Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

Utata wa Kifo Cha Hayati Sokoine

images
images

Hapo ndipo kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Moringe Edward Sokoine
Kweli baada ya Kikao cha Bunge kumalizika alikua aondoke na ndege ya Serikali kwenda Dar-es-salaam
Marehemu Sokoine akachagua atatumia Barabara
Heresay: alikuwa kochi la nyuma peke yake na hakufunga mkanda
ajali ilipotokea alirushwa hadi kioo cha mbele na aliummia kifuani sana (km ni headrest ya abiria wa mbele au dreva vilitoboa haya)
Kitu nisichokiamini ni kuwa walimpiga risasi na kumuita Dube eti alipondeponde hilo gari M-Benz mpaka lichakae NO- BIG- NO
Ninachokumbuka nilikuwa Chuoni siku hiyo na tifu ni kuuendeleza msako wake wa WALANGUZI ambao sasa utawavaa viongozi wa juu, wakatihuo alishakatazw kwani alimkamata Waziri Barongo akitaka aswekwe ndani Marehemu Julius Nyerere akamwambia sasa unaifanya kazi visivyo Barongo Mfungulie
Sokoine alikufa kwa ajali ingawa aliuwa na maadui wengi hasa Viongozi wenzake na wale walioupitia Uwaziri mkuu wakiwemo Msuya na Kawawa

sokoine.jpg


Ukwaju kwa kweli bila hata kujaji kwa namna moja ama nyingine kifo chake kimeandaliwa.

Marehemu E. Moringe apumzike kwa Amani yake BWANA WETU shambani mwake!
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka hata hiyo historia hujaisoma wataka sumbua watu tu hapa! Ati kijiji gani, kata gani, mkoa gani umesoma kweli wewe...!.!.!????
 
Sokoine alikufa kwa ajali ya gari lililoserereka likiendeshwa na raia wa southafrica akijulikana kwa jina la dube hassan dube mengine ni porojo tu
 
Aliamuamua watu wote wawe maskini Tz. Uliza tu utaambiwa jinsi watu walimwaga mafuta sukari na mahela mtoni. Jamaa alikuwa na ndoto za kimaskini wakamdedisha. Wakati ule ukiwaa na Tv home ni issue. Serikali yote itajua na Sokoine hakuwa mbali kukusaka hadi huko kwako. Tz tumepitia mambo ya kishenzi sana.
 
Bila shaka hata hiyo historia hujaisoma wataka sumbua watu tu hapa! Ati kijiji gani, kata gani, mkoa gani umesoma kweli wewe...!.!.!????

We mpuuzi kweli yan,kama nakusumbua usinge soma hii thread wenzako walio thamini hoja zangu mbona wameni elimisha? usinitafutie dhambi bure.
 
Aliamuamua watu wote wawe maskini Tz. Uliza tu utaambiwa jinsi watu walimwaga mafuta sukari na mahela mtoni. Jamaa alikuwa na ndoto za kimaskini wakamdedisha. Wakati ule ukiwaa na Tv home ni issue. Serikali yote itajua na Sokoine hakuwa mbali kukusaka hadi huko kwako. Tz tumepitia mambo ya kishenzi sana.
Umenikumbusha 1984, Marehemu Baba yangu alikuwa amenunua magodoro ya Banco ya futi 6X4 6" kwa ajili ya Guest wakti ni Mfanyakazi Wizra ya Afya na Ustawi wa Jamii ilibidi akamatwe eti tu yanawezekana ni ya Haospitalini (wakati ya Hospitalini ni 6'X2 kwa inch 2 tu yaanai yanapishana hasa kwa usumbufu huo hata mm Sokoine sikumkubali
Kiboko ni alipomkamata Barongo na kuambiwa na Nyerere Huyo muachie na sasa unavuka mipaka ikabidi akasomehwe Romania miezi 6 aliporudi uzi uleule hadi mauti
 
KAKA SOMA HAPA UTAJUA KILA KITU




NYERERE ANATANGAZA KIFO CHA SOKOINE



Ilikuwa majira ya jioni tarehe 12 April 1984 kwenye taarifa ya habari ya saa 10.00 jioni mwaka 1984; kama ilivyokuwa kawaida ya nchi zote za Kikomunist vyombo vya habari vyote vilikuwa ni mali ya serikali, na ilikuwa na desturi ya kila Mtanzania kuhakikisha anakuwa karibu na redio kila inapofika wakati wa taarifa za habari kwa vile ilikuwa ndiyo njia pekee ya kupata habari mbali mbali za hapa nyumbani na nje ya nchi. Ilikuwa ni desturi ya Watanzania popote walipokuwa na wakati wowote inapofika muda wa taarifa ya habari shughuli zote husimama kwa muda wa dakika 10 ili kila mtu asikilize mambo muhimu yaliyotokea ndani na nje ya nchi.

Katika taarifa ya habari ya saa 10 jioni ya siku hiyo ilikuwa tofauti na taarifa za habari za siku nyingine kwa vile siku hiyo mtangazaji wa taarifa ya habari alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na alianza kwa kusema: "Watanzania wenzangu, ndugu yetu, kijana wetu, Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea huko Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogoro akitokea Dodoma kulihutubia bunge; ajali hiyo ilitokea wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua mashamba ya mahindi katika mkoa wa Dodoma na Morogoro. Msafara wa waziri mkuu ulivamiwa na gari aina ya Toyota Land Cruser ya mkimbizi mmoja wa kutoka Afrika ya Kusini kwa jina Dube ambaye alikuwa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mzimbo mjini Morogoro; Dube alisimamishwa na polisi lakini alikaidi na kwa vile alikuwa katika mwendo mkali akasababisha ajali kwa kuigonga gari aina ya Mercedes Benz iliyokuwa imembeba waziri mkuu na kusababisha kifo chake.
Watanzania wenzangu nawaombeni sana mkubali kwamba Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine amefariki kwa ajali ya gari."


<!--[if !vml]--><!--[endif]-->
Hayati Edward Moringe Sokoine
1938-1984
Hayo yalikuwa ni maneno yaliyotamkwa na Nyerere katika taarifa ya habari alipokuwa anatoa taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine. Ukitaka kuthibisha maneno haya Nyerere waweza kuyapata kwenye maktaba ya redio Tanzania, au unaweza pia kuyakuta kwenye maktaba za magazeti ya Uhuru na Daily News.



