Utapeli: Jamaa amtapeli Waziri wa Ulinzi, ajitambulisha kama Katibu Mkuu wa CCM

Utapeli: Jamaa amtapeli Waziri wa Ulinzi, ajitambulisha kama Katibu Mkuu wa CCM

Mtu mmoja aliejitambulisha kama Wilfred Masawe mkazi wa kwa mtoni kwa Azizi Ali wilaya ya Temeke, Dar es Salaam amekamatwa kwa kujifanya Katibu Mkuu wa CCM na kumpigia simu Waziri wa Ulinzi na kumtapeli.

Jamaa anasema alitafuta namba ya Waziri wa Ulinzi, akampigia na kujitambulisha kama Chogolo Katibu Mkuu wa CCM na kuomba mchango wa harusi ya dada yake.

Waziri huyo wa ulinzi alimtumia mchango katibu mkuu huyo fake na jamaa akaitumia pesa kwa matumizi yake binafsi.

Sasa jamaa amekamatwa.
Msikilize hapa chini.

View attachment 1857061
Wiki ya wachaga hii😂😂😂
 
Eti Waziri wa Ulinzi anatapeliwa na boya flan yupo kwa Aziz Ally hapo. Je akibananishwa na Wachina au Mabeberu itakuwaje? Huyo waziri anapenda kutoa rushwa ndiyo maana kaingia kwenye 18 za Masawe
Hivi swala la mchango wa harusi kwa mtu anayepokea million 10 kwa mwezi na posho kibao ni swala la kujiuliza mara 2? Si unatuma laki kama buku tu?

Ukute alituma laki 5 sema mi ningevunja line hapo hapo huyo massawe ni fara! Ukivunja line unasajili nyingine na kitambulisho cha mtu mchezo umeisha na una hama mtaa tu!
 
Hahah kama ni kweli basi mwamba ajengewe sanamu kubwa pale wizara ya ulinzi...

Kumuingiza mkenge waziri wa ulinzi kiurahisi hivyo si jambo la ki sport sport...

Na huyo waziri dah, unaingizwaje cha kike kirahisi hivyo ilihali wewe ni mtu waongoza wizara kubwa hivyo...
Kutapeliwa hakuna bingwa hata wewe nikitaka nakusokota vizuri na unajaa mazima wala sio swala la kucheka mbinu zipo kama buku hivi!
 
Mwengine kamtia shaba mtu Sinza Lemax bar

Screenshot_20210718-090822_Samsung Internet.jpg
 
Back
Top Bottom