Utapeli wa kuagiza gari Japan

Nimeona channel 10 wakimzungumzia huyo tapeli anaitwa somebody Laizer
 
Na kuna tradecarview
 
Ni mimi wala sio rafiki, familia inasubiri gari sijui hata cha kuwaambia, najiuliza hivi ntakuja kaa sawa kweli na kusahau kabisa?
Aisee[emoji3064]
Pole sana Mkuu.

Bwana na atafungua mlango kwa njia nyingine..maisha yana mapito mengi.

Muhimu bado upo hai na una nguvu,basi Mungu atabariki tena na kurejesha hela iliyoliwa na nzige na madumadu.
 
Aisee[emoji3064]
Pole sana Mkuu.

Bwana na atafungua mlango kwa njia nyingine..maisha yana mapito mengi.

Muhimu bado upo hai na una nguvu,basi Mungu atabariki tena na kurejesha hela iliyoliwa na nzige na madumadu.
Amina Amina hata sasa nauona ukuu wake ,Mungu achunguziki unapoona umekwisha kabisa yeye anaanzia hapohapo
 
Kampuni kama Autocom Japan, Beforwad, SBT JAPAN, zina ofisi zao hapa bongo, sio ofisi za wakala NO yaani ofisi zao kabisa ambazo wameajiri wabongo, kusimamia shughuli zao.

So hata wakikuzingua ni rahisi kupata msaada na kusaidiwa.

Sasa unawasiliana na watu mtandaoni ambao hawana local office Tanzania hii ni kurisk sana. Jambo lingine, wachina, wahindi na waarabu ni wapuuzi sana. Mkipishana jambo anabadilika hataki kujadili lolote so unaona hapo amekwambia cancel hiyo order then anakukataa hataki mazungumzo.
 
Ni bahati mbaya tu Mkuu.. Kuna walioagiza direct na wakafanikiwa.

Siku ya kufa nyani miti huteleza yote.
 
Amina Amina hata sasa nauona ukuu wake ,Mungu achunguziki unapoona umekwisha kabisa yeye anaanzia hapohapo
Unaweza shangaa ukapata hela kirahisi.
Mshukuru Mungu kwa yote.

Pengine wakati wako wa kumiliki gari ulikuwa bado,Kuna sababu ya wewe kupita huko.

Hata katika mabaya, yapo mambo mazuri tunayojifunza.. take it in a positive way..
 
Umekosea ku cancel, hayo madai, usinge cancel ufungue Jinai. Sasa ume cancel kwa hiyari? Utateseka sana aisee, ni kiasi gani?
Na wao wamejua kuwa ndio wana matatizo kwa kuchelewesha order ya mteja so walichofanya ni kumwambia acancel ili akija lalamika waseme alicancell order yake mwenyewe, hatukushindwa kumsaidia.
 
Huyu kakutana na scammers wakinaija. real motor OG wako poa tu mbona labda km web yao imehakiwa.

wameweka angalizo kwenye website yao.

Unaweza kuona contact details zao pia humo. km sio hizo mdau umeliwa.
 
Amina Amina hata sasa nauona ukuu wake ,Mungu achunguziki unapoona umekwisha kabisa yeye anaanzia hapohapo
Pole sana. Kuna watu wanakejeli ila mambo kama haya mtu unaweza kupigwa. Ushauri wangu kwako ni kuwa pamoja na kukubali matokeo lakini usiwache hivi hivi bila kujaribu kuchukuwa hatua za kisheria. Mradi tu uwe macho, usikubali kuhonga kwani fedha kama hizo huna uhakika wa kuzipata. Mwambie yeyote anayefuatilia kuwa kama anataka afuatilie halafu fedha zikipatikana umpe commission.
 
Nilikuwa nawasiliana nao kwa email na insta.
Hapo ndo kosa lilipoanzia. Haya makampuni wana internet yao ya ndani kwa ndani. Ukiona unapelekwa instagram, WhatsApp sijui facebook ujue tayari ndo majizi yenyewe hayo. pole sana bro. naamini umejifunza kitu pia.
 
Hii kitu ingewezekana kufuatilia na jamaa akapata haki yake km angekuwa anawasiliana na watu genuine! maana pale ubalozini wanayatambua hayo makampuni.

sasa hapa amewakabidhi pesa majizi watu ambao hamna njia ya kuwapata. namshauri asihangaike atapoteza pesa zaidi bure huko polisi sijui wapi hawawezi kumsaidia!

bro kubali matokeo move on, pesa makaratasi yanatafutwa. mungu jalia utapata ingine, maisha yaendelee.
 
Lakini jamaa jambo lake linafatilika. Labda anachoka tu au anajiskia vibaya kufatilia.

Angeripoti polisi then waanze, kuanzia info za benki.
 
Pole ndugu mpiga kura
 
Lakini jamaa jambo lake linafatilika. Labda anachoka tu au anajiskia vibaya kufatilia.

Angeripoti polisi then waanze, kuanzia info za benki.
mtandaoni kuna mengi mkuu usiamini website unazokutana nazooo...!! hata ukienda mahakamani bado huna cha kusaidiwa maana hawana ofisi bongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…