Ikumbukwe kwamba Sokoine akifariki ndipo vita dhidi ya wahujumu uchumi (mafisadi kwa jina la kizazi kipya) imepamba moto; vita ambayo aliianzisha na alikuwa hachagui wala habagui mkubwa wala mdogo, na wala alikuwa haangalii kwamba wewe ni kigogo au kabwela, wote alikuwa anawashughulikia kikamilifu na sawa sawa bila upendeleo. Sokoine alikuwa anatisha, jina lake mafisadi walipokuwa wakilisikia walikuwa wanajikojolea na hata kuenda haja kubwa bila ya wao wenyewe kujijua, wengine walikuwa wanapata kiwewe na kuzirai na hata wakati mwingine kupoteza maisha; Sokoine alikuwa anatisha, alikuwa hataki mizaha na wala alikuwa habagui bali alikuwa anafuata sheria. Vigogo wote wa nchi hii akiwemo Nyerere ambaye alikuwa Bosi wake Sokoine walikuwa wanamuogopa sana Waziri Mkuu huyu wa aina yake tangu nchi hii ipate uhuru toka kwa Waingereza.
Wahujumu uchumi walitupa magunia ya pesa barabarani, walitupa nyakula magunia kwa magunia, walitupa bidhaa mbali mbali kwa kuogopa kukamatwa na Sokoine! Wahujumu uchumi walikimbilia nchi za jirani kujificha na wengine walikimbilia nchi za mbali kwa kuliogopa jina la Sokoine; ndugu zangu Watanzania mliozaliwa miaka ya mwishoni mwa thamanini na kuendelea Sokoine alikuwa anatisha na pia alikuwa mbabe kwa manufaa ya umma, na kusema kweli huyo ndiye kiongozi pekee tangu nchi hii ipate uhuru wake toka kwa Wakoloni ambaye alikuwa ni kiongozi mwadilifu, mchapa kazi, mbunifu, alikuwa na maono ya mbali, na alikuwa ni mtu wa watu kweli kweli; alikuwa hana makuu, alikuwa na suruali mbili na shati mbili na viatu pair mbili!
Baraza la Mawaziri akiwepo marehem Sokoine wa nne kutoka kushoto mbele. Picha ya
Nkoromo Blog....


Wakati Sokoine ni Waziri Mkuu kulitokea ugonjwa wa mifugo ambao uliua mifugo mingi sana mkoani Arusha; Sokoine alienda bank kuu kumuona Gawana wa bank hiyo wakati huo Mr. Charles Nyirabu ambaye alikuwa Binamu yake Nyerere ili ampe US $ 80,000 kwa ajili ya kuagiza madawa ya mifugo nchi za nje. Alipofika bank kuu na kumueleza Nyirabu kuhusu tatizo hilo Nyirabu alikataa kutoa pesa; Sokoine akamwambia Nyirabu unajua unaongea na nani? Unaongea na Waziri Mkuu wa nchi hii ukifanya mzaha nitakufukuza kazi sasa hivi, Sokoine alisema kwa sauti ya ukali, basi baada ya maneno hayo Gavana Nyirabu akanyanyua simu kuzungumza na binamu yake Nyerere akilalamika kwamba Sokoine anataka apewe pesa baada ya kumkatalia anamtishia kumfukuza kazi; Nyerere alimwamuru kwamba ampe kwa kusema maneno yafuatayo: Ni kweli huyo ni Waziri Mkuu hataki mchezo, anaweza kukufukuza kazi, mpe hicho kiasi anachokitaka. Ndipo Sokoine alipopewa pesa hizo na kuagiza madawa ya mifugo ili ainusuru mifugo ya mkoani Arusha.


Wakati Sokoine anateuliwa na Nyerere kuwa waziri mkuu tulikuwa na mfumo wa chama kimoja na Nyerere wakati huo alikuwa anajulikana kwa jina maarufu kama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi hivyo system yake ilikuwa imejenga utaratibu kwamba mtu yeyote anapokuwepo katika mkusanyiko wa watu (mikutano, sherehe, au kongamano) lazima anapoanza kuzungumza aanze kwa kusema: "Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi" halafu wanaokusikiliza wananyanyua mkono wa kulia juu kwa nguvu na huku ukiwa umekunja ngumi kwa kusema: "Zidumu" hivi ndivyo system ya Nyerere ilivyokuwa imemtengenezea kiongozi wake umaarufu na watu wote wakaiga na ikatokea bahati mbaya umepanda jukwaani ukajisahau kusema maneno hayo ya kumsifia Mwenyekiti wa chama, basi watu wote watakuona kama wewe si mtu wa kawaida, lazima utakuwa na mapungufu fulani, na wakati mwingine waweza hata kuadhibiwa na kitengo chake cha usalama wa taifa kwa kosa la kutomtambua Mwenyekiti wa chama cha Kikomunist! Sokoine alipoingia tu madarakani akayaona hayo makosa na akawasahihisha Watanzania kwamba wasiseme tena kwamba "Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi" bali waseme "Zidumu Fikra Sahihi za Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi" aliongeza neno Sahihi kwa kusisitiza kwamba siyo kila fikra za Mwenyekiti ni sahihi, kitu ambacho hakikumfuhisha Nyerere kwa vile alikuwa ni mtu aliyekuwa anajiamini kupita kiasi na alikuwa hapendi ushauri wa mtu yeyote wala alikuwa hategemei kwamba kuna mtu anayeweza kumkosoa kutokana na jinsi alivyokuwa anaogopewa; lakini Sokoine alimkosoa na kumrekebisha na Watanzania wakajisahihisha kwa hilo.


