UTAPELI: Hayawi hayawi sasa yamekua: Tayari LBL kimewalamba

Mimi sijui kwanini michezo hii ya ku download pesa huwa siingiagi licha ya ushawishi na ushahidi kutoka Kwa watu wanaocheza
 
Kuna ile kampuni iliitwa, Pride, ya, kutoa mikopo, miaka ile ya, 2000,ilipiga pesa sana za wa bongo, kampuni yq vigogo wa ccm, serikali, mmoja wapo Has kitine, Spy director wa, zamani wa, TISS, hawa kenge waliumiza sana wa bongo maskini, unakopeshwa Leo 50K, wiki ijayo unatakiwa kuanza kurejesha fedha, ukishindwa, waliokudhamini, kinawalamba, Mali, zao zinapigwa mnada,tv, makochi, viti, ndoo, wajomba wanakuja kubeba kila kitu
 
Malipo yapo kwenye process,
mafundi wanarekebisha mitambo server zimezidiwa,
subirini Kila kitu kitakaa sawa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Yaani kabla ya kulizwa kauli hua ni hizihizi hazibadiriki
 
Nafikir ishu ya LBL ni kuinyamazia ili kutokujenga taharuki kwa waliojiunga...ikishazimwa kabisa ndo uje na unabii uliotabiri kipindi hiko cha nyuma.
 
Majuzi wanawake walikuwa wamejiunga na kitu kinaitwa Hallelujah Challenge. Yaani dada zetu ilikuwa huwaambii kitu kuhusu hiyo challenge iliyoanzishwa na tapeli mmoja huko Nigeria. Bahati nzuri haikuhusisha pesa.
 
Kaka umeshaenda kuwithdraw? Asubuhi hii ndo nimejua kaka angu aliweka laki 5 tokea wiki iliyoisha hela haitoki.
Kasema sijui mmeambiwa mkatoe leo
Moto ushawaka tayarii 😅 😅 😅 😅 😅 😅 😅 😅 😅 😅
 
Em mnijuze hiyo LBL ni nini, na inafanya kazi gani?
Nimepitwaa kabisa. Lol
 
Yapo on process ? Sawa sawa...lakin me nimetoka kutoa hela mpesa sasa hivi haina on process wala nini..Hao jamaa wanaizima hiyo platform mdogo mdogo na haiji kuwashwa tena...atasubir On process mpaka December mwaka huu, hata kalinda ilikuwa hivi hivi hao washatembea wanakusanya vitu vyao taratibu wakiona washamaliza wanazima server mazima
 
Awali ilikuwa unatoa muda wowote, sasa inafikia ukingoni ndio wakaanzisha kutoa kwa level nadhani ilianza wiki iliyopita.
Huo ni ujanja tu hao hawawashi tena hiyo server....Niamini mimi washafikia malengo hawataki tamaa, saivi watawadanganya system iko slow sababu rate ya watu my withdraw ni kubwa lakini kimsingi wamecheza kidogo tu na code ya hiyo platform, ngoja hizi siku mbili watatoa hata herufi a tu kwenye form ya my login watu watakuwa hawawez kulogin utaona mijitu itakavyopagawa. Kusikia kwa kenge mpaka damu imtoke masikioni.
 
Kaka angu nae kaniambia hela ipo kwenye process 125,000 ila hela ya wiki iliyopita hajapewa ndo basi tena🤣
 
Wakamatwe waliotapeli na wale waliotoa usajili wa hiyo kampuni ya desi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…