Utaratibu na Ratiba za kumjibu Joseph Sinde Warioba kutokana na Press yake leo

Hawa wazee ndo waasisi wa mambo yote ya hovyo halafu sasa hivi wanajitokeza kuongea kinafiki. Huyu unaambiwa alikuwa chawa wa mwalimu haijawahi tokea. Hakuwa mshauri mzuri kwa mwalimu.
 
Makonda mtoe hawezi kumjibu Warioba mmejijengea fikra potofu. Ila Ally Happi, Kawaida, Kibajaji, UVCCM, Wasanii kama Steve Mengele, Mwijaku hao wanaweza kujitosa lakini watadunda.

Mzee Warioba hajatoka tu kusema alichosema ijapokuwa naye ni kama au uoga fulani maana anadai polisi imeanza kuingizwa kwenye siasa tangu 2019 na 2020 wakatiwa JPM na hakuwahi kumkemea kuna walakini mahala.
 
Wamjibu nini cha maana alichosema, anaongea kama anatabiri nani huyo aliyemwambia jeshi nitaingilia siasa. eti lisiingilie siasa nani kamwambia, kama sio uchawi. Mzee ana sura mbaya kama roho yake ilivyo. Anawanga mchana. Kama kidume kweli atukane wote sio anatukana taasisi zote hawana maadili ila Raisi hamgusi. Nani anaongoza serikali? unafiki tu
 
Japo umeandika kwa sarcastic manner!! Ila Mimi binafsi Nina haya ya kusema.

CCM ya Sasa hivi ni chama kilichooza na kinanuka uovu wote wa Kila aina, uuaji, ufisadi,wizi,ubakaji, utekaji n.k na watu kama mzee Warioba ambao walilelewa kwenye CCM safi huwa wanaumizwa sana na haya mambo ya ovyo yanayofanywa na CCM hii ya Sasa na ndio maana huwa anashindwa kuvumilia anaamua kusema pasipokujali kama atawakwaza makada wa chama Chake.

Kwa bahati mbaya sana watu wanaopenda kusimama kwenye ukweli na Haki Kama mzee Warioba kwa hii CCM ya Sasa huwa wanaonekana ni maadui wa chama, Tena hili linathibitishwa hata na baadhi ya comments zilizopo kwenye huu Uzi.

Hii CCM ya Sasa hivi inataka wazee wajinga wajinga na wanafiki wanafiki wenye vinasaba vya uchawa kama mzee Yusufu Makamba ambao hawana ujasiri wa kukemea maovu.

Kila mtu ameona jinsi CCM walivyoharibu uchaguzi wa mwaka huu, halafu Hawa UVCCM wanakuja kumzodoa mzee Warioba kwa hiki alichokiongea? Wanataka Kila mwanachama awe kondoo tu wakufumbia macho maovu?

Nyie UVCCM mkimuheshimu mzee dalali mzee Kinana pamoja na mwenzake Yusufu Makamba inatosha, sisi wengine tutamuheshimu mzee wa mzalendo wa kweli Joseph Warioba
 
Na haya ndio maneno ya kuongea kuhusu mzee Warioba? Kwamba nyie UVCCM wa Sasa h ndio mna uchungu sana na chama pamoja na taifa kwa ujumla kuliko hata mzee Warioba??

Yaani hii comment yako inaonesha jinsi gani upumbavuu, ujinga, malezi ya ovyo pamoja na elimu duni ulivyonavyo kiasi Cha kuonekana hauna tofauti na kichaa.

Wewe acha kuleta kashifa za kipuuzi hapa, jibu hoja zake.

Kwanini kwenye uchaguzi huu wagombea walionekana Wana dosari na hatimae kuwa disqualified walikuwa ni wagombea wa vyama vya upinzani tu? Ina maana huko CCM wagombea wake wote hawakuwa na dosari za majina kama zile walizokuwa nazo wapinzani?
 
Najiuliza siku Ile Mhe Sinde Waryoba anashambuliwa na Makonda,,, walinzi wake walikuwa wapi ? Kama angepata madhara makubwa wangewajibika au ilipangwa ?
 
