UTAPELI WA FOREX: Francisco Magnetics adaiwa kuhama nchi, anadaiwa pesa nyingi. Polisi wamsaka!



yap unawazungumziaje hao wadau aise?
 
Hizo BMW X6 zimenunuliwa kwa hela ya signals na mentorship boss, ukiongeza na hela ya account management ndo kabisa. Hawa jamaa wanakula kitu kinaitwa IB contracts (Introducing broker). Ukishapewa hiyo mikataba ndani yake kuna kuwa na percentage na commission za juu kwa kila mtu unayemuingiza hii inafanana na watu wa forever living and so forth, kwa hiyo jinsi watu wengi wanavyokuwa chini yako ndo jinsi commission yako inazidi. Sasa katika izo IB contracts unapata hela nyingi zaidi kuliko hata kutrade mpaka hapo kunakuwa na conflict of interest. katika hayo makubaliano yao moja wapo ni kuchoma hela za kila mtu atakyekuwa chini yako. Zipo njia nyingi sana boss nikianza kutype hapa ntamaliza siku nzima ila hii ndo kubwa ambayo inatumika zaidi na kitu kibaya zaidi ni kwamba hawa brokers wengi hawapo regulated NFA, CFTC,FTA na regulators wengine na hao ndo huwa wanatoa izo ib contracts kwa watu
 
Unapo sema hakuna hela rahisi unamaanisha nn mkuu?

Kama unadhani hakuna hela rahisi basi huyo dogo asingeweza kununua hilo BMW X6,
 
Tuachen jamani na forex yetu
Kumpa mtu hela atrade badala ya kusoma ufanye wewe ni umbulula yaani watz tunapenda mteremko sana aisee
kama elimu ipo kwanini usitake shamba?
Unataka mahindi tuuu mahindi tuuu
haya sasa mmepewa gunia na mmemwachia shamba nini mmefaidika?

Kwa wanaojielewa wanasoma forex na hawajutii mda wao waliouwekeza katika kusoma forex, Kuna jamaa mmoja yeye anakuambia anakufundisha
Ada ni USD500 ukimaliza kusoma still anakuambia ulipie tena usd300 kwa miezi miwili mnakuwa mnafanya analysis pamoja kapiga hela katengeneza wanafunzi ambao wamekuwa waalimu now hana habari tena na hizi mambo ya kufundishana
ni bata tu.


Forex is real ukiamua kuisoma just pay for knowledge not for management
 
orodhesha kama broker Watatu ambao wako regulated
 
nimesoma untrade stocks mkuu, so stcocks ndio kuna unafuu zaidi ya forex hii tunayoijua au...kuna utofauti upi?

Boss kama hiyo comment nilivyosema kuna options nyingi tu za kutrade ni wewe mwenyewe kuchagua ipi ambayo inakupa faida. Naweza kukwambia Stocks zinalipa ila wewe ukajaribu kuzitrade na ukawa unapata hasara tu. Wakati naanza kuna jamaa aliniambiaga trade pair mbili tu kwa sababu wewe ni beginner ila mi nikamuuliza je izo pair mbili ntakazochagua ikitokea kwa bahati mbaya mwezi mzima hazitembei ina maana trading career yangu ndo imefia hapo? Nilichofanya mimi nilitrade kila kitu kilichopita mbele ya macho yangu, mwaka wa kwanza portfolio yangu ilikuwa na instruments zaidi ya 146 ila now nna instruments 18 tu.
 
huyu jamaa alisababishaga nikajoin forex but niliweka $10 nikapata profit ya $7 nikasepa mpaka leo
 
Kwanini hawa watu wa Forex lazima waoneshe kuwa wamefanikiwa?
Wakiishi kimya kimya kuna shida gani?
Kuwavuta watu mkuu,ni kama wafanyavyo wale jamaa wa Forever Living na Alliance International tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…