Kwa wanaojua kinachoendelea kwa swala la Baba wa Taifa Kanisani,haya ya nani kamuua Mwalimu kinachopaswa kufanyika ni confession nakisha kila mtu kuendea sawa na maisha yake.Kwa kuwa kuna Watanzania na Wanafamilia wana amini kuwa mwalimu hakufa kifo cha kwaida [Natural death].
Kama kuna Mtu anaitajika kutubu atubu vinginevyo madhara yake nimakubwa sana kwa kuwa imani ujenga.Wanaoamini Mwalimu aliuawa na kuna Mtanzania naye anatuhumiwa kujua kifo hicho basi ni vyema kuconfesse ufahamu wake juu ya swala zima hata kama kuna wageni walimzidi kete aseme kwa kuwa tunajua Tanzania ni Taifa andamwa kwa kuwa lina madini na malighafi nyingi na wajanja wa dunia wanajua njia nyepesi ya kuja kuchukua ni kuwaondoa walinzi wakuu wa maliasili hzio kisha unapatikana uchocholo wa kuchota.
Kuna baadhi ya wananchi wanajua hata baadhi ya viongozi wanavyoingizwa kwenye mitego bila kujijua [Brackmail] kisha wanabaki kuwa watumwa wa mawakala wa wezi wageni ambao wamengineer issue nzima ya kumuingiza kiongozi matatizoni,na kwa kuwa viongozi ni watu wasio na tabia ya kusema wazi basi wanabaki kufuata maagizo ya mablackmail, Je wataishi chini ya kivuli cha blackmail mpaka lini,hatimae ukweli lazima ujulikane tu.Je wangesema jamani kuwa fulani kanilubuni hakika uku mbeleni ingemletea mtu heshima,kulubuniwa ni udhaifu wa kibinadamu sio dhambi,japo utahukumiwa na umma lakini ukweli utafahamika.
Si ajabu maskini Mzee BWM alikuja kuonyeshwa document za kampuni zenye address ya IKULU pasipo yeye kujua nani kafanya biashara ikulu?Mungu alimuuliza adamu huko wapi, adamu kwa aibu akaitika rabeka Mungu niko huku !! umefanya nini !! akasema ni huyu mdada ulienipa ndie ndie ndie!!!!!!!!!!.
Toba itamuweka mt huru daima yeye na kizazi chake na kupitia toba Mungu anafungua milango ya ukweli kufahamika.Ukweli ucheleweshwa lakini hafungwi daima bali ujifungua kutoka kwenye uongo daima.