Utatu ni wa majukumu si mamlaka. Yesu ni Mungu lakini si Mkuu kuliko Baba

Mungu ni mmoja tu, YHWH.

Yesu hakuwahi kudai yeye ni Mungu. Anglesea yeye ni Mungu, wayahudi wangemuua kwa mawe. May be hata kwa Pilato asingefika.
1. Ukisoma injili zote, Yesu hakudai kuwa yeye ni Mungu, wala kujipa nafasi moja na Mungu. Kitu cha msingi pia, takamatsu mashtaka Wayahudi walipelekea kwa utawala wa Warumi, kuwa anajiita Mfalme wa Wayahudi. Angejiita ni Mungu, wangempiga mawe kama Torati inavyosema. Kwa hiyo Yesu hakudai kuwa yeye ni Mungu.
2. Soma Matendo ya Mitume (Acts of Apostles). Kuna mara kadhaa maombi ya mitume yameandikwa, wakimuomba Mungu na sio Yesu. Na hata kwenye kuhubiri kwao hawakusema Yesu ni Mungu, bali mtumishi maalum wa Mungu/mwana wa Mungu. Ni muhimu hilo.
3. Injili ya Yohana, ndo yenye kuleta some ideas juu ya uungu wa Yesu. Lakini Injili hii imeandikwa takribani miaka 70 tangu Yesu amekufa. Hapa tayari kuna theology zilishaanza kujengwa, na ikazichukua hizo. Lakini injili za mwanzoni kabisa hazina hii dhana.
4. Utatu kama dhana imekuja kujengwa baadae, na sio dhana iliyokuwa katika kanisa la mitume wa kwanza. Muingiliano wa imani za Kirumi, kigiriki, imani za Asia ilichangia kutokea kwa baadhi za theolojia zilizomo kwenye Ukristo leo hii.
 
Umesamehewa. Tuishie hapo. Mavuno ni mengi watenda kazi ni wachache. Tuukomboe wakati, tutumie muda mwingi kutimiza agizo kuu la Yesu. Ubarikiwe
 
Yohana 10:30
"Mimi na Baba tu umoja."

Yohana 10:33
"Wewe u mtu tu, wajifanya kuwa Mungu." - Waliona Yesu kama anajifanya Mungu.

Yohana 8:58
"Kabla Abrahamu hajazaliwa, Mimi niko."

Kutoka 3:14
"MIMI NIKO AMBAYE NIKO."

Marko 2:5-7
"Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.
Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"


Mathayo 9:2-3
"Dhambi zako zimesamehewa.
Mafarisayo wakajibu - Huyu anamamlaka gani ya kusamehe dhambi?"

Mathayo 28:17
"Nao walipomwona, wakamsujudia."

Yohana 20:28
"Thomaso akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu!"

Wakolosai 2:9
"Katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili."
2. Soma Matendo ya Mitume (Acts of Apostles). Kuna mara kadhaa maombi ya mitume yameandikwa, wakimuomba Mungu na sio Yesu. Na hata kwenye kuhubiri kwao hawakusema Yesu ni Mungu, bali mtumishi maalum wa Mungu/mwana wa Mungu. Ni muhimu hilo.
Matendo 7:59-60
"Na walipokuwa wakimpiga kwa mawe, Stefano aliomba, akisema:
Ee Bwana Yesu, pokea roho yangu.
Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, akasema,
Bwana, usiwahesabie dhambi hii."

Kumtaja Yesu kama "mtumishi wa Mungu" haikufuta Uungu wake, kama ilivyoandikwa pia kuwa Yesu "alitwa mdogo kuliko malaika kwa muda kidogo" - Waebrania 2:9 lakini ni Mungu aliyejifunua katika mwili - 1 Timotheo 3:16.

Lete hizo nakala za kale - tuthibitishe!!
 
Umesamehewa. Tuishie hapo. Mavuno ni mengi watenda kazi ni wachache. Tuukomboe wakati, tutumie muda mwingi kutimiza agizo kuu la Yesu. Ubarikiwe
Amen - Hata mimi nimekusamehe kwa kujibu kwa hisia bila maandiko ili Mungu apate kukusamehe.
 
Uungu wa Yesu haukusubiri kura ya Nicaea.
Mitume walimwita "Bwana wangu na Mungu wangu - "Yoh 20:28" kabla ya Constantine kuzaliwa.

Stefano alimwomba Yesu - Matendo 7:59 kabla ya Nicea kufikirika.

Yesu alisamehe dhambi (Marko 2:5) — mamlaka ya Mungu pekee.

Na Biblia haisemi "Homoiusios" wala "Heteroousios" inasema -
"Katika Yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili." - Wakolosai 2:9.

SAYANSI NA FALSAFA HUBADILIKA LAKINI NENO HALIBADILIKI.
Kwanza Arius alikataa Yesu kuwa wa asili moja na Baba halafu Falsafa ya Nicaea (325 AD) ikasema Homoousios Kwamba ni wa asili moja – ὁμοούσιος.

Baadaye wakaja wanafalsafa Wengine wakapendekeza Homoiusios - Kwamba wanafanana kwa asili na Mjadala ukaendelea hadi Konsili ya Constantinople 381 AD ambapo nayo ikasisitiza Uungu kamili wa Kristo.

Lakini Mitume hawakutumia neno la Mungu kifalsafa wala hawakuwa na kuyumba yumba na kubadilika badilika - walimwona Yesu, wakamgusa, wakamwabudu — wakamshuhudia kuwa ni Mungu aliye hai.

Niko standby hiyo saa nane au tisa ukishamtumikia Kaisari.
 
Yohana 10:30
"Mimi na Baba tu umoja."

Yohana 10:33
"Wewe u mtu tu, wajifanya kuwa Mungu." - Waliona Yesu kama anajifanya Mungu.

Yohana 8:58
"Kabla Abrahamu hajazaliwa, Mimi niko."

Kutoka 3:14
"MIMI NIKO AMBAYE NIKO."
Kuhusu Yohana, injili iliandikwa takribani miaka 60-70 toka Yesu. Nadhani unajua juu ya fasihi simulizi. Injili za mwanzo ni Marko, Mathayo na Luka.
Mathayo 9:2-3
"Dhambi zako zimesamehewa.
Mafarisayo wakajibu - Huyu anamamlaka gani ya kusamehe dhambi?"
Alipewa mamlaka na Mungu. Naye aliwapa mamlaka wanafunzi wake kuponya na kusamehe dhambi. Haikuwapa wanafunzi wake uungu.
 
GPT inaanza kukudanganya sasa
 
DR Mambo Jambo Kaisari anahitaji umetengenezee kiasi gani tukusaidie kumlipa ili uje utoe hoja zako hapa??
 
Nakubaliana nawe 💯
 
Hagawanyi majukumu vipi mbona kuna malaika ambao wanafanya kazi zake?
 

Yn 14:1-3​

Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo
 
Mathayo 28:19
[19]Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Go ye therefore, and teach all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost:

Kama ROHO Mtakatifu sio NAFSI ujue hata baba na mwana sio NAFSI. Kwa jina la Roho Mtakatifu... Hakuna maelezo yanayosema utatu Una NAFSI 2 (it is wrong)Ila nikukumbushe kama Wewe ni shahidi WA Yehova utaweza kujàdiliana na mashahidi wenzio Tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…