Hii taarifa haijakamilika inamaswali kibao,. Napata shida kuona watu wanavyoanza kuto povu na kutukana watu na mamlaka hovyo hovyo, hata uhakika wa taarifa yenyewe hawana niyakusadikika tu. Rai yangu tuache majungu na porojo na mihemko tujikite kwanza kupata data za kisayansi kuhusu jambo husika, yaweza kuwa ni mabifu yao, au mamlaka za ulinzi na usalama au ujambazi au vinginevyo, na kama ni mamlaka zetu za ulinzi na usalama tunapaswa pia kujua sababu za kuwakamata ili tujue kama wamefanya kwa masilahi mapana ya Taifa au uonevu.Tukumbuke hata kama ni wasanii Hawana kinga ya kutokamatwa kama kweli wamefanya kosa, tusiunganishe mihemko ya Ney kwenye hili sakata