- Kama marehemu alikuwa mgonjwa wa akili, kwanini muajiri wake aliendelea kumruhusu kwenda kazini, au unless mwajiri wake naye awe na tatizo la akili!
- Wakati ndugu na mke wa marehemu wakihangaikia kumtafuta marehemu, maafisa wenzie walishirikiana vipi na familia katika kumtafuta, au kwakuwa walijua wapi maiti ilipo hivyo haikuwa na haja ya kumtafuta?
- Pump za kusukuma maji kutoka kwenye reserve kubwa sana ya maji iliopo, zilienda wapi kiasi kwamba mtu, au marehemu akafuate maji kwa ngata na ndoo kisimani kama kijijini?
- Kisima kilipo hakiwezi kuwa barabarani.....kwahiyo marehemu alisikia kiu akaamua kwenda kunywa maji kisimani? Na alieugundua mwili wa marehemu kisimani, naye alisikia kiu hivyo kufuata maji kisimani?
Sihoji sababu za kwanini auwawe (kama ni hivyo). Lakini kama ni ndiyo, basi aina ya uuwaji na mateso yamekuwa too obvious kiasi kwamba huacha maswali mengi zaidi ya majibu! Pia tumeshuhudia maafisa wengi wa tiss wakifanya kazi kwa maslahi yao binafsi na sio ya nchi wala maagizo ya idara na hawajatolewa macho, au kusingiziwa wao ni ernest mushy (white)..ili wauwawe....wapo na wanapeta! Kwakuwa sisi sote ni waja wa mungu....hivi kabla ajent hajauwawa....imeshindikana kabisaa kumuamisha, kumsimamisha kazi...kumpa kifungo cha ndani n.k?......damu ya mtu ni kitu kibaya sana....huwa haimwagiki hivi hivi...ina bei yake!
Kama anahusika na utoaji wa siri kwa vyama vya upinzani....bado sio kosa...tena la kumtoa roho kwakuwa, idara ya uwt ipo kwaajili ya wananchi wote, wa vyama vyote na wasio na vyama! Tiss si
o kwa ajili ya ccm tu, tiss haipo kwa ajili ya kulinda msalahi ya wachache wanaoiibia nchi! Sio kosa kwa ajent wa tiss kutoridhika na mwenendo wa uendeshaji wa idara...! Wanajeshi walimpa mtu 10,000/- ili aende dodoma bungeni kuwaona wabunge wa cdm, ili mambo yawe hadharani! kwanini hwakumtuma kwa wabunge wa ccm?