Utapeli wa Dawa ya 'HIT' katika kuua Mbu

Auntie tena hizi za kuchoma unaona kabisa mbu walivyokufa yaani auntie hit bado haijaisha kila siku naipuliza ukikaa kidogo unasikia mbu wanalia

Rungu afadhali napuliza kwa week mara mbili ila hit hapana kwakweli
HIT hamna kitu mle Auntie...
Wakati naanza kuitumia nilikuwaga nasema Dawa ya Mbu si ndiyo hii....Ile harufu yao...

Ila ukiipuliza Lisaa limoja likiisha Mbu hao...

Rungu kiboko yao
 
ukitaka mbu afe ni umshike umpulizie usoni😂😂😂
Mkuu hawa Mbu wa kizazi hiki ni mbu wa siku za mwisho hawasikii dawa. Pia hawana adabu hata kidogo usipokua makini wanawezakuwa wanageuza kichwa chako lodge wanamaliza mambo yao hapo
 
Mkuu kuhusu hit ni kweli jamani inalevya mbu sio kuua mpaka nilijiuliza au hii ni fake bora rungu mara 100 kuliko hit
I wish ningekuwa na Mamlaka huko TBS hii dawa ingebaki historia.
 
Ahsante sana kwa ushauri.

Eneo nilipo nipo na shughul za ufugaji pia nafuga mifugo mbalimbali ikiwemo na Samaki, sasa matumizi ya dawa kwa njia ya Fumigation ni risk mno. Natamani kutumia dawa za aina hiyo.
 
Tanzania kila kitu ni feki.Hao TBS wenyewe nadhani ni feki pia
 
ukitaka mbu afe ni umshike umpulizie usoni😂😂😂
Mkuu hawa Mbu wa kizazi hiki ni mbu wa siku za mwisho hawasikii dawa. Pia hawana adabu hata kidogo usipokua makini wanawezakuwa wanageuza kichwa chako lodge wanamaliza mambo yao hapo
Mbu wa sahivi wapo very technical kwanza wanakuuma kwanza alafu maumivu unapata tyr ameshaondoka eneo la tukio yaan wapo stealthy..... .

Kingine hawaonekani kirahisi/kijingajinga.

Pia ni wabishi kufa au kuzimia.

Nahis hawa mbu ni laboratory modified species..
 
Ni kweli kabisa,mbu hawafi na hata rungu ni harufu tu inabaki muda mrefu lakini haziui.
Nimeamua kujibana narumia x pel bei sio poa Sana imesimama
Biadhaa Tanzania ni utapeli Mtupu hata maji ya Kopo haya tunayonunua ukifatilia kwa makini utaona ni maji feki.

Sema walishapewa nembo za kubandika za Mamlaka husika basi haya maji ya nomba wanatuwekea tu
 
KDR.... knock down resistance mechanism ndani ya mbu ndio kitu kinawasaidia kupambana na sumu mnazo-wapulizia.
 
Watakua wale wa jangwani
 
Hii dawa ya HIT haifai hata kuwa air freshner, nilishawahi kuitumia nilijuta kununua...
Kwanza ina harufu mbaya utadhani kitu kilichooza,
PIli, haiui mbu hata sisimizi haiui.

Ni dawa isiyofaa hata ukipewa bure
Huu uzi unatakiwa uwe viral hadi social media zote.
Tunaibiwa sana Nchi nzima
 
leo nimempata kunguni mmoja nikamuweka sehemu open nakachukua HIT kuona kama wanaosema ni kweli? nikampulizia yule kunguni nikaona bado anatembea tena fasta nikasubiri dakika moja nikampulizia tena HIT nikaona bado anatembea tu, nikahakikisha yanayosemwa ni ukweli, HIT NI OVYOOO SINUNUI TENA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…