Kuchukuliwa kwa Roma na wenzake na watu wasiowajua kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia na Inahitaji miwani mikali sana inayoweza kupenya kwa rays!!
Kwanza Roma Mkatoliki mwanamuziki si tishio kwa usalama wa Taifa kabisa hata maudhui ya nyimbo zake ameanza kuimba toka utawala wa Dr Kikwete wala sio tishio kabisa ila anapeleka ujumbe tu.
Ila kutoka na Serikali ya Dr Magufuli kutishia usalama wa maslahi ya wasiopenda kufuata sheria za nchi hii basi Serikali yake imekuwa na maadui kila kona na kila siku wanatafuta namna ya kuitangazia dunia kuwa Serikali ya Dr Magufuli ni kandamizi kitu ambacho si kweli.
Na Imani kabisa walioteka Roma Mkatoliki ni watu wenye lengo la kuichafua Serikali ya Dr Magufuli matope na nia hii ovu utashindwa tu kwasababu Rais anasimamia maslahi ya watanzania wote bila kujali DINI,rangi,kabila wala elimu iliyokuwa nayo.
Serikali ina mambo mengi ya msingi ya kushughulika nayo hawezi kuacha ianze kukata Roma MTU anajitafutia riziki kwa kuimba tena ktk hali ngumu hii ambayo watu wamepunguza hata starehe sasa.