Vita dhidi ya wahujumu uchumi aliyoianzisha Sokoine ilivuma kila kona ya nchi hii, mijini na vijijini wahujumu walinywea, nakumbuka kule mkoani Kilimanjaro kuna mto unaitwa mto kikavu basi baada ya Sokoine kuanza kuwakamata wahujumu uchumi, baadhi ya wafanyibiashara wa mkoani humo walichukuwa magunia kwa magunia ya sukari waliyokuwa wameyaficha kwa ajili ya kufanya ulanguzi na kuyatupa ndani ya mto Kikavu na maji ya mto huo yakageuka maji ya sukari; watu waliokuwa wanaishi kando kando ya mto huo walikuwa hawanunui sukari bali walikuwa wanachota maji ya mto huo kuyaweka majani kuyachemsha na kunywa chai! Sokoine alisema ninaanza kuwashughulikia mawaziri wangu, nikimaliza kuwapekuwa namfuata Nyerere naye nikampekue. Kutokana na kauli ya kijasiri na ya aina yake iliyotolewa na Sokoine, Nyerere alipata wakati mgumu sana, na alihangaika vibaya mno, wakati huo Sokoine ana umaarufu mkubwa kuliko Nyerere, wananchi wametokea kumuamini Sokoine kama yeye ndiyo rais wa nchi kutokana juhudi zake za kweli na za vitendo za kuusaidia umma. Jina la Sokoine wakati huo linatajwa na hata watoto wadogo, katika mazingira kama haya na kulingana na tabia ya Nyerere hakufurahishwa kabisa na hali kama hiyo. Kipindi hiki ndicho Sokoine alipompa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa (Waziri katika ofisi ya rais wakati huo) siku 7 arudishe pesa za umma shilingi milioni sitini ambazo aliuza meli ya serikali lakini hakupeleka pesa hazina bali akaziweka mfukoni mwake! Sokoine alimwambia Kawawa kama ifuatavyo: "Nakupa Siku Saba Urudishe Pesa za Wananchi, Ukishindwa Nitakupeleka Radio Tanzania Uwaambie Watanzania kwa Njia ya Radio Pesa Zao Umezipeleka Wapi?; Mimi Naenda Dodoma Kuhutubia Bunge, Nikirudi Nipate Majibu" Wakati Sokoine anaenda kulihutubia bunge Dodoma, Kawawa akarudi kijijini kwake huko Liwale mkoani Lindi na Nyerere akafanya safari ya ghafla ya kwenda kumuona rafiki yake mpenzi rais wa Mozambique wakati huo Samora Machele. Nyerere alipofika kwa Samora alimlalamikia kwamba nimemchagua waziri mkuu Sokoine lakini ananipeleka puta kweli kweli hata najuta kwa nini nilimchagua, na sijui nifanyeje? Samora akamshauri kwamba amfukuze kazi; Nyerere akamuambia siwezi kumfukuza kazi kwa vile Wananchi wanampenda kuliko wanavyonipenda mimi, na jina lake linavuma na ni kubwa kuliko mimi, hivyo nikimgusa tu wananchi hawatakubali kabisa! Nyerere akarudi Dar es Salaam na huku akiwa na hofu kwamba Sokoine akimalizana na mawaziri wake zamu inayofuata ni yake (Mwenzio akinyolewa na Wewe Tia Maji)! Kabla ya siku saba hazijaisha Sokoine anakufa kwa ajali ya gari iliyotokea huko Dakawa nje kidogo ya mji wa Morogoro.


Kwa muda wote huo Kawawa bado alikuwa yupo huko kijijini kwake Liwale mkoani Lindi lakini aliposikia tu taarifa za kifo cha Sokoine alirudi Dar es Salaam siku hiyo hiyo na kusisitiza kwamba Sokoine azikwe mara moja bila ya kuchelwa, lakini aliambiwa haiwezekani kiongozi wa kitaifa azikwe haraka haraka kiasi hicho, hivyo zikafuatwa taratibu za kuchunguza mwili wake kama inavyokuwa kwa watu wengi kabla ya kuzikwa. Ni mila na desturi za kila jamii kote duniani kuwaruhusu wanafamilia wa marehemu kuwa huru na mwili wa marehemu kama ambavyo ilivyo tabia na desturi zetu sisi Watanzania, lakini utawala wetu umekuwa na utaratibu tofauti na zilivyo nchi zingine hasa akifa kiongozi wa kitaifa wanafamilia hawana haki na mwili wa marehemu: tunakumbuka alipokufa makamu wa rais Ali Juma pia wanafamilia hawakuwa huru na mwili wa ndugu yao; au alipokufa Gavana wa Bank Kuu Balabi pia wanafamilia hawakuruhusiwa si kuuona tu mwili wa marehemu bali hata hawakuruhusiwa kuliona kaburi lake! Inaonekana huyu alikabidhiwa kwa malaika na kuzikwa huko mbinguni!
Wajerumani walipinga kifo cha Sokoine, hawakuamini kwamba Sokoine amekufa kwa ajali ya gari kwa vile alikufa akiwa amepanda Mercedes Benz magari ambayo yanatumiwa na viongozi wote mashuhuri duniani, ni magari yanayoaminiwa kiusalama kulingana na yalivyodizainiwa kwamba hata itokee ajali ya namna gani si rahisi kiongozi kufa; Wajerumani walipinga vikali wakiilamu serikali ya Tanzania kwamba inalichafua jina la Benz na kwa kufanya hivyo wanawavunjia soko la magari yao yasiendelee kununuliwa na nchi mbali mbali duniani! Wajerumani walipinga wakisema hata kama Mercedes Benz iliyokuwa imembeba Waziri Mkuu ingekuwa imegangana na SCANIA BOUBLE TRAILER ikiwa na mzigo wa tani 40 bado isingeweza kumuua Waziri Mkuu, sasa imetokeaje agongane na Toyota Land Cruiser afe! Haiwezekani kabisa, walihoji Wataalamu wa Benz wa Ujerumani. Kulingana na msimamo huo kampuni inayotengeneza magari ya Mercedes Benz ambayo ni ya kutoka nchini Ujerumani, ilituma ujumbe wa watu 7 kuja kuchunguza ajali inayodaiwa imemuua Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine, walipofika hapa nchini na kumuona Nyerere kuhusu mpango wao huo wa kutaka kufanya utafiti juu ya kifo cha Sokoine, Nyerere aliwaomba waondoke nchini mara moja kwa vile alishawaomba Watanzania waamini kwamba Sokoine amekufa kwa ajali ya gari na Watanzania wameshaamini! Sasa wakichunguza wakileta ushahidi mwingine Watanzania watamuelewaje wakati yeye ni rais wa nchi!? Wajerumani waliondoka lakini hawakufurahishwa na kitendo cha magari yao ya Benz kusingiziwa uongo ambao unaweza kuyadhuri katika soko la ushindani.
Kuanzia wakati huo hadi leo hii kifo cha Sokoine kimebakia Siri ya Taifa kama ambavyo alisema IGP Said Mwema kwamba swala Dr. Stephen Ulimboka la kuteswa na maafisa wa Ikulu ni Siri ya Taifa!
Pamoja na kwamba kifo cha Sokoine kimebakia kuwa Siri kubwa ya Taifa tangu mwaka 1984 hadi leo hii, lakini Watanzania wengi wamekuwa wakijiuliza maswali mengi bila ya majibu, hasa wanapojaribu kuitafsiri kauli ya Nyerere ya kusema: "Nawaombeni Muamini kwamba Sokoine Amefariki kwa Ajali ya Gari!" Hivi mtu aliyefariki kwa ajali ya gari unahitajiwa kuombwa uamini kwamba mtu fulani amekufa kwa ajali ya gari, wakati ajali yenyewe inaonekana!? Na kama Mercedes Benz imeweza kusababisha ajali kwa kiongozi wetu wa kitaifa, kijana wetu mpendwa Edward Moringe Sokoine kwanini tusingewaruhusu Wajerumani wathibitishe ajali hiyo ili waweze kutulipa fidia kwa kutuulia kiongozi wetu!?




