Utata wa maelezo juu ya kifo cha Katibu na motive ya Mkandamizaji

Utata wa maelezo juu ya kifo cha Katibu na motive ya Mkandamizaji

Anecheza mchezo hatari halafu kasepa marekani in case akitaka kikamatwa.
Kuna muda nakuwa tofauti kidogo.. ukweli anao marehemu.. ingawaje lazima kuna gap ipo mahala fulani ambayo kama wapelelezi wakiitumia vizuri ukweli utajulikana kuhusu ni nini hasa kimetokea...
 
Wadau, leo kumesambaa taarifa kwenye vyombo vya habari kutoka kwa kamanda wa polisi Muliro akielezea sababu za kujiua katibu wa Feel Free Church kutokana na uchunguzi wa awali.

Maelezo ya kamanda yanapeleka kwenye hitimisho moja kuwa, Mama Mchungaji (Monica) na marehemu hawakuwa na mahusiano na kwamba katibu amejiua kwa kukataliwa baada ya kuwa akimtongoza Monica. Inasemekana marehemu, alikuwa akimtumia jumbe za kimapenzi, jambo ambalo lilimfanya Monica akiwa na mama mtu mzima(hakutajwa jina) kufika nyumbani kwa marehemu siku moja kabla ya kifo chake kwa leo kumuhabarisha kuwa hataki kutumiwa jumbe hizo na wala hawezi kuwa nae kwa vile yeye ni mke wa mtu.

UTATA MTUPU…!

Kwa sisi wapenda documentaries za crime, hizi sababu zinaleta utata kuliko majibu. Katika matukio ya vifo kama hivi vinavyohusika mapenzi au fedha, lazima kitu kiitwacho MOTIVE kiwe established.
Katika wahusika wote watatu katika tukio hili, mtu mwenye motive kubwa ni Masanja. Haijalishi alikuwepo nchini au hakuwepo wakati tukio linatokea.

Ukifikiri kwa kina, haina maana ya mtu kujinyonga kisa kukataliwa, tena na mke wa mtu. Na ni mke wa mtu gani eti anakwenda nyumbani kwa anayemtongoza ili kumkataa? Kama amekuwa anamkataa siku zote, alishindwaje kumtaarifu mumewe kuwa katibu amevuka mstari? Badala yake akaenda na mama mtu mzima nyumbani kwa marehemu ili kumtaarifu juu ya kumkataa?

Je, ni kweli marehemu alijinyonga? Au amenyongwa halafu cover up imefanyika?

Je, inawezekana Masanja aligundua haya mahusiano na kutumia njia za kimafia kumueliminate marehemu huku yeye akiwa nje ya nchi ili kukwepa kushukiwa?( Mambo ya kawaida haya kwenye Investigation Discovery)

Uzuri kamanda amesema maelezo yake ya leo ni uchunguzi wa awali na bado wanaendelea. Naamini majibu yatapatikana tu, ila Masanja Mkandamizaji aangaliwe kwa ukaribu sana. Ndiye mtu pekee mwenye MOTIVE ya kuchezesha mambo. Simu za wahusika wote zikaguliwe kwa kina, na majibu yatakuwemo humo.
Eeeehhhh,
 
Huenda kaenda huko ili ajitoe kabisa kwenye msala.. Asihusishwe
Ukingalia sana crime documentaries za USA utakutana nacho sana hiki kitu. Watu wanatuma watu wengine kuua spouses wao afu wao wanakuwa sehemu nyingine labda na watu wengine so inawapa alibi. Mtu mmoja hawezi kuwepo sehemu mbili tofauti kwa wakati mmoja. So huenda jamaa alifanya hivi kama ALIBI
 
Haya mambo yanafikirisha! Unfortunately inaonekana dogo ana familia dhaifu kufatilia hili kwa kina maana kama una akili timamu hesabu zote zinagoma! Hakuna anayeomba mabaya kwa Masanja lakini hili swala hata kama ukifunika kombe bado linatatiza sana ....
 
Hapa bongo kila MTU ni FBI.

