Utata wa siku 3 za Yesu na hesabu zetu

Sawa kwa utaratibu huu ni kuwa Ijumaa inaanza Alhamisi Jioni hadi Ijumaa jioni- siku ya kwanza; Jumamosi inaanza Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni-siku ya pili; Jumapili inaanza Jumamosi jioni hadi Jumapili jioni-siku ya tatu. Lakini yeye alifufuka jumapili asubuhi kabla siku ya tatu haijakamilika!
 
hakika
 
usiwe mzito kuelewa walikuwa wanahesabu siku sio masaa
Mkuu nakubaliana na wewe walikuwa wanahesabu usiku na mcha kuwa ndio siku moja. sasa kama alizikwa ijumaa jioni siku ya kwanza iliisha jumamosi jioni, ya pili ikaanza jumamosi jioni. huoni hapo tunapata siku moja na nyingine kama nusu hivi. Think out of the box.
 
Ndi hivyo mkuu . Kuna watu wanalazimisha kwamba ijumaa jioni mpaka jumapili kabla ya alfajiri ni siku tatu. Hoja yangu ni kuwa hakuna ushahidi kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa. Mwenye huo ushahidi atupatie. Tunajifunza
 
Maandiko yanataka USIKU 3 na MCHANA 3 , ili siku 3 zikamilike, nnje ya hapo hakuna siku tatu msilazimishe mambo
umenena vyema mkuu. Na mojawapo ya vitu tunavyovifanya kwa kuwaamini viongozi wetu ni kuamini kuwa kuna siku tatu kati ya Ijumaa jioni na Jumapili alfajiri. Pia kuamini kwamba Yesu alisulubiwa siku ya ijumaa
 
Kwa kweli hizi hesabu za makanisani zinapingana na hesabu zilizoandikwa hii ni hatari kwa afya ya mwanadamu
Kweli mkuu. Tunaamini mambo ya uongo kabisa kwa mambo ya wazi hivi, je yale yenye utataje. Ia maana mambo mengi tunayoaminishwa si ya kweli
 
Inclusive Reckoning
The only way we can harmonize all of these apparently contradictory statements of Jesus is to understand them in the light of inclusive reckoning of time. This was the method used throughout the Bible in computing time, and we must apply the same method now, unless we want mass confusion. The unreasonable insistence upon the use of twentieth century English idioms of speech to interpret first century Greek or Hebrew has led to some extreme views indeed. Jesus and His friends spoke and wrote in harmony with the common literacy usage of the day, and that usage recognized inclusive reckoning of time. In simple language, this means that any part of a day was counted as a whole day.

Nadhani mtoa mada utapata kitu hapa
 
Mkuu, ukihesabu 'siku' in terms of a time period utakuwa umeharibu. Wayahudi wakishaona jua limezama na nyota tatu... zimetamalaki angani basi kitendo hicho kilihesabiwa kuwa ni mwanzo wa siku nyingine hivyo ikiwa Yesu labda angefufuka siku ya Jumapili saa 10 alfajiri au siku ya Jumapili saa 6 mchana still bado ingehesabika kuwa ni siku ya tatu.

Ebu soma Kitabu cha Esta 4:16 Vs Esta 5:1 kisha leta mrejesho hapa kunako Jukwaa.
Kama Wayahudi wangekuwa wanahesabu siku kama tunavyohesabu sisi, Esta angekwenda kumuona Mfalme siku ya nne na siyo siku ya tatu.
 
Mkuu ungeweka kwa Kiswahili ingekuwa safi maana sisi wengine lugha ya Malkia haipandi.
 
Mkuu ungeweka kwa Kiswahili ingekuwa safi maana sisi wengine lugha ya Malkia haipandi.
Kwa ufupi tu mkuu ina maana kwa uhesabuji wa siku kipindi hicho hata kama tukio lilitokea kwa kipindi kifupi katika siku ilihesabika ni siku moja hiyo kwa hiyo Yesu kufa ijumaa ilihesabika ni siku moja halisi kukaa kaburini siku iliyofuata na kufufuka siku ya tatu zilihesabika siku nzima hata kama haikutimia kwa masaa
 
Ndiyo maana yake boss wangu!
 
Alizikwa jioni na siyo saa tisa .
Mathayo27:57 Ilipokuwa jioni, akaja mtu mmoja tajiri mwenyeji wa Armathaya, jina lake Yosefu. Yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akamwendea Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Basi, Pilato akaamuru apewe. 59 Yosefu akauchukua ule mwili akauzungushia sanda safi ya kitani, 60 akauweka ndani ya kaburi lake jipya alilokuwa amelichonga katika mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake
 
Wakati huo hakukuwa na jumamosi wala jumapili zenu.
Kumbuka! ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya kwanza
 
Kumbuka aliwaambia kuwa atakaa kaburini siku tatu usiku na mchana kama Yona alivyokaa tumboni mwa Samaki siku tatu usiku na mchana. Hakusema tu siku tatu Bali siku tatu usiku na mchana. kwa kiingereza alisema Three days and three nights

Mathayo 12:40 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa katika tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku,+ ndivyo Mwana wa binadamu atakavyokuwa katika moyo wa ardhi siku tatu mchana na usiku
 
Mkuu, kwani point yako ni nini hasa?
 
Inaweza kuwa kweli.

Lakini hebu tena soma haya mafungu kwa kiswahili na kiingereza halafu utafakari. Kwamba Yesu asema atakaa kaburini three days and three night, halafu wewe useme hata akikaa masaa matatu ya ijumaa ni siku nzima.Sikubaliani na wewe.

Mathayo12:38 Ndipo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu kwa kumwambia: “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”+39 Akawajibu: “Kizazi kiovu na chenye uzinzi* kinaendelea kutafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya nabii Yona.+ 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa katika tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku,+ ndivyo Mwana wa binadamu atakavyokuwa katika moyo wa ardhi siku tatu mchana na usiku.

The Scribes and Pharisees Ask for a Sign
Mathew12:38 Then some of the scribes and Pharisees answered, saying, “Teacher, we want to see a sign from You.”

39 But He answered and said to them, “An evil and adulterous generation seeks after a sign, and no sign will be given to it except the sign of the prophet Jonah. 40 For as Jonah was three days and three nights in the belly of the great fish, so will the Son of Man be three days and three nights in the heart of the earth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…