Opera Min
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 890
- 658
Kabla ya leo hisia zilikuwa zinapatikana wapi vile....
ha ha ha hawezi kukujibu hili swali.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabla ya leo hisia zilikuwa zinapatikana wapi vile....
Daah! hii kweli ni conspiracy!!
![]()
![]()
Hapo ndipo kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Moringe Edward Sokoine
Kweli baada ya Kikao cha Bunge kumalizika alikua aondoke na ndege ya Serikali kwenda Dar-es-salaam
Marehemu Sokoine akachagua atatumia Barabara
Heresay: alikuwa kochi la nyuma peke yake na hakufunga mkanda
ajali ilipotokea alirushwa hadi kioo cha mbele na aliummia kifuani sana (km ni headrest ya abiria wa mbele au dreva vilitoboa haya)
Kitu nisichokiamini ni kuwa walimpiga risasi na kumuita Dube eti alipondeponde hilo gari M-Benz mpaka lichakae NO- BIG- NO
Ninachokumbuka nilikuwa Chuoni siku hiyo na tifu ni kuuendeleza msako wake wa WALANGUZI ambao sasa utawavaa viongozi wa juu, wakatihuo alishakatazw kwani alimkamata Waziri Barongo akitaka aswekwe ndani Marehemu Julius Nyerere akamwambia sasa unaifanya kazi visivyo Barongo Mfungulie
Sokoine alikufa kwa ajali ingawa aliuwa na maadui wengi hasa Viongozi wenzake na wale walioupitia Uwaziri mkuu wakiwemo Msuya na Kawawa
![]()
Hakufa kwa ajali ya gari, alikufa kwa kupigwa risasi.
Najua Lumumba mtabisha pamoja na kuwa mnajua huu ndio UKWELI
Bila shaka hata hiyo historia hujaisoma wataka sumbua watu tu hapa! Ati kijiji gani, kata gani, mkoa gani umesoma kweli wewe...!.!.!????
Umenikumbusha 1984, Marehemu Baba yangu alikuwa amenunua magodoro ya Banco ya futi 6X4 6" kwa ajili ya Guest wakti ni Mfanyakazi Wizra ya Afya na Ustawi wa Jamii ilibidi akamatwe eti tu yanawezekana ni ya Haospitalini (wakati ya Hospitalini ni 6'X2 kwa inch 2 tu yaanai yanapishana hasa kwa usumbufu huo hata mm Sokoine sikumkubaliAliamuamua watu wote wawe maskini Tz. Uliza tu utaambiwa jinsi watu walimwaga mafuta sukari na mahela mtoni. Jamaa alikuwa na ndoto za kimaskini wakamdedisha. Wakati ule ukiwaa na Tv home ni issue. Serikali yote itajua na Sokoine hakuwa mbali kukusaka hadi huko kwako. Tz tumepitia mambo ya kishenzi sana.
nikiwa mdogo nilisikia tetesi kwamba kuna mganga wa kisangoma anataka kumrudisha Sokoine kwani alisema bado hajaharibwa huko aliko !! lakini uongozi wa juu wa nchi akiwemo baba wa taifa wakasema itakuwa aibu kwa dunia - maana ametangazwa amefariki tena aibuke mzima tutaonekana vipo sisi watanzania!!
Pia nilisikia toka wa wazee kwamba Prof. Shaba wakati ule pale Mifupa Moi ndiyo alimfanyia postmortem - kama bado anaishi anaweza kutujuza kwamba ilikuwaje kuwaje riport yake original kutotolewa mpaka leo; hata familia hawajawahi kuiona
Ndio sawasawa kabisa alikuwa ni Dr Shaba maana alisema wazi kabisa kwamba kutokana na miiko ya kazi alitakiwa aandike chanzo cha kifo, lakini akapigwapigwa danadana na akaishia kuzuiwa pale Ocean Road.
Dr Shaba aliishia kuwa na maisha ya ajabu ajabu tu.
