Utapeli wa Dawa ya 'HIT' katika kuua Mbu

Utapeli wa Dawa ya 'HIT' katika kuua Mbu

Ni kweli. Hili ni la siku nyingi sana. Sana sana unakuwa kama unawapulizia mbu perfume ili watoke out kuja kunyonya damu wakiwa wananukia vizuri. Vipi Expel siku hizi hamna? Jmabo jingine la kuzingatia ni kununua dawa kutoka vyanzo vinavyoaminika. Binadamu tumekuwa kama wanyama na tuko tayari kutengeneza dawa zenye madhara ili tu kupata fedha. Kama mchina mimi simwamini kabisa.
Kwamba unawapulizia Mbu unyunyu waje Wavuvi kempu kunywa Coctail ya Damu.. heheh.

Kuhusu vyanzo kwa kweli nanunua ktk haya maduka yetu ya mtaani.
 
Mbu wame evolve na kuweza kutengeneza usugu dhidi ya hizi dawa. Inatakiwa kununu dawa ya aina tofauti ili kupata matokeo chanya, jaribu kumtumia Ile dawa ya kuchoma inakua kwenye package ya silver .
Haina maajabu siku hizi Mbu washaizoea. Si ile inauzwa pakt moja sh 100?
 
Kweli mkuu wanazimia tu halafu wanaamka. zamani ulikuwa unazoa/unafagia mbu kibao ukifukiza kwa dawa za kuchoma.
Yes na Walikuwa wanaanguka kweli so unatime unawafagia.

Ila sahivi hawazimii wanajificha wanakaa huko wanajificha(Nahis wanavuta bangi zao) wakirudi ni spana tu.
 
Hizi dawa zilikuwa vizuri miaka minne iliyopita ila hali ya sasa kwa kweli ni UTAPELI wa wazi.

1_ Haiui MBU kwa kiwango kinachopaswa yaani katika Mbu 50 watakufa watatu (3).

Yaan mpk mbu afe ni umloweshe na hiyo dawa ndio atakufa ila ukipuliza kama inavyoelekezwa upulize ktk mazingira ya eneo waliopo, hakika hatokufa Mbu hata mmoja, ukitaka mbu afe ni umshike umpulizie usoni.

2_ Hata Mbu kuzimia kidogo hakuna! Sana sana watajificha tu kwa muda wa lisaa limoja baada ya kupuliza ila watarudi na wakirudi wanarudi na NJAA ya kufa mtu. (Inawezekana hii Dawa ina wapa Appetite zaidi)
Hizo ni bora ukapuliza perfume kuliko hizo takataka, jana nimetoka kugombana na mhudumu wa lodge moja mitaa ya Mawasiliano kwa kunilaza na mbu kisa HIT
 
Kwamba unawapulizia Mbu unyunyu waje Wavuvi kempu kunywa Coctail ya Damu.. heheh.

Kuhusu vyanzo kwa kweli nanunua ktk haya maduka yetu ya mtaani.
Ndiyo, wengi tunanunua huko. Ni Mungu tu anasaidia kwani Bongo mtu anaweza kuchanganya chochote bila kujali madhara. Chanzo cha kuaminika nimemaanisha kama unataka kununua brand nzuri ya bei kubwa kama aliyopendekeza mdau mmoja.
 
Yes na Walikuwa wanaanguka kweli so unatime unawafagia.

Ila sahivi hawazimii wanajificha wanakaa huko wanajificha(Nahis wanavuta bangi zao) wakirudi ni spana tu.
Hadi mijusi ilikuwa inakufa lakini kwa sasa utaona tu unaambulia mbu wawili watatu sakafuni ukifukiza.
 
Hizo ni bora ukapuliza perfume kuliko hizo takataka, jana nimetoka kugombana na mhudumu wa lodge moja mitaa ya Mawasiliano kwa kunilaza na mbu kisa HIT
Sirudii tena kuzinunua.. na sijui TBS wanafanyaga kazi gani hasa au wao kazi yao ni kukagua vipodozi vya carolite tu.

Haya madawa yanaumiza waTz wengi kiuchumi na kiafya pia, maana MALARIA inazid kutuumiza bado msongo wa mawazo kuwaza MBU usiku nalalaje etc.
 
miaka flani nyuma, kibanda hakijaisha vyema
niliziba madirisha, nilipiga chumbani, kwa kua inachoke nikatoka nje kwa mda wa dk 20

kurudi, nakuta mende, mijusi, nyoka wadogo, tandu, buibui, wote wamekufa wako pembeni
nilishangaa sana, ilihali lengo ilikua ni kuua mbu, nilishangaa pia kuona naishi na tandu chumbani 😅
Hapo kwenye nyoka wadogo umetuchomeka.
 
Ndiyo, wengi tunanunua huko. Ni Mungu tu anasaidia kwani Bongo mtu anaweza kuchanganya chochote bila kujali madhara. Chanzo cha kuaminika nimemaanisha kama unataka kununua brand nzuri ya bei kubwa kama aliyopendekeza mdau mmoja.
75k ndugu yangu.. unajua si mchezo.......
 
Back
Top Bottom