UTAPELI WA FOREX: Francisco Magnetics adaiwa kuhama nchi, anadaiwa pesa nyingi. Polisi wamsaka!

UTAPELI WA FOREX: Francisco Magnetics adaiwa kuhama nchi, anadaiwa pesa nyingi. Polisi wamsaka!

Heading To Work kwa upande wangu naona kama wanawavutia watu waingie kwenye kumi na nane zao wawapige kama hivyo na kauli yako kuwa kuna wabongo wanapiga pesa toa vielelezo wanapigaje ili na hao wengine wanaotaka kufanya Forex wafanye wenyewe wapige hiyo hela kama ni rahisi tuu ingawaje Mimi sifikirii wala siji kuja kuifanya...watu wapo busy na picha za BMW X 6 kwa kuwavutia wapigwaji..
Hizo BMW X6 zimenunuliwa kwa hela ya signals na mentorship boss, ukiongeza na hela ya account management ndo kabisa. Hawa jamaa wanakula kitu kinaitwa IB contracts (Introducing broker). Ukishapewa hiyo mikataba ndani yake kuna kuwa na percentage na commission za juu kwa kila mtu unayemuingiza hii inafanana na watu wa forever living and so forth, kwa hiyo jinsi watu wengi wanavyokuwa chini yako ndo jinsi commission yako inazidi. Sasa katika izo IB contracts unapata hela nyingi zaidi kuliko hata kutrade mpaka hapo kunakuwa na conflict of interest. katika hayo makubaliano yao moja wapo ni kuchoma hela za kila mtu atakyekuwa chini yako. Zipo njia nyingi sana boss nikianza kutype hapa ntamaliza siku nzima ila hii ndo kubwa ambayo inatumika zaidi na kitu kibaya zaidi ni kwamba hawa brokers wengi hawapo regulated NFA, CFTC,FTA na regulators wengine na hao ndo huwa wanatoa izo ib contracts kwa watu
 
Nilimsoma sana habari zake, lakini sikumuelewa ... Lifestyle yake , halafu sikuona anapata hizo hela zote... Nikamua kukaa mbali. Niliposikia Tanzania, forex forex, nikajua mchezo, umehamishiwa bongo kwa style nyingine.. Hakuna hela rahisi, yeyote anayekuambia utapata hela kwa njia nyepesi, anataka kukupiga..
Angalizo benki , investment house wanafanya sana biashara ya forex, ambayo imejengwa kwenye msingi wa speculation... Lakini wale wanatumia hela ya benki na wana mfumo wa kuwawezesha kutrade dunia nzima.. Hawa wa kwetu, ni watu wa fursa tu.
Unapo sema hakuna hela rahisi unamaanisha nn mkuu?

Kama unadhani hakuna hela rahisi basi huyo dogo asingeweza kununua hilo BMW X6,
 
Tuachen jamani na forex yetu
Kumpa mtu hela atrade badala ya kusoma ufanye wewe ni umbulula yaani watz tunapenda mteremko sana aisee
kama elimu ipo kwanini usitake shamba?
Unataka mahindi tuuu mahindi tuuu
haya sasa mmepewa gunia na mmemwachia shamba nini mmefaidika?

Kwa wanaojielewa wanasoma forex na hawajutii mda wao waliouwekeza katika kusoma forex, Kuna jamaa mmoja yeye anakuambia anakufundisha
Ada ni USD500 ukimaliza kusoma still anakuambia ulipie tena usd300 kwa miezi miwili mnakuwa mnafanya analysis pamoja kapiga hela katengeneza wanafunzi ambao wamekuwa waalimu now hana habari tena na hizi mambo ya kufundishana
ni bata tu.


Forex is real ukiamua kuisoma just pay for knowledge not for management
 
Hizo BMW X6 zimenunuliwa kwa hela ya signals na mentorship boss, ukiongeza na hela ya account management ndo kabisa. Hawa jamaa wanakula kitu kinaitwa IB contracts (Introducing broker). Ukishapewa hiyo mikataba ndani yake kuna kuwa na percentage na commission za juu kwa kila mtu unayemuingiza hii inafanana na watu wa forever living and so forth, kwa hiyo jinsi watu wengi wanavyokuwa chini yako ndo jinsi commission yako inazidi. Sasa katika izo IB contracts unapata hela nyingi zaidi kuliko hata kutrade mpaka hapo kunakuwa na conflict of interest. katika hayo makubaliano yao moja wapo ni kuchoma hela za kila mtu atakyekuwa chini yako. Zipo njia nyingi sana boss nikianza kutype hapa ntamaliza siku nzima ila hii ndo kubwa ambayo inatumika zaidi na kitu kibaya zaidi ni kwamba hawa brokers wengi hawapo regulated NFA, CFTC,FTA na regulators wengine na hao ndo huwa wanatoa izo ib contracts kwa watu
orodhesha kama broker Watatu ambao wako regulated
 
nimesoma untrade stocks mkuu, so stcocks ndio kuna unafuu zaidi ya forex hii tunayoijua au...kuna utofauti upi?

