Utaratibu wa wafiwa kuwalisha waombolezaji wengine umerasimishwa Tanzania?

Mimi naongelea kwa Upande wa Uislamu
Sheria ya kiislamu inasema wafiwa ndo wanatakiwa wapelekewe chakula kwa muda wa siku 3 na majirani ili kuonesha upendo bcz kwa mda ule wafiwa wanakua kwenye huzuni kubwa na majonzi

Na nyumba ya mfiwa haitakiwi kutoka moshi ndani ya siku hizo 3 kwa mafundisho sahihi kabisaa ya Uislamu.

Uislamu haujaacha kitu ambacho m.damu anakiishi sasa ivi na atakiishi hapo baadae

Ila kuna watu wanafnya mambo kimazoea lkn si kma mafundisho.yasemavyo

Ukienda misiba ya kiislamu usitarajie kwenda kula bali ww nenda ukashiriki kwenye mazishi na urudi kwako au kwenu ukale.

#Dini ya haki#
 
Ungewachapa makofi. Ila kwa vijijini kwetu kule kaskazini magharibi Kuna utofauti kidogo. Ukitokea msiba majirani kwanza wanakuja na chochote immediately. Na Kuna vyama vya kuchangiana, wanamchangia vyakula, mboga na kufanya kazi.
 
Msiba ni msiba tu kwa kweli aidha ndugu ama jamaa wasipochangia kuuendesha ama ofisi ya marehemu basi jua tu kuwa wahusika hela itawatoka tu!
 
Na hapo wamekuja rundo hawana hata rambirambi wamefuata nguo za marehemu, nilizigawa kwa hao ndugu na nauli nikawapa.

Mkuu acha tuyaache.

Tamaduni nyingi nu.za.kutupa hata kuchangushana harusini pia si sawa
Daaah mkuu umenena. Mimi sichangii harusi. Za ndugu mpaka huwa naongea kwerikweri.
 
Tuachane na yoooote, kwanini Wali wa kwenye msiba hua mtamu namna ile???? Hua una ladha flani hivi amazing wakikuwekea na Maharage na kachumbari, alooooooo, [emoji39]

Btw, hua sipendi kula Nyama msibani yaani siwezi kabisa.
 
Ungewachapa makofi. Ila kwa vijijini kwetu kule kaskazini magharibi Kuna utofauti kidogo. Ukitokea msiba majirani kwanza wanakuja na chochote immediately. Na Kuna vyama vya kuchangiana, wanamchangia vyakula, mboga na kufanya kazi.
Si mmoja NI wengi na ni watu anafahamiana nao ndio maana wakamwambia ila wengine walilalamika pembeni
 
Kuna baadhi ya vijiji mpaka leo majirani ndio huwa wanapeleka chakula kwa wafiwa...unakuna kila mtu kabeba chochote kitu..hasa mahindi.!
 
Wengine wanaomba mpaka nauli ya kuwarudisha makwao
 
Tuachane na yoooote, kwanini Wali wa kwenye msiba hua mtamu namna ile???? Hua una ladha flani hivi amazing wakikuwekea na Maharage na kachumbari, alooooooo, [emoji39]

Btw, hua sipendi kula Nyama msibani yaani siwezi kabisa.
Chakula chochote cha shughulini kina.ladha ya tofauti [emoji3][emoji3], nimeamua nisijiendekeze nikienda kwenye mgao naomba kachumbali tu tena nione ilivyotengenezwa vinginevyo sili nakula kidogo sana labda tonge mbili basi, hiki chakula ukikizoea unaweza kuwa na tabia ya kutafuta maturubai yalipotundikwa ukakunje mguu na kapilipili na ndiziI yako mfukoni [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kila watu na tamaduni zao
Maadamu hawajavunja katiba ya nchi wewe inakuhusu nini?
Kwani utaratibu wa kupokea rambirambi kutoka kwa waombolezaji umeruhusiwa na nani?
 
Msiba ni msiba tu kwa kweli aidha ndugu ama jamaa wasipochangia kuuendesha ama ofisi ya marehemu basi jua tu kuwa wahusika hela itawatoka tu!
Ayo ni mazoea yenu lkn Uislamu ndo unatufundisha ivo
 
Unakuta "Mijitu" inaenda misibani kwa ajili ya kula tu,ikishakula hiyoooooo inalala mbele!,hata aibu haioni!,unakuta jitu badala liende hata ndani kusalimia wafiwa lenyewe linakomea getini linapiga msosi halafu linalala mbele!!
 
Vingi vya vyakula vinavyoliwa kwenyi baadhi ya misiba(mingi) ni kafara.
Baadhi yavyo ni maelekezo ya kishirikina yaliyoelekezwa kwa wanufaika na kifo cha mhusika.
Sisemi yote ila baadhi. Na katika hii baadhi kama wewe ni mgeni kwani ugeni wako ni mwaliko wa harusini hata uhudumiwe kwa vyakula? Kama kuna ulazima wa kula kwa nini kila mtu asiende na chakula chake?
 
Mwanadamu ana sikukuu kuu tatu.
1. Kuzaliwa
2. Kuoa au kuolewa (japo zi wote wanaobahatika kusherehekea sikukuu hii)
3. Kufa
Hivyo chakula ni muhimu kwa sababu ni sikukuu kwa huyo aliyeondoka. Sasa sikukuu unataka nani achangie tena?? ninavyojua watu wanaokuja msibani huwa wanachanga kiasi. Cha maana misiba isiwe ya siku nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…