Utambulisho wa "Wakili Msomi" kwa Mawakili au wanaSheria

ukienda shule wewe ni msomi.

kama inakuuma nenda kasome sheria na wewe ujiite wakil msomi hatutakuuliza
 
Hivi kwanini kila wakili siku hizi anaitwa wakili msomi? Utasikiaa ooh wakili msomi Jebra Kambona, mara wakili msomi Fatma Shomari. Hii ina maana gani hasa katika nchi ya watu wazima kama yetu? Si aina ya insanity hii?
Asante sana. Naomba nikupe kwa ufupi tu. Uanasheria ni kada za kitaaluma kama ualimu, udaktari, uhandisi (wa aina aina), uaskari, siasa nk.
Uanasheria kama kada zingine ina misamiati (terminologies) mbalimbali za kiueledi, sifa, heshima, upambanuzi nk.
Uanasheria unayo namna yake ya uandishi wa lugha tofauti kabisa na weledi mwingine. Waweza kupata shida kuelewa kama si mweledi mwenza. Lugha yaweza kuwa (kiingereza) ya mizunguko mingi, ngumu, yenye utata au hata kukuhamisha kifikra usipokuwa makini.
Sasa basi, kama nilivyotanabaisha hapo juu, kila weledi una lugha yake. Kwa mfano, unaposema /andika neno socket mweledi wa elimu ya viumbe ana maana yake na mjuvi wa elimu ya fizikia akawa na maana yake.
Turudi kwenye mada, wanasheria kujiita "wasomi" ni lugha ya staha, kujali, kukweza, kutambua na kumuweka msomi mwenza katika hoja. Ni kama vile mmoja kumuita mwenzake daktari bingwa. Utakaa unajiuliza :Hivi binadamu gani aliwahi kuwa bingwa wa magonjwa haya yanayoua kila siku hadi mengine tunaambiwa hayana tiba?
Wakati haujaweka mwili sawa kutafakari, nakuongezea tu ya kwamba neno "Wakili msomi" ni terminology tu itumiwayo na "mafundi wa sheria"! Usiugue, kuvuta mdomo wala kuhemuka kwa yaso kuhusu. Utazeesha sura bure.
 
Learned brother

Kazi zao zinahitaji usomaji

wa mara kwa mara

ni miongoni mwa profession

ambazo once ukishakuwa wakili

lazima usome ili uweze kumudu

kufanya kazi zako vizuri

Utasoma vitabu vya sheria statute

judgment .......ni fani ambayo. Pia

wakati mwingine inahitaji ufanye

research ya hali ya juu (legal research)
 
Sina kipya cha kuelezea sana zaidi ya kujiulisha juu ya utambulisho huu kwa hawa mawakili.

Je wamejiita hivyo au kujitambulisha hivyo kuonyesha umaalumu wa uwakala wao ?

Au

Hawajiamini ?

Au

Wanajifaragua au ?

Au

Kujitambulisha kwa tamko "Wakili" hakutoshi ?

Au

Katika elimu ya sheria kuna kipya gani tofatuti na elimu nyingine ?

Msaada tafadhali.
 
Hahahaaa!! ngoja waje tuasikie. Kwani kuna wakili wa kawaida na wakili msomi?, nawaza kwa maandishi wakuu!!
 
Sina kipya cha kuelezea sana zaidi ya kujiulisha juu ya utambulisho huu kwa hawa mawakili.

Je wamejiita hivyo au kujitambulisha hivyo kuonyesha umaalumu wa uwakala wao ?

Au

Hawajiamini ?

Au

Wanajifaragua au ?

Au

Kujitambulisha kwa tamko "Wakili" hakutoshi ?

Au

Katika elimu ya sheria kuna kipya gani tofatuti na elimu nyingine ?

Msaada tafadhali.
Hata kwenye idara ya misitu na mazingira kuna mawakili,ukisikia wakili MSOMI ni yule aliyekwenda shule na kusomea sheria hasahasa!!kwani sio kila wakili awe amesomea sheria una kuta mtu mfano ni mwana mazingira hivyo anatetea hasa ubaribifu wa mazingira huyo ni wakili wa mazingira japo hana elimu ya sheria!!ila ukisikia wakili msomi sio kwamba anajisifia bali ni haki yake kuitwa hivyo amepiga chuo kikuu na kumalizia shule ya sheria,ila zamani kulikuwa na board ambayo ndio walikuwa wanafanya mitihani yake na kupewa uwakili kabla ya shule ya sheria haijaanza!!mitihani hii ya board ilikuwa kuishinda ni kama kupata uraia wa USA!!!
 