Tuliogopa kitu gani kuwaruhusu Wajerumani kufanya uchunguzi huru, ili wakithibitisha ubovu wa magari yao waturudishie gharama zetu zote tulizotumia kuyanunua magari hayo!? Je, hatuoni kwamba kiuchumi hatuchukua hatua sahihi!? Je, huu siyo ufisadi wa aina yake!?
Nikirudi upande wa Tanzania ni kwamba wote tunafahamu fika kwamba msafara wa Waziri Mkuu unakuwa na magari yasiyopugua sita yakitanguliwa na pikipiki yenye king'ora ambayo inakuwa mbele kuyatahadharisha magari yote yaliyopo barabarani kwamba sasa mkubwa anakuja hivyo wekeni vyombo vyenu vya usafiri pembeni. Kulingana na ukweli huu ni kwamba ni vigumu kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kuamini kwamba Waziri Mkuu akiwa katika msafara anaweza kupata ajali ya kugongwa na gari iliyotokea kichochoroni! Kwa vile hata akatokea mwendawazimu akaamua kukaidi na kuendelea kuendesha gari, asingeweza kumgonga Waziri Mkuu kwa vile kuna magari yasiyopungua matatu ambayo yapo yanatangulia mbele ya gari la Waziri Mkuu, hivyo magari hayo kwanini yasiligonge hilo gari lililokaidi amri ya kusimama!? Ni kwanini gari hilo liachwe mpaka liende likamgonge Waziri Mkuu!? Na kwanini Waziri Mkuu alikufa peke yake katika ajali hiyo!? Na baada ya kufa kwanini hakuna tume yoyote huru iliyoundwa kuchunguza kifo cha kiongozi wa kitaifa!? Kwanini badala ya kuunda tume ya kuchunguza kifo chake, badala yake Nyerere anawaomba Wananchi waamini kwamba Sokoine amefariki kwa ajali ya gari!? Je, ndugu zangu Watanzania mpaka hapo hatuoni kwamba Nyerere na utawala wake walikuwa na chuki binafsi na Sokoine!? Inakuwaje Waziri Mkuu afariki kifo ambacho siyo cha kawaida na serikali ibaki kimya bila ya kuchukuwa taratibu zinazotakiwa, bali ikiwashawishi Wananchi waamini kwamba kiongozi wao amekufa kwa ajali ya gari!? Kwanini tangu mwaka 1984 hadi leo serikali bado haijawachukulia hatua wale wote waliokuwepo katika msafara wa Sokoine kwa kuwafikisha mahakamani na kujibu mashitaka kwa kusababisha kifo cha waziri mkuu kwa uzembe wao!? Au ndiyo desturi na mila zile zile za Nyerere za kulindana na kuhamishana huku na kule!? Hivi Watanzania tumekuwa watu wa namna gani, yaani Watanzania wote tunaombwa tuamini kwamba mtu amekufa kwa ajali ya gari na sisi tukakubali na tumekaa kimya! Kolimba akapewa kipaza sauti aeleze ni jinsi gani CCM imepoteza dira na mwelekeo ile kukifikisha kipaza sauti puani akafa! CCM wakasema amepaliwa na mate na madaktari wakasema hivyo hivyo! Wauza madini wakauwawa na kunyang'anywa madini yao, na kesi ilipoenda mahakamani maafisa wa serikali waliokuwa wanashutumiwa wakaachiwa huru kama vile mchezo wa kuigiza! Leo ametekwa Dr. Stephen Ulimboka ameteswa na kutupwa porini na maafisa wa Ikulu; serikali inasema hiyo ni siri ya taifa! Kwa utaratibu huu tumefika wapi na tunaelekea wapi!? Pamoja na sinema zote hizi bado akina Mzee Malecela wanasema hawataki rais apunguziwe madaraka, bali wanataka aongezewe madaraka zaidi ili afanye kazi vizuri!
Baada ya Sokoine kufariki dunia watu wote walioshuhudia kifo chake walibadilishiwa kazi na kupewa kazi zingine ikiwa ni pamoja na wengine kupelekwa kufanya kazi katika balozi zetu huko nchi za nje: Mzee Harris Kolimba wakati kikitokea kifo cha Sokoine alikuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye alihamia Dar es Salaam na kuwa katibu mkuu wa CCM, ambaye naye mwaka 1993 alikorofishana na Nyerere baada ya kusema CCM haina Dira na imepoteza mwelekeo, baada ya maneno hayo alikufa kifo cha kutatanisha! Wengine waliomfanyia postmortem kwenye hospitali ya Muhimbili kama akina Dr. Shaba walipewa kazi maalumu huko kwenye ubalozi wetu nchini Marekani na kadhalika!
Baada ya kifo cha Sokoine ndipo vita dhidi ya wahujumu uchumi ilipozikwa rasmi kule Dakawa na hata zile pesa alizokuwa anazidai Sokoine kwa niaba ya umma toka kwa Kawawa hakuna aliyezifuatilia tena, bali tukaendelea na maneno yale yale ya kinafiki ya majukwaani ya kukemea rushwa kwa mkono wa kulia na huku mkono wa kushoto unapokea rushwa na kuisukumia mfukoni! Wakati Kawawa akiuza meli ya umma, tulikuwa na meli moja tu, sasa waziri katika ofisi ya rais ameuza meli moja tu inayomilikiwa na serikali bila ya rais kujua licha ya kwamba magazeti yalindika sana!
Nyota ya Sokoine iliibuliwa toka mafichoni na rais wa kwanza wa nchi moja ya Afrika magharibi ijulikanayo kama Guinea Conakry Mr. Ahmed Sekou Toure. Rais Ahmed Sekou Toure alifanya ziara ya kiserikali hapa nchini, alipotembelea wilaya ya Mondoli alionyeshwa watoto wawili wa kimasai ambao walikuwa yatima; Sekou Toure aliwaomba hao watoto awachukue akawalee; alipewa watoto hao wawili aondoke nao, na Sokoine wakati huo alikuwa ni afisa katika wilaya Monduli aliombwa awasindikize hao watoto hadi Guinea Conakry pamoja na rais huyo wa Guinea.