Naombeni mniambie aliyemuua Dr. Mvungi.!
Haha mzee kwa FBI hii ishu ilikuwa ishakwisha mchana kweupeeeee😂😂😂tena mauaji yanayohusisha mapenzi ndo rahisi kukamata watu maana huwa wanatumia emotions zaidi kuliko thinking.
 
Suspicious no 2
Kwa nini masanja akatuma mtandaoni post ya kumsamehe mkewe siku moja baada ya tukio? Alikuwa na haraka gani? Alikuwa anajua kinachoendelea na kitakachotokea!?
Na kwa nini amsamehe mkewe kama ilikuwa anatongozwa tu? Je mke kutongozwa ni kosa la mke mpaka asamehewe? Hapa kuna maswali yasiyo na majibu. Angesema amemsamehe marehemu hapo kidogo ingeleta mantiki.

Lakini kumsamehe mtongizwaji ambaye alikuwa anakataa mahusiano kwa kulinda heshima ya mmewe ni kosa kubwa alilofanya Masanja katika kupanga mipango yake. Ningekuwa askari sasa hivi Masanja angekuwa anajibu maswali hayo kwa kuanzia uchunguzi.
 
Kweli hapo kwenye kumkataa angempiga block na angeendelea na usumbufu angemtaarifu mumewe amfukuze hapo kanisani

Unatongozwq kisha unamfuata nyumbani anayekutongoza kumkatalia?? Haingii akilini
Haiingii akilini,mke wa bwana mkubwa "kumfuata nyumbani,katibu akisindikizwa na mama ambaye jina lake halijatajwa"!!
,Kwa nini asingeripoti katika uongozi wa kanisa???
 
Na kwa nini amsamehe mkewe kama ilikuwa anatongozwa tu? Je mke kutongozwa ni kosa la mke mpaka asamehewe? Hapa kuna maswali yasiyo na majibu. Angesema amemsamehe marehemu hapo kidogo ingeleta mantiki.

Lakini kumsamehe mtongizwaji ambaye alikuwa anakataa mahusiano kwa kulinda heshima ya mmewe ni kosa kubwa alilofanya Masanja katika kupanga mipango yake. Ningekuwa askari sasa hivi Masanja angekuwa anajibu maswali hayo kwa kuanzia uchunguzi.
Aliwahi kupost bila kufikiria ,madhara yake.
 
Ah mkali gwala hii! Mambo ya udetective haya. Unasamehe mkeo kutongozwa na kumkataa mtongozaji?
 
Polisi ifikie mahala, wawe na akili wanapo toa taarifa za uchunguzi karne ya 21. Yaani kumkataa mtu hadi ukodi rafiki wa kukusindikiza? Unaenda kwake ili iweje?

Hapa Masanja achunguzwe-Kuna Movie ka icheza.
Hahahaaa yaani nimechekaaa
 
Haya mambo yanafikirisha! Unfortunately inaonekana dogo ana familia dhaifu kufatilia hili kwa kina maana kama una akili timamu hesabu zote zinagoma! Hakuna anayeomba mabaya kwa Masanja lakini hili swala hata kama ukifunika kombe bado linatatiza sana ....
Kumbuka kuna uhusiano wa "baba mchungaji na katibu wa kanisa",kama kijana alikataliwa,walishindwa nini kumuita katika uongozi wa kanisa?? Badala yake wakaenda kwake kumuambia aache kutuma ujumbe wa mapenzi??
 
Mkuu umenikumbusha channel yangu pendwa...Investigation Discovery..kuna wabobevu huko na manguli wa hizi kazi,kuna mamilioni ya kesi kama hizi za Masanja ambazo zimekua solved.
Inapatikana wapi hiyo
 
Kuhusu mlango kufungwa kwa ndani mtu kama ni funguo ndogo anaweza ufunga kwa nje na funguo kurushwa ndani ili ionekane kajifungia.na hospitalini wamesema kuwa hakuwa na alama yeyote ya mapambano kabla y kifo chake zaidi ya kujinyonga.
 
Back
Top Bottom