Kama wewe ni mwanasheria toa jibu tu wakili msomi ni nani au maana yake nini?!?Sasa unauliza ya nini wakati wewe sio Mwanasheria?
Neno Wakili Msomi naona linaenea kwa kasi kubwa huwa sielewi lina maanisha nini linapotumika hasa hasa na Watangazaji wetu wa vyombo vya habari! nikijua kabisa huwezi kuwa wakili kama sio mwanasheria ambaye ni msomi.
Na kila fani kwa waliokwenda shule hasa level za chuo kikuu huwa ni wasomi.
Sasa kwanini wanaitwa Wakili Msomi je Kuna wakili asiye msomi au??
Mimi si mwanasheria!!
Wewe ulisikia nani ameitwa Wakili msomi?Kama wewe ni mwanasheria toa jibu tu wakili msomi ni nani au maana yake nini?!?
Leo nimesikia Clouds FM kipindi chao cha michezo usiku huu Mtangazaji akitamka Wakili Msomi.........Wewe ulisikia nani ameitwa Wakili msomi?
Kwahiyo wasomi wapo kwenye sheria tu? Hakuna wahasibu wasomi? Wanauchumi wasomi? Mainjinia wasomi? kwani msomi si mtu aliyesoma? kwanini wakili ndio wawe wasomi? ina maada kada nyingine sio wasomi(hawajasoma)?
Pamoja na Maelezo yako mazuri tu lakini si kweli kuwa fani ya sheria ndiyo kujua Fani zingine si kweli Hata kidogo.Niliwahi kusoma mahala, hii sio Tanzania tu, ni Dunia nzima kwa wanasheria kuitwa au kujiita wasomi au Learned brothers/sisters.
1. Mawakili wanapokua mahakami na wakawa wanabishana kwa hoja, wakili mmoja haweza kumpinga mwenzake kwa kumuita mjinga au mpumbavu, hapana anatakiwa hata kama hoja ya wakili wa upande wa pili ni ya kijinga, anatakiwa kusema wakili msomi mwenzangu hapo napingana na wewe hivi na hivi na sio kutumia maneno mabaya au majina mabaya katika kupinga hoja. Yani hutakiwi kumuonyesha mtu ni mjinga moja kwa moja, unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Kwamba kama mtu ni mjinga usimwambie wewe ni mjinga, mwambie tu brother uwezo wako wa kukubali mambo unashuka ndugu yangu(your level of appriciating things is diminishing)
2. Mawakili au wanasheria wanafundishwa kumshitaki au kumtetea yoyote kutoka katika taaluma yoyote ile, iwe unatoka uhasibu, sheria, uchumi, uinjinia, sayansi, udaktari, wizi, ujambazi, ulawiti, ubakaji, urubani, fani zote.
Hivyo wanajiona kua wanajua mambo karibu yote kama sio yote kwa ujumla yaliyo chini ya jua. Ndio maana huwezi kupeleka kesi mahakamani ya udaktari hakimu akakuambia kua bwana sisi sio madaktari hivyo hiyo kesi haitasikilizwa, hapana , wataipokea na kuisikiliza hadi mwisho na hukumu itatolewa utafikiri wao wanajua udaktari.
Kwa mantiki hiyo wanasheria toka zamani wamekua wakiona fani nyingine kama fani za kiwango cha chini na kijiona wao ni bora na ni wasomi kuliko wengine.
Kama ndivyo mbona uwa kuna areas of specialization kadhaa kwenye sheria mfano enviromental law, bankruptcy law, corporate law, admiralty/maritime law n.k? Ina maana kila wakili ni mbobezi katika maeneo yote hayo?Niliwahi kusoma mahala, hii sio Tanzania tu, ni Dunia nzima kwa wanasheria kuitwa au kujiita wasomi au Learned brothers/sisters.
1. Mawakili wanapokua mahakami na wakawa wanabishana kwa hoja, wakili mmoja haweza kumpinga mwenzake kwa kumuita mjinga au mpumbavu, hapana anatakiwa hata kama hoja ya wakili wa upande wa pili ni ya kijinga, anatakiwa kusema wakili msomi mwenzangu hapo napingana na wewe hivi na hivi na sio kutumia maneno mabaya au majina mabaya katika kupinga hoja. Yani hutakiwi kumuonyesha mtu ni mjinga moja kwa moja, unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Kwamba kama mtu ni mjinga usimwambie wewe ni mjinga, mwambie tu brother uwezo wako wa kukubali mambo unashuka ndugu yangu(your level of appriciating things is diminishing)
2. Mawakili au wanasheria wanafundishwa kumshitaki au kumtetea yoyote kutoka katika taaluma yoyote ile, iwe unatoka uhasibu, sheria, uchumi, uinjinia, sayansi, udaktari, wizi, ujambazi, ulawiti, ubakaji, urubani, fani zote.
Hivyo wanajiona kua wanajua mambo karibu yote kama sio yote kwa ujumla yaliyo chini ya jua. Ndio maana huwezi kupeleka kesi mahakamani ya udaktari hakimu akakuambia kua bwana sisi sio madaktari hivyo hiyo kesi haitasikilizwa, hapana , wataipokea na kuisikiliza hadi mwisho na hukumu itatolewa utafikiri wao wanajua udaktari.
Kwa mantiki hiyo wanasheria toka zamani wamekua wakiona fani nyingine kama fani za kiwango cha chini na kijiona wao ni bora na ni wasomi kuliko wengine.
Nitajie jina la wakili mmoja ambaye ulisikia anatajwa kuwa ni Wakili msomi?Leo nimesikia Clouds FM kipindi chao cha michezo usiku huu Mtangazaji akitamka Wakili Msomi.........
Na nimekuwa nikisikia Mara kadha...Kamati inaongozwa na Wakili msomi.......
Mara utasikia kesi hii Wakili msomi ......amejitoa
Sasa mawakili wengine siyo wasomi au??