Walipokuwa kwenye ndege Sokoine na Rais Ahmed Sekou Toure walipata muda mwingi wa kuongea mambo mengi sana yanayohusu nchi za kiafrika kwa ujumla, na pia walipofika Guinea Sokoine na Ahmed Sekou Toure waliweza kuongea mambo mengi yanayohusu Tanzania na Guinea kwa ujumla; Rais Ahmed Sekou Toure akawa amevutiwa sana na fikra pevu za kijana Edward Moringe Sokoine na kumwandikia Nyerere barua kwamba amchukue Sokoine awe karibu naye kwani ni mtu mwenye busara sana anaweza kumsaidia kwenye uongozi wake; baada ya mapendekezo hayo ndipo Nyerere alipomsogeza Sokoine karibu na yeye, na kweli alikiona kipaji cha Sokoine licha ya kwamba hakukipenda, lakini kwa sisi wanyonge huyu ndiye alitakiwa awe kiongozi wetu. Wale watoto waliosindikizwa na Sokoine kwenda Guinea wamesharudi nchini na mmoja wao ni Dr. Toure yupo katika moja ya hospitali za hapa nchini anafanya kazi.
Inasemakana kuna mtoto wa kiume wa Marehemu Edward Moringe Sokoine ambaye amajitahidi kwa muda mrefu sana ili aingie kwenye siasa kwa kutaka kugombea ubunge kwenye jimbo lake la Monduli, lakini ameshindwa kabisa kulingana na hali ya siasa za chuki za nchi yetu; kama baba yako alikosa au alikosana na Nyerere na kwa bahati mbaya akafa kabla hajaomba msamaha, basi jina lake likiambatana na wanae na kizazi chake chote wataendelea kupata adhabu! Hiyo ndiyo Tanzania ninayoijua mimi inayosifiwa kuwa kisiwa cha amani na utulivu!
Pamoja na ujasiri aliouonyesha Edward Moringe Sokoine lakini hakuna hata mwanasiasa, mwanaharakati wala raia anayetaka kulitaja jina lake hasa tunapopambana na wimbi kubwa la ufisadi, kinyume chake wote hawa wanasema eti angelikuwepo Nyerere yote haya yasingetokea! Nyerere hakupambana na ufisadi hata siku moja, bali alikuwa hodari wa kupiga blaa blaa za majukwaani ambazo hazina vitendo vyovyote bali Sokoine ijitolea kufa kwa kuupigania umma wa Watanzania. Utawala wa Nyerere ndiyo ulioanzisha ufisadi nchi hii hasa baada ya kuanzisha utaratibu wa kutonunua kitu chochote bila ya kupata kibali toka kwa wale walioteuliwa kuvitoa vibali hivyo; hakuna kibali kilichotolewa bure, lazima utoe kitu kidogo kwa wateule!
Sokoine alikuwa ni kiongozi wa pekee si hapa Tanzania tu bali hata kidunia ukichunguza kwa makini, si rahisi kwa viongozi wengi duniani kusimamia haki wakati anaonekana akifanya hivyo atamuudhi boss wake; viongozi wenye ujasiri wa aina hiyo kwa dunia ya leo niwakutafuta; Sokoine alikuwa si mtu wa mitandao wala majungu, alikuwa ni mtu anayefanya mambo kulingana na taratibu zilizowekwa; alikuwa habagui watu kimatabaka kama ilivyo viongozi wengi wa nchi hii; Sokoine alikuwa hana hulka ya Udini kama alivyokuwa Boss wake na viongozi wengi wa serikali yetu; Sokoine alikuwa anajua kuna watu wanaitwa Watanzania na raia wake ni Watanzania basi. Tupende tusipende Sokoine pamoja na kwamba hakudumu kwa muda mrefu lakini Sokoine ni kiongozi wa aina yake katika karne ya 20, na kusema kweli itatuchukuwa karne nyingi mbele kuja kumpata Sokoine mwingine katika nchi hii.
Hivi karibuni tumesherehekea miaka 50 ya uhuru, lakini fumbo la kifo cha Sokoine limebakia kuwa Siri ya Taifa, na hata jina lake pia limebakia nao kuwa shubiri katika majukwaa ya siasa hapa nyumbani. Ningependa kuwaasa wanasiasa na wanaharakati kwamba kama wana nia ya kweli ya kuukomboa umma wa Watanzania ambao umekuwa katika mikono ya wagandamizaji kwa zaidi ya miongo mitano, basi hawana budi kulienzi jina la Sokoine kwenye kila jukwaa la kutetea maslahi ya umma kama ishara ya Ukombozi wa kweli; pia ningependa kuwaonya wanasiasa na wanaharakati waache kulitaja jina la Nyerere kwenye majukwaa yanayotetea haki za umma kwa vile kulitaja jina hilo ni kama kutonesha kidonda cha dhuluma na ugandmizaji uliozagaa kila pembe ya nchi hii, ugandamizaji ambao umeufanya umma kuwa masikini wa kupindukia wakati watawala wakiendelea kujineemesha wao na vizazi vyao vingi tu vijavyo!
Sokoine amefariki tumeachwa wakiwa, tuombe mungu atushushie Sokoine mwingine kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa 2015; tusilale tukeshe tukiomba kwani tukifanya hivyo mungu aweza kusikia kilio chetu; tusikate tamaa, tuendelee kuomba bila ya mapumziko, mungu ana huruma sana, hawezi kukubali umma wake uendelee kuteseka miaka mingine 50 ijayo; miaka 50 tuliyoteseka inatosha.
Katiba mpya iweke wazi akifa kiongozi wa kitaifa katika mazingira tatanishi ni lazima iundwe tume huru kuchunguza kifo chake.