Nchi hii ina vituko vingivingi tu, na wewe Chinga 1 ni mdogo sana kuweza kuchimba haya.
Mkuu Joka Kuu, usione wengi wetu siku hizi hatupendi sana kuchangia mada zilizokosa weledi kama hizi; kujibizana na watu kama hawa ni kama kumkimbiza kichaa aliyetimka na nguo zako wakati unaoga mtoni. Watu wanakaa barazani, vyumbani na magengeni halafu wanajitungia umbea wakiupa jina utafiti na kuuleta JF kama historia, historia my foot! Lengo hasa la watu hawa ni kuichafua JF ionekane hakuna umakini, hawa watu wametumwa kwani JF inakosesha watu usingizi. Huyo anayejiita Mwansile ndio hao hao, yupo mwingine eti ndiye anaijua historia ya kweli ya Tanganyika kumbe ni porojo tu za barazani uswahilini kutoka kwa wazazi wao waliojaa chuki. Hakuna cha historia, hakuna cha utafiti wala nini; ni histohisia zao tu.Mwansile,
..I am sorry lakini hii habari uliyotuletea ina makosa mengi sana.
..Yaani ina makosa hata pale ambako kulikuwa hakuna sababu yoyote ile kukosea.
..Taarifa ya Mwalimu Nyerere kuhusu kifo cha Waziri Mkuu Edward Sokoine ilikuwa fupi sana, na Mwalimu hakuzungumza lolote kuhusu Sokoine kufariki akitokea ktk ukaguzi wa mashamba ya mahindi.
..Pia habari kwamba Prof.James Shaba alipewa kazi maalum ktk ubalozi wa Tanzania Marekani umezitoa wapi? Mbona huyu Mzee alitumikia pale Muhimbili na kustaafu miaka mingi baada ya Sokoine kufariki?
..Hata majina ya wahusika mbalimbali na nafasi zao wakati wa msiba wa Sokoine pia umekosea. Horace Kolimba, wewe unamuita Harris Kolimba. Huyu hakuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kama unavyodai, bali alikuwa Msaidizi au Katibu wa Waziri Mkuu.
..Baada ya kifo cha Waziri Mkuu Sokoine, Horace Kolimba alipata kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania, JUWATA. Baadaye akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.
..Suala lingine ni kwamba makala yako inaweza kutoa tafsiri kwamba marehemu Edward Sokoine alikuwa mtu mbabe, asiyeheshimu taratibu za kazi, na asiyejua mipaka ya madaraka yake.
..Hii habari kwamba Waziri Mkuu Sokoine alikwenda BOT na kumuamuru gavana wa benki kuu ampe fedha za kuagiza madawa ya mifugo sijui umezitoa wapi. Unadai marehemu Sokoine alikuwa hajui taratibu za utoaji fedha za serikali mpaka akafikia kwenda mwenyewe BOT akachukua Usd 80,000?!
..Naomba nikomee hapa, lakini nakushauri ukafanye utafiti wa kina kuhusu makala yako ili kurekebisha makosa ambayo kwa hakika ni mengi mno.
cc kipuyo, LiverpoolFC, Jasusi, Mag3, Mzee Mwanakijiji
Nimesha anza kupata connection ya utajiri wa lowassa,ila kwa kawawa napata shida kuamini kidogo alishiriki hii kitu kwa madhumuni gani? maana kama ni kwa lengo la kufanya biashara ya kilanguzi mbona mzee mfaume kafa hana hata hela ya kununulia shuka?
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;
1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?
2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?
3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?
4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?
4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?
5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?
6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?
7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?
kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.
Chinga 1.
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;
1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?
2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?
3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?
4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?
4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?
5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?
6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?
7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?
kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.
Chinga 1.
Baada ya miaka 29 Mtoto wa Sokoine ataka mwili wa baba yake uchunguzwe.
MTOTO mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine, Lazaro Sokoine, ameibuka na kutoa madai mazito ya kutaka mwili wa baba yake ufanyiwe uchunguzi, kubaini chanzo cha kifo chake.
