Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Mi nikionaga tukio limetokea na.polisi wako.kimya kama wamepigwa ganzi basi najua litakuwa na uhusiano na lile jeshi jingine la koromije
 
mgongo wa shangazi yako.ulivyo kuwa na akili fupi kama maisha ya inzi chooni.unadhani kila anayepotea ni njama za magufuli acha ufala.roma apotezwe kwa lipi.
Ha haaaaaa. Kwa povu hili jibu tumelipata. Ila kawaambie unaowasujudia,sasa hamtatuteka Bali tutapambana tu.kila mtu ajilinde roho yake.
 
Wakitoka kwa wasanii wanaenda wapi sasa? maana huku walisha pita
-Wafanyabiashara
-Vyombo vya habari
-Upinzani
-
-
-
Ukitaka kujua stori za wafanya biashara na magu na bashite muulize mange
 
Kuchukuliwa kwa Roma na wenzake na watu wasiowajua kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia na Inahitaji miwani mikali sana inayoweza kupenya kwa rays!!

Kwanza Roma Mkatoliki mwanamuziki si tishio kwa usalama wa Taifa kabisa hata maudhui ya nyimbo zake ameanza kuimba toka utawala wa Dr Kikwete wala sio tishio kabisa ila anapeleka ujumbe tu.

Ila kutoka na Serikali ya Dr Magufuli kutishia usalama wa maslahi ya wasiopenda kufuata sheria za nchi hii basi Serikali yake imekuwa na maadui kila kona na kila siku wanatafuta namna ya kuitangazia dunia kuwa Serikali ya Dr Magufuli ni kandamizi kitu ambacho si kweli.

Na Imani kabisa walioteka Roma Mkatoliki ni watu wenye lengo la kuichafua Serikali ya Dr Magufuli matope na nia hii ovu utashindwa tu kwasababu Rais anasimamia maslahi ya watanzania wote bila kujali DINI,rangi,kabila wala elimu iliyokuwa nayo.

Serikali ina mambo mengi ya msingi ya kushughulika nayo hawezi kuacha ianze kukata Roma MTU anajitafutia riziki kwa kuimba tena ktk hali ngumu hii ambayo watu wamepunguza hata starehe sasa.
 
Huyu mzee bhana daah! Hivi magu na mke wake makonda...wanataka waabudiwe ndo waridhike kabisaaa. shenzi zaooo si kwa kutufunga mdomo kiasi hiki.
 
Wakati mnamtafuta Msanii wa Hip Hop Roma Mkatoliki na Moni Centralzone pamoja na Vijana wengine waliotekwa pale Studio za Tongwe Records, Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana yupo katika mtandao wa kijamii wa Instagram anafanya kazi ya kugonga 'LIKES' katika post za Mange Kimambi.

bgv.png
 
Hakuna taarifa iliyosema kakamatwa na polisi na ingekua polisi tungejua yupo kituoni
Ok fine. Lakini nadhani makosa makubwa tulifanya pale alipopotea Saanane. Wengi tumeshamsahau, hata Mbowe humsikii akimuongelea mara kwa mara japokuwa alikuwa msaidizi wake.

Jambo la Saanane lilikuwa rahisi kulipotezea kwasababu alikuwa mwanachadema. Hapo ndipo tulikosea, hakuna aliye salama tena maana wanatujua watanzania moto wetu wa mabua-tunapiga kelele baada ya muda mfupi tunanyamaza. Ni kama maji ya moto, ukiyapa muda yanapoa.
 
Kupotea kwa Roma si tukio la serious ni kutafuta kiki tu

Alikuwa kashapotea kwenye game hivyo basi anatafuta kiki ili arude kwenye chati
 
Halafu alivyo mnafiki anajifanya mzalendo sana,muda wote na bendera ya Tanzania kama gari la DC/RC huku huyo huyo wizara yake imetoa arrest warrant kwa Mange akipita mpaka wowote nchi hii!!
 
Back
Top Bottom