nen.png
Boss kama hiyo comment nilivyosema kuna options nyingi tu za kutrade ni wewe mwenyewe kuchagua ipi ambayo inakupa faida. Naweza kukwambia Stocks zinalipa ila wewe ukajaribu kuzitrade na ukawa unapata hasara tu. Wakati naanza kuna jamaa aliniambiaga trade pair mbili tu kwa sababu wewe ni beginner ila mi nikamuuliza je izo pair mbili ntakazochagua ikitokea kwa bahati mbaya mwezi mzima hazitembei ina maana trading career yangu ndo imefia hapo? Nilichofanya mimi nilitrade kila kitu kilichopita mbele ya macho yangu, mwaka wa kwanza portfolio yangu ilikuwa na instruments zaidi ya 146 ila now nna instruments 18 tu.
 
magnenga.png

tweet.png

tweet2.png


Ni kijana ambae hapo nyuma amepata kufanikiwa kwa haraka sana na kuishi maisha ya juu sana na kukiri kuwa na uwezo wa kutengengeneza takribani milioni 9 kila wiki, Ilifikia kipindi akanunua gari ya kifahari aina ya BMW X6, sijui kama ilikuwa ni bahati mbaya au maksudi kimaslahi hio gari ilikula mzinga wiki kama sio miezi michache kabla hajaondoka nchini ikiambatanishwa na "tetesi" ya kwamba kuna aina za bima endapo gari ikipata ajali shirika la bima humlipa mmiliki pesa ya kununua gari upya.

Kijana kwa sasa hayupo nchini na inadaiwa anatafutwa na polisi kwa kile kinachosadikiwa ya kwamba kakimbia na pesa anazodaiwa na wawekezaji wake waliowekeza pesa zao kwake ili wapate faida kwa kuziongeza kupitia skills za forex alizonazo kijana. Kuna "tetesi" ya kwamba wawekezaji walioowekeza wanamdai kiasi cha dola laki tatu (takribani milioni 690 za kitanzania).

HITIMISHO
Walengwa wanaomdai huyu kijana inawezekana wakadhani kwamba kijana kakimbia na pesa zaokumbe sivyo , Kijana kaahidi ya kupitia account yake ya twiiter kwamba atarudisha pesa zao, walengwa itapendeza wawe wavumilivu wakiwa na uhakika wa kurejeshewa pesa zao.

NJE YA MAADA
Awali majuzi tarehe 7 - 5 -2019 huko nchini afrika kusini mfanya biashara wa forex aliekuwa na pesa chafu ambae pia wawekezaji walikuwa wakiwekeza pesa kwake kwa jina la "cashflow ngcobo" amefungwa kifungo cha miaka sita na kulipa faini ndefu baada ya kupatikana na kesi ya kutapeli wawekezaji

CHIMBUKO LA FOREX TANZANIA
Miaka ya 2017 kuna kijana anaefahamika kwa jina la "Ontario ama Sir jeff dennis" ndie aliekuwa chanzo cha watanzania wengi kuanza kuisoma, kuifatilia na kuifanya forex, alileta muamko mkubwa sana wa forex nchini ikafika kipindi habari ya mujini ilikuwa ni forex na hata post yake ilivunja rekodi ya ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa jamiiforums kwa kuwa na wasomaji wengi. Baada ya miezi michache kijana huyu alianzishiwa maada / thread kibao humu ndani zilizomshtumu kwamba ni mpigaji aliekuwa analazimisha wanafunzi wake watrade kwa kumtumia broker waliekuwa wanagawana faida
huyu jamaa alisababishaga nikajoin forex but niliweka $10 nikapata profit ya $7 nikasepa mpaka leo
 
Kwanini hawa watu wa Forex lazima waoneshe kuwa wamefanikiwa?
Wakiishi kimya kimya kuna shida gani?
Kuwavuta watu mkuu,ni kama wafanyavyo wale jamaa wa Forever Living na Alliance International tu.
 
Back
Top Bottom