close.gif
MWISO WA STORY
 
nikiwa mdogo nilisikia tetesi kwamba kuna mganga wa kisangoma anataka kumrudisha Sokoine kwani alisema bado hajaharibwa huko aliko !! lakini uongozi wa juu wa nchi akiwemo baba wa taifa wakasema itakuwa aibu kwa dunia - maana ametangazwa amefariki tena aibuke mzima tutaonekana vipo sisi watanzania!!

Pia nilisikia toka wa wazee kwamba Prof. Shaba wakati ule pale Mifupa Moi ndiyo alimfanyia postmortem - kama bado anaishi anaweza kutujuza kwamba ilikuwaje kuwaje riport yake original kutotolewa mpaka leo; hata familia hawajawahi kuiona


Hata nami nilipataga kusikia hili! Kazi kweli kweli ipo!
 
Mwansile,

..I am sorry lakini hii habari uliyotuletea ina makosa mengi sana.

..Yaani ina makosa hata pale ambako kulikuwa hakuna sababu yoyote ile kukosea.

..Taarifa ya Mwalimu Nyerere kuhusu kifo cha Waziri Mkuu Edward Sokoine ilikuwa fupi sana, na Mwalimu hakuzungumza lolote kuhusu Sokoine kufariki akitokea ktk ukaguzi wa mashamba ya mahindi.

..Pia habari kwamba Prof.James Shaba alipewa kazi maalum ktk ubalozi wa Tanzania Marekani umezitoa wapi? Mbona huyu Mzee alitumikia pale Muhimbili na kustaafu miaka mingi baada ya Sokoine kufariki?

..Hata majina ya wahusika mbalimbali na nafasi zao wakati wa msiba wa Sokoine pia umekosea. Horace Kolimba, wewe unamuita Harris Kolimba. Huyu hakuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kama unavyodai, bali alikuwa Msaidizi au Katibu wa Waziri Mkuu.

..Baada ya kifo cha Waziri Mkuu Sokoine, Horace Kolimba alipata kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania, JUWATA. Baadaye akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

..Suala lingine ni kwamba makala yako inaweza kutoa tafsiri kwamba marehemu Edward Sokoine alikuwa mtu mbabe, asiyeheshimu taratibu za kazi, na asiyejua mipaka ya madaraka yake.

..Hii habari kwamba Waziri Mkuu Sokoine alikwenda BOT na kumuamuru gavana wa benki kuu ampe fedha za kuagiza madawa ya mifugo sijui umezitoa wapi. Unadai marehemu Sokoine alikuwa hajui taratibu za utoaji fedha za serikali mpaka akafikia kwenda mwenyewe BOT akachukua Usd 80,000?!

..Naomba nikomee hapa, lakini nakushauri ukafanye utafiti wa kina kuhusu makala yako ili kurekebisha makosa ambayo kwa hakika ni mengi mno.

cc kipuyo, LiverpoolFC, Jasusi, Mag3, Mzee Mwanakijiji
 
Last edited by a moderator:
Ndio sawasawa kabisa alikuwa ni Dr Shaba maana alisema wazi kabisa kwamba kutokana na miiko ya kazi alitakiwa aandike chanzo cha kifo, lakini akapigwapigwa danadana na akaishia kuzuiwa pale Ocean Road.

Dr Shaba aliishia kuwa na maisha ya ajabu ajabu tu.

Nchi hii ina vituko vingivingi tu, na wewe Chinga 1 ni mdogo sana kuweza kuchimba haya.


..pale karibu na Ocean Road Hospital ndipo alipokuwa akiishi Prof.Shaba, kabla na baada ya kifo cha Sokoine.

..Prof.Shaba hakuzuiwa wakati wowote ule, aliendelea na kazi yake kama Mkuu wa Kitengo cha Pathology ktk Hospitali ya Muhimbili mpaka alipostaafu kazi.

..tatizo la Prof ni kwamba alikuwa anatumia pombe kupita kiasi, na akishakunywa kauli zake zilikuwa za maudhi. kuna kipindi alipigwa risasi ya mguu na askari waliokuwa wanalinda karibu na nyumbani kwake kutokana na ukorofi wake akishapata kinywaji.

cc rahim_baharia
 
Last edited by a moderator:
Mwansile,

..I am sorry lakini hii habari uliyotuletea ina makosa mengi sana.

..Yaani ina makosa hata pale ambako kulikuwa hakuna sababu yoyote ile kukosea.

..Taarifa ya Mwalimu Nyerere kuhusu kifo cha Waziri Mkuu Edward Sokoine ilikuwa fupi sana, na Mwalimu hakuzungumza lolote kuhusu Sokoine kufariki akitokea ktk ukaguzi wa mashamba ya mahindi.

..Pia habari kwamba Prof.James Shaba alipewa kazi maalum ktk ubalozi wa Tanzania Marekani umezitoa wapi? Mbona huyu Mzee alitumikia pale Muhimbili na kustaafu miaka mingi baada ya Sokoine kufariki?

..Hata majina ya wahusika mbalimbali na nafasi zao wakati wa msiba wa Sokoine pia umekosea. Horace Kolimba, wewe unamuita Harris Kolimba. Huyu hakuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kama unavyodai, bali alikuwa Msaidizi au Katibu wa Waziri Mkuu.

..Baada ya kifo cha Waziri Mkuu Sokoine, Horace Kolimba alipata kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania, JUWATA. Baadaye akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

..Suala lingine ni kwamba makala yako inaweza kutoa tafsiri kwamba marehemu Edward Sokoine alikuwa mtu mbabe, asiyeheshimu taratibu za kazi, na asiyejua mipaka ya madaraka yake.

..Hii habari kwamba Waziri Mkuu Sokoine alikwenda BOT na kumuamuru gavana wa benki kuu ampe fedha za kuagiza madawa ya mifugo sijui umezitoa wapi. Unadai marehemu Sokoine alikuwa hajui taratibu za utoaji fedha za serikali mpaka akafikia kwenda mwenyewe BOT akachukua Usd 80,000?!

..Naomba nikomee hapa, lakini nakushauri ukafanye utafiti wa kina kuhusu makala yako ili kurekebisha makosa ambayo kwa hakika ni mengi mno.

cc kipuyo, LiverpoolFC, Jasusi, Mag3, Mzee Mwanakijiji
Mkuu Joka Kuu, usione wengi wetu siku hizi hatupendi sana kuchangia mada zilizokosa weledi kama hizi; kujibizana na watu kama hawa ni kama kumkimbiza kichaa aliyetimka na nguo zako wakati unaoga mtoni. Watu wanakaa barazani, vyumbani na magengeni halafu wanajitungia umbea wakiupa jina utafiti na kuuleta JF kama historia, historia my foot! Lengo hasa la watu hawa ni kuichafua JF ionekane hakuna umakini, hawa watu wametumwa kwani JF inakosesha watu usingizi. Huyo anayejiita Mwansile ndio hao hao, yupo mwingine eti ndiye anaijua historia ya kweli ya Tanganyika kumbe ni porojo tu za barazani uswahilini kutoka kwa wazazi wao waliojaa chuki. Hakuna cha historia, hakuna cha utafiti wala nini; ni histohisia zao tu.
 
