UTAPELI: Hayawi hayawi sasa yamekua: Tayari LBL kimewalamba

Hawa na wanaochota petrol kwenye magari yanayopata ajali hawana tofauti. Wanaungua kila mara lakini yakianguka tuu utawaona na madumu mbio.
 
Nilikua sijajua ujanja ujanja wa hizi scheme, ila huku kuna pesa.

Kuna kipindi nilidownload pesa kidogo nikapotezea, sasa hivi acha nidowload tena.

Hii ni kamali, ukuchelewa unalizwa, ukiwahi unapiga. Acha nijupatie hela za bia.

NB. Sio kila ponzy scheme ni ya kutia kibunda.
 
Aiseeee watanzania ni wajinga mnoo mno hawashughulishi fuvu zao,yaani kuna wilaya nipo aiseee wadada wamejiunga mno.
Nimejaribu kuwahoji hoji ila bado inaonekana suala la elimu lizidi kupewa kipaumbele,wanapenda sana hela ya bure.
Ukiwaoji fu unaona ni ujinga ujinga tu
 
Afrika ni tatizo sana , unamuingiza mtu unapata commission ya 10% unasema eti unapiga hela ni ujinga . Haya ndio hupelekea watu kuuza waafrika wenzao
Kwan huna akili?
Ukiwa nyumbu lazima uuzwe tena mchana jua linawaka kaliii
 
Nimewauliza hapa kuna mtu amewahi kurudisha mtaji wake,wote wanajiumauma,watanzania wao huwa hawareason hata siku moja.
 
Awali ilikuwa unatoa muda wowote, sasa inafikia ukingoni ndio wakaanzisha kutoa kwa level nadhani ilianza wiki iliyopita.
Ukingoni kivipi, siwamesema 18k unaingiziwa kila siku kwa mwaka
 
Kaka umeshaenda kuwithdraw? Asubuhi hii ndo nimejua kaka angu aliweka laki 5 tokea wiki iliyoisha hela haitoki.
Kasema sijui mmeambiwa mkatoe leo
Na hapo ataambiwa ni matatizo ya kiufundi, wataalamu wapo kulishughulikia mambo yatakaa sawa 😂
 
Ndio maana Kuna watu nawaambia kwamba Tanzania hii ukiamua kujifyatua akili kidogo ni rahisi kupiga Sanaa pesa kwasababu karibu 90% ya watz hapa nchini ni wajinga wa milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…