Matamanio ya mioyo yetu.
Kama swala ni utaalamu tu na kwamba wao ni wajuzi wa mambo basi wataalam wa siasa na elimu wasingetufikisha hapa katika maswala ya elimu na siasa!Hao wanao wapeleka huko ni wataalamu wa wanyama nina imani wanajua wanachokifanya.
Nikusamehe tu kutokukujibu kwa sababu umefubazwa na mapenzi na ushabiki zaidi ya uhalisia.Hujui chochote kuhusu simba wewe itakua unaangalia life za simba NatGeo tu ama channels zenu za kiarabu, watu tumechunga maporini misitu minene tena huko huko biharamulo na chato na mnakutana na simba na wanakuja kila leo kuvamia ng'ombe na mbuzi.
Ila hata huko unakoangaliaga atleast ungesema ulishawahi una simba wa jangwani, lions of namib desert.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mhadzabe hata kama unashinda porini usinisamehe nijibu tu, sina ushabiki ni hisia zako naongelea uhalisia nasi hisia.Nikusamehe tu kutokukujibu kwa sababu umefubazwa na mapenzi na ushabiki zaidi ya uhalisia.
Laiti ungekuwa unanijua au ungepata picha ya hapa nilipo muda huu ungeona aibu na kufuta ulichokiandika.
Ila kwa kuwa akili zetu watanzania tuliowengi ni mfano wa huu mtazamo wako, nakustili tu mtanzania mwenzangu.
Itapendeza wakiwahamishia wamasai huko ili kuongeza mvuto!Chato haiwezi kuwa na mvuto hata kwa cosmetics!!
Nakubaliana na wewe.Mhadzabe hata kama unashinda porini usinisamehe nijibu tu, sina ushabiki ni hisia zako naongelea uhalisia nasi hisia.
Ukiandika humu nyuma ya keyboard usi'assume kuwa mawazo yako ni sahihi ndio maana tumo humu kubadilishana mawazo
Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya siasa na elimu third world kila mtu mtaalamu.Kama swala ni utaalamu tu na kwamba wao ni wajuzi wa mambo basi wataalam wa siasa na elimu wasingetufikisha hapa katika maswala ya elimu na siasa!
Hahahahaha Mkuu kila kitu ukikiomea, ukakifanya kwa muda mrefu, ukapata uzoefu nao jambo hilo huwa jepesi kwako na kustajabisha wasio na uzoefu na elimu au ujuzi nalo.Mambo ya siasa na elimu third world kila mtu mtaalamu.
Hila kitendo cha kwenda kumkamata Simba inataka umuelewe kweli kweli; ukitaka kujua angalia taarifa ya habari ya jana ITV kupitia you tube channel yao uone askari wa kawaida mwenye bunduki aliesimama karibu na cage Simba alipogonga cage alivyoruka. Halafu linganisha na huyo jamaa TAWA mtaalamu Simba alivyokuwa anatishia nyau alivyokuwa anamwangalia tu.
Anyway binafsi kwakuwa my knowledge is limited nasoma tu perspective zote na ku absorb inaonekana kuna watu wana address serious concerns kwa uzoefu wao sasa nani anajua zaidi sijui; hila personally I’ll take an expert word anytime wherever possible isipokuwa tu pale chui sijui atakapoingia ndani ya gari akaniambia nitulie awezi fanya kitu kwa kweli sijui itakuwaje.
It seems you know more; thanks for your perspective.Hahahahaha Mkuu kila kitu ukikiomea, ukakifanya kwa muda mrefu, ukapata uzoefu nao jambo hilo huwa jepesi kwako na kustajabisha wasio na uzoefu na elimu au ujuzi nalo.
Hili swala la kuwapeleka Simba Chato halina ubaya kwa sababu unaweza ukawapeleka popote provided umewawekea mazingira rafiki kama ya asili wanapotoka. Ndio maana hata Oman, Dubai, Norway China hata Bahrain wana zoo ambazo unaweza kukuta Simba wapo.
Shida itakuja je watakuwa na tabia na uzaliano uliobora kama walivyokuwa katika maeneo yao ya asili? Na je rate yao kuzaliana itakuwaje?
Kwa Chato kama nilivyosema awali wataishi lakini kwa gharama kubwa za uangalizi, na labda with due time watakuwa na kizazi cha Simba hybrid kitabia tofauti na wale wa asili kwa sababu ya artificial environment waliowekewa!
Ulivyo comment awali ulionesha ni kiasi gani unasukumwa na hulka za kishabiki na ndio maana ulijivimbisha na kumwambia Mhadzabe hajui lolote, sasa jamaa anaonekana ni mjuvi wa hayo mambo zaidi yako ambae unaonesha ni mfugaji usie na elimu ya maisha ya wanyamapori, na akaamua kukusamehe, usidharau mtu usiemjua, hilo ndio tatizo lenu team LumumbaMhadzabe hata kama unashinda porini usinisamehe nijibu tu, sina ushabiki ni hisia zako naongelea uhalisia nasi hisia.
Ukiandika humu nyuma ya keyboard usi'assume kuwa mawazo yako ni sahihi ndio maana tumo humu kubadilishana mawazo
Sent using Jamii Forums mobile app
Mpaka serikali hii iondoke madarakani tutashuhudia vituko vingi saanaSimba wakianza kuvamia nyumba za watu wasitishie watakaoweka clips mitandaoni. Maana hicho ndicho kitakaxhofuatia
Infrastructure bado haziko sawa sawa sana upande ule. Ila Tanzania ina opportunities nyingi kila upande. Nafikiri nia isiwe kuangalia Chato tu. Naamini mambo mengi ni ya kupita, ila Tanzania itaendelea kuwepo tu. Tabora, Kigoma na Katavi au hata Mbeya kuna vivutio.Nadhani wanasiasa wanafikiri wataweza kuifanya Burigi Chato sawa na Serengeti au Tarangire.
Ukweli mchungu kuuza safari kanda ya kaskazini ni rahisi zaidi kwasababu mbuga zote maarufu zipo karibu na nirahisi kumshawishi mteja kwenda huko.
Ukishuka Kilimanjaro Airport unakutana na Kilimanjaro National Park 20 kilometer,ARUSHA National Park 30 kilometers,Tarangire 70 kilometers,Manyara 70 kilometer,Ngorongoro & Serengeti 130 kilometers Hii ni parkage moja katika eneo moja.
Rubondo,Kitulo,Mahale & Gombe zipo muda mrefu lakini hazimo miongoni mwa hifadhi zinazoingiza mapato.Zipo kwasababu ya ruzuku from others Park kama Kilimanjaro,Serengeti & Ngorongoro.
Hao simba walio kuwepo wakaenda wapi?Sishabikii mbuga ila natoa taarifa kuwa Simba walikuwepo kabla ya barabara za Muleba Biharamulo na Muleba Chato kuwekwa lami. Wanaoifahamu barabara ya Muleba Biharamulo kuna mlima unaitwa mlima wa Simba.