Mzee ana hoja, bt natatizika kumuelewa, coz ujambazi ktk chaguzi zetu haujaanza leo, why hakuwahi fanya anachofanya sasa?
Mzee wa watu amepiga kelele muda mrefu kuhusiana na mwenendo wa Chaguzi lakini hajawahi kusikilizwa!
Ni mmoja wa Wazee walioambiwa wanawashwashwa!
Sasa afanyeje?
 
Nitatazama press yake huko YOU TUBE ili nije nitoe tamko kuhusiana na alichoongea. Tamko langu ndo utakuwa msimamo wa JF kuhusu alichokiongea Mzee Warioba.
Huna huo uwezo mkuu! Aliyoyaongea yote ni kweli.
Hoja hujibiwa kwa hoja siyo vijembe vya U CHAWA CHAWA
 
Hapa naona umeanza ishambulia hadi sura yake. Hii inaonesha CCM ina vijana wapo kuipigania.
 
Badala ya kufanyia kazi maoni yake, wao wanapanga kumtukana
Ni kumtukana tu maoni yake au hoja zake haina haja ya kujibu. Tutamtukana yeye na kukosoa hata alivyoumbwa. Sisi tunaipenda sana CCM huyu mzee anajua nini kuhusu Chama? Sisi ndo tunakijua chama tumetoka nacho mbali.
 
Mzee ana hoja, bt natatizika kumuelewa, coz ujambazi ktk chaguzi zetu haujaanza leo, why hakuwahi fanya anachofanya sasa?
Kwa sababu hakikuwahi kutokea kama kilichotokea 2019, 2020 na mwaka huu!
 
Hawa wazee ndo waasisi wa mambo yote ya hovyo halafu sasa hivi wanajitokeza kuongea kinafiki. Huyu unaambiwa alikuwa chawa wa mwalimu haijawahi tokea. Hakuwa mshauri mzuri kwa mwalimu.
umeeleza ukweli sana comrade

halafu wengi hawajui kwamba mzee wetu huyu ambae tunampenda na tunamuheshimu sana hakua na ushawishi wowote wakati akiwa kiongozi, alikua wakawaida tu kama walivyo wengine, na ndiyo maana alishindwa uchaguzi huko Bunda, tena kwao kabisa mchana kweupe na upinzani.

bila ya hayati Nyerere kumshika mkono,
hapangelikua na mtu anaetangatanga kama alivyo sasa, angekua anasugua gaga tu huko bunda kwao.

halafu pia,
nadahani ana kinyongo na wivu flani moyoni mwake dhidi ya serikali, sasa sijui ni kwasababu wanae na ndugu zake wako nje ya game la siasa za Tanzania ama ni unafiki wake tu...
 
Nadhani ungemuuliza huyu mzee wako mwanga wakati wa JPM alikuwa wapi? alisema nini kuhusu uchaguzi? ukija na majibu nitakujibu.
 
Hapa naona umeanza ishambulia hadi sura yake. Hii inaonesha CCM ina vijana wapo kuipigania.
Yes sababu ana sura mbaya kama roho yake ilivyokuwa mbaya. Shida ya huyu mzee alikuwa wapi wakati wa JPM anawavuruga wapinzani? alisema nini? Mzee shida yake kubwa anachuki na wa Zanzibar hii ya Rais kutoka kule inamnyima usingizi. Mzee mwanga wa mchana amekuwa kama bundi kutabiri nuksi.
 
Steve Nyerere.
 
Jibuni hoja zake siyo kumshambulia yeye.
 
Tuendelee kumshambulia Mzee Warioba. Na angekuwa karibu hata tungempiga mawe. Tusiache mshambulia na kumtukana mpaka akome kuwa anaongea ukweli. Anatakiwa abadilike ajifunze kusema mitano tena.
hakuna haja kumshambulia au kumpiga mawe yeyote nchi hii ya amani gentleman,

muhimu ni kuupinga unafiki wa mtu mzima mwenye heshima na familia, ambae alipaswa kulea wajukuu nyumbani anakuja kumbwelambwela kana kwamba ati nae ni gen z aliopoteza uelekeo
 
Kwani huamini kama dunia ina mwisho?
Mzee anaongea ukweli japo mnauchukia ukweli huwo kwasababu ya maslahi yenu binafsi.
gentleman,
binafsi naamini Mungu pekee na sio huo ushirikina na unafiki wa huyo mzee amabae kama taifa tunamuheshimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…