Mbali na kutaka uchunguzi huo, Lazaro pia amemuandikia barua Rais Jakaya Kikwete akielezea mlolongo wa matukio mengi, likiwemo mgogoro wa familia hiyo na kuporwa kwa ardhi na mali zake zingine alizoachiwa na Hayati Sokoine.
Lazaro alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, huku akishusha madai mazito dhidi ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Namelock Sokoine, ambaye ni mdogo wake.
Kwa nini mwili wa Sokoine uchunguzwe?
Akielezea sababu za kutaka mwili wa Sokoine uchunguzwe, Lazaro alisema miezi minne kabla ya kifo chake mwaka 1984 baba yake alienda nchini Cuba wakati Lazaro akiwa masomoni nchini humo; Sokoine alimwambia mwanaye huyo kuwa asishangae kusikia amekufa kwa njia yoyote ile ikiwamo kupigwa risasi kwani kuna watu wanamuwinda.
Alisema baada ya baba yake kumueleza hivyo alihoji sababu ya kuwa na hofu hiyo ambapo Sokoine alijibu kuwa hali ya nchi wakati huo chini ya Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa mbaya kutokana na vita dhidi ya wahujumu uchumi.
Mtoto huyo (pichani) ambaye ana hali mbaya kiuchumi, alisema baba yake aliendelea kumwambia kuwa kutokana na hali hiyo, Mwalimu Nyerere alimuongezea ulinzi kutoka askari wanne hadi 14.
Baba alikuja Cuba kwa ajili ya sherehe za uhuru wa nchi hiyo na akaniambia maneno hayo mazito nami nikaenda kuongea na walinzi wake ambao ni Mashaka, Kimaro na Kalbert juu ya hofu hiyo ya baba, alisema Lazaro.
Alisema miezi minne baadaye alipata taarifa ya kifo cha baba yake kupitia Ikulu ya Cuba hali iliyomfanya ayakumbuke maneno ya tahadhari aliyoambiwa juu ya hofu ya kuuawa.
Akieleza sababu nyingine iliyomfanya atake mwili wa baba yake uchunguzwe upya, Lazaro alisema agizo la Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa wakati huo Imran Kombe, kuwataka walinzi wa Sokoine waliokuwa Dodoma watangulie Arusha badala ya kuandamana naye kwenda jijini Dar es Salaam, linatia shaka kwamba kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua.
Alisema kutokana na mazingira hayo, amekuwa akitamani sana kuanzisha harakati za kutaka mwili wa kiongozi huyo maarufu uchunguzwe, lakini hali yake kiuchumi ndiyo inayomkwamisha.
Kwa sasa sina uwezo ila nikipata pesa nitaanzisha mchakato wa kuchunguza kifo cha baba yangu; nimekuwa nikiuliza hili kwa muda mrefu, watu wamenichukia na sasa wananipiga vita hadi ndani ya familia kwa kuhoji suala hilo, mdogo wangu anayeitwa Joseph Sokoine aliyeko ubalozi wa Tanzania nchini Canada aliniambia nisiulizeulize hili suala, wala nisiliingilie kwani siku moja wataningoa macho au kuniondoa duniani, anaongeza Lazaro.
Alisema hivi karibuni wakati mwili wa Sokoine ulipozikwa kwenye kaburi jipya kutoka lile la awali, aliiambia familia yake kwamba isifunge milango ya kaburi ili uchunguzi wa mwili wa baba ufanyike.
Hivi karibuni gazeti hili lilipata kuandika taarifa ya mwili wa Sokoine kuzikwa kwenye kaburi jipya baada ya lile la awali kuharibika na kwamba familia ina mpango wa kutaka kuufanyia uchunguzi mwili huo.
Ikumbukwe kuwa wakati wa kifo chake kulikuwa na mjadala mzito, wengi wakidai aliuawa na kwamba kifo chake kilipangwa na mahasimu wake ndani na nje ya serikali ambao walikerwa na operesheni yake ya kupambana na wahujumu uchumi na mali za taifa.
