Utapeli wa Dawa ya 'HIT' katika kuua Mbu

Rungu ndo dawa ya Mbu... HIT tena lile kubwaa jinhaa ndo usijaribuuu haliuiii mbu lileee ni Air freshner...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Sinunui HIT tena.
 
What if ni mbu wamekua sugu
Wao wanatakiwa waje na solution means waongeze ingredients kupambana na usugu. Naamini watakuwa na Maabara ya kupima quality.
 
Hizi dawa zilikuwa vizuri miaka minne iliyopita ila hali ya sasa kwa kweli ni UTAPELI wa wazi.

1_ Haiui MBU kwa kiwango kinachopaswa yaani katika Mbu 50 watakufa watatu (3).

Yaan mpk mbu afe ni umloweshe na hiyo dawa ndio atakufa ila ukipuliza kama inavyoelekezwa upulize ktk mazingira ya eneo waliopo, hakika hatokufa Mbu hata mmoja, ukitaka mbu afe ni umshike umpulizie usoni.

2_ Hata Mbu kuzimia kidogo hakuna! Sana sana watajificha tu kwa muda wa lisaa limoja baada ya kupuliza ila watarudi na wakirudi wanarudi na NJAA ya kufa mtu. (Inawezekana hii Dawa ina wapa Appetite zaidi)

Si kwa HIT tu nimetumia dawa ya RUNGU pia haina matokeo mazuri ktk kuangamiza MBU.

Je wana JF mmekutana na hii changamoto?

Je mnapendekeza dawa ipi bora ya kuangamiza hawa viumbe?

NB: nimezungumzia kwa upande wa Mdudu aina ya MBU tu kwa kuwa ndio mdudu anayenisumbua mahala nilipo, hakuna Mende wala wadudu wengine, hivyo ufanisi wa dawa hii kwa kuua viumbe wengine sijaupima.

Nawasilisha.
bora hata HIT kidogo inasaidia hii rungu inakulowesha mkono halafu inanuka mafuta ya taa na wakati mwingine dawa haitoki ila unashangaa ndani ya kopo bado ipo nyingi
 
Aise huu ni ukweli kabisa leo nilivyouona huu uzi Sasa ndo napigia mstari kabisaa, hit nilitumia siku za nyuma lakin kila nikirud nyumban nakuta mbu wako vilevile hawajafa na taratibu zote za kupuliza nimefanya

ila Kati ya Hit na rungu angalau Rungu napuliza mara 1 tu kwa wiki inasaidia mbu hawapo hawa hit bidhaa yao haiuwi mbu kabisa
 
Hizi dawa zilikuwa vizuri miaka minne iliyopita ila hali ya sasa kwa kweli ni UTAPELI wa wazi.

1_ Haiui MBU kwa kiwango kinachopaswa yaani katika Mbu 50 watakufa watatu (3).

Yaan mpk mbu afe ni umloweshe na hiyo dawa ndio atakufa ila ukipuliza kama inavyoelekezwa upulize ktk mazingira ya eneo waliopo, hakika hatokufa Mbu hata mmoja, ukitaka mbu afe ni umshike umpulizie usoni.

2_ Hata Mbu kuzimia kidogo hakuna! Sana sana watajificha tu kwa muda wa lisaa limoja baada ya kupuliza ila watarudi na wakirudi wanarudi na NJAA ya kufa mtu. (Inawezekana hii Dawa ina wapa Appetite zaidi)

Si kwa HIT tu nimetumia dawa ya RUNGU pia haina matokeo mazuri ktk kuangamiza MBU.

Je wana JF mmekutana na hii changamoto?

Je mnapendekeza dawa ipi bora ya kuangamiza hawa viumbe?

NB: nimezungumzia kwa upande wa Mdudu aina ya MBU tu kwa kuwa ndio mdudu anayenisumbua mahala nilipo, hakuna Mende wala wadudu wengine, hivyo ufanisi wa dawa hii kwa kuua viumbe wengine sijaupima.

Nawasilisha.
Umejua kunichekesha. Nilikuwa na stress ila kwa andiko lako mbavu zimeuma. Anyways kwa Sasa hakuna dawa za mbu, ni usanii TU.
 
Back
Top Bottom