Ni kweli, mawakili wana haki ya kuitwa wasomi.

Ni watu wanaosoma kila nyanja ya maisha kuanzia sheria za uhalifu, sheria za ardhi, sheria za mazingira, sheria za haki za binadamu, sheria za biashara, sheria za maliasili, sheria za mitandao, sheria za kimataifa, sheria za habari...nk.

Hakuna nyanja ya maisha ambayo wakili haijaisoma.

Ukiwa na shahada ya sheria, ni sawa na kuwa na PhD ya proffesion zote zingine.
 
Kaka mada yangu iko wazi,nawazungumzia mawakala wa sheria,tena sheria za ki sekula (secular).

Hao wa misitu na hao wengine hapa hawahusiki. Kwahiyo jikite katika kile kilichokusudiwa na mada.
 
Ni kweli, mawakili wana haki ya kuitwa wasomi.

Ni watu wanaosoma kila nyanja ya maisha kuanzia sheria za uhalifu, sheria za ardhi, sheria za mazingira, sheria za haki za binadamu, sheria za biashara, sheria za maliasili, sheria za mitandao, sheria za kimataifa, sheria za habari...nk.

Hakuna nyanja ya maisha ambayo wakili haijaisoma.

Ukiwa na shahada ya sheria, ni sawa na kuwa na PhD ya proffesion zote zingine.

Kaka nakupa faida ukisema wamesoma kila nyanja una maanisha nini ?

Je wamezisoma nyanja hizo kama fani au kama fani yao inavyoelekeza katika kutoa hukumu ?

Ukisema kama fani wewe utakua muongo hata kupigiwa mfano hufai.
 
Hapana, sijamaanisha wana technical knowledge ya fani husika, isipokuwa wanasoma madodoso yote ya kisheria kuhusu fani zingine zote na nyanja zote za maisha.

SHAHADA ya sheria ni sawa na PhD mia mbili za fani zingine.

Usomi ni usomi kweli kweli sio jina tu.

Hauwezi kunielewa kama wewe hukuwahi kuingia shule ya sheria.
 
Ni kweli, mawakili wana haki ya kuitwa wasomi.

Ni watu wanaosoma kila nyanja ya maisha kuanzia sheria za uhalifu, sheria za ardhi, sheria za mazingira, sheria za haki za binadamu, sheria za biashara, sheria za maliasili, sheria za mitandao, sheria za kimataifa, sheria za habari...nk.

Hakuna nyanja ya maisha ambayo wakili haijaisoma.

Ukiwa na shahada ya sheria, ni sawa na kuwa na PhD ya proffesion zote zingine.

Kaka unasema "ukiwa na shahada ya sheria ni sawa na kuwa na PhD ya proffesion nyingine"

Kaka sio kila unaloweza kuliandika au kuliongea uliandike au uliseme. Lazima uwe na vipimo mzee.
 
Hapana, sijamaanisha wana technical knowledge ya fani husika, isipokuwa wanasoma madodoso yote ya kisheria kuhusu fani zingine zote na nyanja zote za maisha.

SHAHADA ya sheria ni sawa na PhD mia mbili za fani zingine.

Usomi ni usomi kweli kweli sio jina tu.

Hauwezi kunielewa kama wewe hukuwahi kuingia shule ya sheria.

Sasa kama ni wadodosaji huwezi kusema wamesoma kila nyanja.

Embu toa sababu nyingine za mashiko za kuwafanya mawakala hawa wajiite au wajitambulishe kwa utambulisho wa "Wakili Msomi" ?
 
Kaka unasema "ukiwa na shahada ya sheria ni sawa na kuwa na PhD ya proffesion nyingine"

Kaka sio kila unaloweza kuliandika au kuliongea uliandike au uliseme. Lazima uwe na vipimo mzee.
Unahitaji vipimo gani?

Shahada ya sheria ina mkusanyiko wa taaluma za nyanja zote za maisha. NAMAANISHA NYANJA ZOTE ZA MAISHA. ZOTE KABISA.

Kwanini wasiwe wasomi sasa!!
 
Sasa kama ni wadodosaji huwezi kusema wamesoma kila nyanja.

Embu toa sababu nyingine za mashiko za kuwafanya mawakala hawa wajiite au wajitambulishe kwa utambulisho wa "Wakili Msomi" ?
Unaelewa nini kuhusu neno "MSOMI"?
 
Back
Top Bottom