Sokoine alipigwa risasi na mlinzi wake katika utosi kwa kutumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti(silencer).Baada ya hapo gari yake ililengeshwa kwenye gari ya Damisan Dube ambaye alikuwa akishangaa gari lile la Waziri Mkuu likimjia kwa kasi ya ajabu.Aliwahi kutokea mlango wa abiria na kuangukia nje kabla ya kufuatwa na kuondolewa haraka eneo lile.Jamaa walimpakia Sokoine kwenye gari nyingine akiwa ameshakata roho!Yakafanyika mawasiliano ya haraka kuhusu "AJALI" hiyo ili kuondoa hali ya mashaka.Masikini Dube alitiwa kibano cha nguvu na hakuwa akielewa kilichotokea hata yeye kuhusishwa na ajali ile.Kesi ilifanyika haraka na baadaye aliachiwa na baada ya hapo tu "alipotezwa" kimoja!
Angalizo: Katika msafara wa kiongozi, akiwa katika gari ndogo (Salon car) anakuwa anakaa kiti cha nyuma kwa wakati huo.Sokoine alikuwa katika Mercedes Benz 280 D,kiti cha nyuma na gari yake iligongwa kwa mbele na siyo nyuma alipokuwa amekaa na kufunga mkanda1 Iweje gari kama ilivyoonekana katika picha imegongwa mbele anapokaa dereva na mlinzi wasiumie vibaya hata kufa,aje afe Sokoine aliyekaa nyuma???? Halafu magari mawili ya defence ya kushoto na kulia yasigongwe ligongwe la Waziri Mkuu????
Mwenye ubongo na atafakari!
 
Nimesha anza kupata connection ya utajiri wa lowassa,ila kwa kawawa napata shida kuamini kidogo alishiriki hii kitu kwa madhumuni gani? maana kama ni kwa lengo la kufanya biashara ya kilanguzi mbona mzee mfaume kafa hana hata hela ya kununulia shuka?

Kawawa aliutaka Urais, na ikumbukwe Sokoine alishaandaliwa kumrithi Nyerere, hivyo watu wanahisi Kawawa alicheza rafu ili apate Urais.
 
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.

Nafikiri Kolimba alifahamu A to Z, kuhusu kifo cha Sokoine maana yeye ndio alikuwa Mkuu wa msafara kwa siku hiyo.
 
Wadau ningependa kujua chanzo halisi cha kifo cha waziri mkuu wa zamani hayati sokoine kwa vile alipo fariki nilikua bado sijazaliwa,nimejaribu kupitia baadhi ya makala mbali mbali naona hazielezi mazingira halisi ya ajali hiyo kwa msingi huo napenda kushare na nyie maswali kadhaa;

1.ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine ilikua ya aina gani? kupinduka kwa gari,kugongana uso kwa uso? ama kugonga mti?

2.katika hiyo ajali hayati sokoine na dereva wake walifia papo hapo ama hospitali?

3.kama ni ajali ya magari kugongana uso kwa uso vipi kuhusu dereva na watu walio kuwemo kwenye gari ya pili walikufa ama wako hai?

4.kama wakk hai vipi dereva alichukuliwa hatua gani? maelezo ya dereva yanasemaje?

4.Ushahidi wa mashuhuda wa hiyo ajali wanasemaje?

5.Uchunguzi wa polisi unatoa maelezo gani kuhusu ajali iliyo sababisha kifo cha sokoine? ni uzembe wa madereva? au ni matatizo ya kiufundi? ama ni conspiracy?

6.Eneo la ajali ni wapi? i mean kijiji,kata,wilaya na mkoa gani na ilikua mda gani mchana au usiku?

7.KWA NINI HAKUNA SOKOINE DAY KWENYE KALENDA YA NCHI YETU KAMA ILIVYO NYERERE DAY NA KARUME DAY?

kuna maswali mengi sana ila kwa leo naomba niyaweke hayo muhimu.

Chinga 1.

Kuna Kitabu kinaitwa Morani tulikisoma A-level, kinaelezea harakati za Sokoine, japo hakutumia jina halisi, na mwishowe tunaona jinsi mhusika Dongo (Sokoine), anavyouliwa kwa kukatwa ulimi na wahujumu uchumi
 
Mtoto wa Sokoine.jpg
Baada ya miaka 29 Mtoto wa Sokoine ataka mwili wa baba yake uchunguzwe.
MTOTO mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine, Lazaro Sokoine, ameibuka na kutoa madai mazito ya kutaka mwili wa baba yake ufanyiwe uchunguzi, kubaini chanzo cha kifo chake.

Mbali na kutaka uchunguzi huo, Lazaro pia amemuandikia barua Rais Jakaya Kikwete akielezea mlolongo wa matukio mengi, likiwemo mgogoro wa familia hiyo na kuporwa kwa ardhi na mali zake zingine alizoachiwa na Hayati Sokoine.

Lazaro alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, huku akishusha madai mazito dhidi ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Namelock Sokoine, ambaye ni mdogo wake.

Kwa nini mwili wa Sokoine uchunguzwe?

Akielezea sababu za kutaka mwili wa Sokoine uchunguzwe, Lazaro alisema miezi minne kabla ya kifo chake mwaka 1984 baba yake alienda nchini Cuba wakati Lazaro akiwa masomoni nchini humo; Sokoine alimwambia mwanaye huyo kuwa asishangae kusikia amekufa kwa njia yoyote ile ikiwamo kupigwa risasi kwani kuna watu wanamuwinda.

Alisema baada ya baba yake kumueleza hivyo alihoji sababu ya kuwa na hofu hiyo ambapo Sokoine alijibu kuwa hali ya nchi wakati huo chini ya Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa mbaya kutokana na vita dhidi ya wahujumu uchumi.

Mtoto huyo (pichani) ambaye ana hali mbaya kiuchumi, alisema baba yake aliendelea kumwambia kuwa kutokana na hali hiyo, Mwalimu Nyerere alimuongezea ulinzi kutoka askari wanne hadi 14.