Kwa mujibu wa sheria, mwili ukishazikwa unaruhusiwa kufanyiwa uchunguzi baada ya miaka 30 na mwakani mwili wa Sokoine utafikisha umri wa miaka 30 tangu ulipozikwa na huo utakuwa muda muafaka kwa wana ndugu hao kutaka kujua ukweli wa kifo cha ndugu yao.
Madai ya kuporwa mali
Akizungumzia suala la kuporwa mali na ardhi, Lazaro alisema ameamua kumuandikia barua Rais Kikwete ili aingilie kati kupata haki zake.
Alisema mwaka 1983, akiwa nchini Cuba Sokoine alimkabidhi kiwanja katika eneo la Kunduchi na hati ya kusaini umiliki wa kiwanja hicho ilipelekwa nchini humo na Paraseko Kone, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Alisema baada ya kumaliza kusaini, Kone alizirejesha hati hizo na kumkabidhi aliyekuwa Mkurugenzi wa Katapila Tanzania kwa wakati huo, Victor Ole Kimesera, ambaye kwa sasa ni Katibu Mtendaji ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA.
Aliongeza kuwa mwaka 1984 alipokuwa kwenye msiba wa baba yake, aliulizia mahala zilipo nyaraka hizo na mama yake alimueleza zilikokuwa na kwamba alipomaliza masomo nchini Cuba alirejea nchini na kukuta kiwanja hicho kimemilikishwa kwa mdogo wake Kilimbe Edward Sokoine.
Alisema baadaye kiwanja hicho kwa kushirikiana na mdogo wake, walikiuza kwa kampuni moja (jina linahifadhiwa), bila ridhaa yake.
Kwa sasa mimi nina matatizo makubwa hata msaada unaotolewa na serikali kwa familia yetu mimi sijawahi kuupata nakuapia hata gari wananikataza nisisogelee na anayefanya hivi ni mdogo wangu, Namelock, alisema Lazaro na kuongeza.
Baba aliniambia kiwanja nimekupatia na pia kuna ngombe dume 600 wa kutumia kujengea hicho kiwanja.
Lazaro alisema kutokana na hali hiyo aliamua kumuandika barua Rais Kikwete Mei 13 mwaka huu na kulazimika kuja jijini Dar es Salaam kujua hatma ya barua yake kama ilishafika mikononi mwa Rais Kikwete.
Nina mke na watoto wawili hadi hivi sasa mke wangu amerudi kwao kwa kukosa matunzo, maisha ya kulala chini na kukosa chakula yananikabili; ninaleta matatizo haya kwako ili uweze kunisaidia kupata haki zangu zilizotaifishwa ili niondokane na maisha magumu niliyonayo ya kukosa sehemu ya kulala huku nikiwa na watoto wadogo chini ya miaka mitano na kukosa pesa ya kujikimu kimaisha, inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Kutokana na madai hayo Tanzania Daima Jumatano iliwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa simu kujua ukweli wa madai hayo.
Mkuu wa mkoa huyo alisema hakumbuki kupeleka fomu kwa Lazaro akiwa masomoni Cuba, lakini alikiri kukutana naye nchini homo.
Nakumbuka nilikutana na kijana huyo wakati huo akiwa masomoni Cuba ila sikumbuki hilo la kumpelekea fomu ya umiliki wa kiwanja, alisema Kone.
Kwa upande wake Namelock ambaye ni mbunge wa viti maalumu (CCM) alikiri kuwa kiwanja anachoeleza kaka yake ni haki yake na kwamba kwa sasa kinamilikiwa na watu watatu kwa njia ya ujanja.
Tumefuatilia bila mafanikio na juzi alipoenda Ikulu nilimwambia afadhali amwandikie barua Rais, na aliandika imefika kwa kuwa msaidizi wa Rais alinipigia, tena ramani ya hicho kiwanja ninayo hadi sasa, alisema Namelock.
Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 eneo la Wami-Dakawa akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.
Chanzo: Tanzania Daima.