“Baba alikuja Cuba kwa ajili ya sherehe za uhuru wa nchi hiyo na akaniambia maneno hayo mazito nami nikaenda kuongea na walinzi wake ambao ni Mashaka, Kimaro na Kalbert juu ya hofu hiyo ya baba,” alisema Lazaro.

Alisema miezi minne baadaye alipata taarifa ya kifo cha baba yake kupitia Ikulu ya Cuba hali iliyomfanya ayakumbuke maneno ya tahadhari aliyoambiwa juu ya hofu ya kuuawa.

Akieleza sababu nyingine iliyomfanya atake mwili wa baba yake uchunguzwe upya, Lazaro alisema agizo la Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa wakati huo Imran Kombe, kuwataka walinzi wa Sokoine waliokuwa Dodoma watangulie Arusha badala ya kuandamana naye kwenda jijini Dar es Salaam, linatia shaka kwamba kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua.

Alisema kutokana na mazingira hayo, amekuwa akitamani sana kuanzisha harakati za kutaka mwili wa kiongozi huyo maarufu uchunguzwe, lakini hali yake kiuchumi ndiyo inayomkwamisha.

“Kwa sasa sina uwezo ila nikipata pesa nitaanzisha mchakato wa kuchunguza kifo cha baba yangu; nimekuwa nikiuliza hili kwa muda mrefu, watu wamenichukia na sasa wananipiga vita hadi ndani ya familia kwa kuhoji suala hilo, mdogo wangu anayeitwa Joseph Sokoine aliyeko ubalozi wa Tanzania nchini Canada aliniambia nisiulizeulize hili suala, wala nisiliingilie kwani siku moja wataning’oa macho au kuniondoa duniani,” anaongeza Lazaro.

Alisema hivi karibuni wakati mwili wa Sokoine ulipozikwa kwenye kaburi jipya kutoka lile la awali, aliiambia familia yake kwamba isifunge milango ya kaburi ili uchunguzi wa mwili wa baba ufanyike.

Hivi karibuni gazeti hili lilipata kuandika taarifa ya mwili wa Sokoine kuzikwa kwenye kaburi jipya baada ya lile la awali kuharibika na kwamba familia ina mpango wa kutaka kuufanyia uchunguzi mwili huo.

Ikumbukwe kuwa wakati wa kifo chake kulikuwa na mjadala mzito, wengi wakidai aliuawa na kwamba kifo chake kilipangwa na mahasimu wake ndani na nje ya serikali ambao walikerwa na operesheni yake ya kupambana na wahujumu uchumi na mali za taifa.

Kwa mujibu wa sheria, mwili ukishazikwa unaruhusiwa kufanyiwa uchunguzi baada ya miaka 30 na mwakani mwili wa Sokoine utafikisha umri wa miaka 30 tangu ulipozikwa na huo utakuwa muda muafaka kwa wana ndugu hao kutaka kujua ukweli wa kifo cha ndugu yao.

Madai ya kuporwa mali

Akizungumzia suala la kuporwa mali na ardhi, Lazaro alisema ameamua kumuandikia barua Rais Kikwete ili aingilie kati kupata haki zake.

Alisema mwaka 1983, akiwa nchini Cuba Sokoine alimkabidhi kiwanja katika eneo la Kunduchi na hati ya kusaini umiliki wa kiwanja hicho ilipelekwa nchini humo na Paraseko Kone, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Alisema baada ya kumaliza kusaini, Kone alizirejesha hati hizo na kumkabidhi aliyekuwa Mkurugenzi wa Katapila Tanzania kwa wakati huo, Victor Ole Kimesera, ambaye kwa sasa ni Katibu Mtendaji ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA.

Aliongeza kuwa mwaka 1984 alipokuwa kwenye msiba wa baba yake, aliulizia mahala zilipo nyaraka hizo na mama yake alimueleza zilikokuwa na kwamba alipomaliza masomo nchini Cuba alirejea nchini na kukuta kiwanja hicho kimemilikishwa kwa mdogo wake Kilimbe Edward Sokoine.

Alisema baadaye kiwanja hicho kwa kushirikiana na mdogo wake, walikiuza kwa kampuni moja (jina linahifadhiwa), bila ridhaa yake.

“Kwa sasa mimi nina matatizo makubwa hata msaada unaotolewa na serikali kwa familia yetu mimi sijawahi kuupata nakuapia hata gari wananikataza nisisogelee na anayefanya hivi ni mdogo wangu, Namelock,” alisema Lazaro na kuongeza.

“Baba aliniambia kiwanja nimekupatia na pia kuna ng’ombe dume 600 wa kutumia kujengea hicho kiwanja.”

Lazaro alisema kutokana na hali hiyo aliamua kumuandika barua Rais Kikwete Mei 13 mwaka huu na kulazimika kuja jijini Dar es Salaam kujua hatma ya barua yake kama ilishafika mikononi mwa Rais Kikwete.

“Nina mke na watoto wawili hadi hivi sasa mke wangu amerudi kwao kwa kukosa matunzo, maisha ya kulala chini na kukosa chakula yananikabili; ninaleta matatizo haya kwako ili uweze kunisaidia kupata haki zangu zilizotaifishwa ili niondokane na maisha magumu niliyonayo ya kukosa sehemu ya kulala huku nikiwa na watoto wadogo chini ya miaka mitano na kukosa pesa ya kujikimu kimaisha,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Kutokana na madai hayo Tanzania Daima Jumatano iliwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa simu kujua ukweli wa madai hayo.

Mkuu wa mkoa huyo alisema hakumbuki kupeleka fomu kwa Lazaro akiwa masomoni Cuba, lakini alikiri kukutana naye nchini homo.

“Nakumbuka nilikutana na kijana huyo wakati huo akiwa masomoni Cuba ila sikumbuki hilo la kumpelekea fomu ya umiliki wa kiwanja,” alisema Kone.

Kwa upande wake Namelock ambaye ni mbunge wa viti maalumu (CCM) alikiri kuwa kiwanja anachoeleza kaka yake ni haki yake na kwamba kwa sasa kinamilikiwa na watu watatu kwa njia ya ujanja.

“Tumefuatilia bila mafanikio na juzi alipoenda Ikulu nilimwambia afadhali amwandikie barua Rais, na aliandika imefika kwa kuwa msaidizi wa Rais alinipigia, tena ramani ya hicho kiwanja ninayo hadi sasa,” alisema Namelock.”

Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 eneo la Wami-Dakawa akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Chanzo: Tanzania Daima.



Pata 'info' zaidi..
 
Back
Top Bottom