Utawala wa Rais, Samia Suluhu Hassan unastahili kongole kwa barabara za Mitaa na taa za barabarani

Utawala wa Rais, Samia Suluhu Hassan unastahili kongole kwa barabara za Mitaa na taa za barabarani

Hayo mambo ya kongole na pongezi ndio uchawa wenyewe. Taa za barabarani ni wajibu wa serikali na ni haki ya wananchi sababu wanalipa Kodi hata kama mradi ni WA mkopo wa IMF.

Kasome notes za mtoto wako za civics jikumbushe rights and responsibilities za citizen.

Hivi ukimpa ujauzito mke wako au mwenza wako unataka tukupongeze? Huo si wajibu wako? Na mkeo au mwenza si haki yake kubeba mimba?
 
Kumbuka uzi huu siyo hoja ya kumjibu Mheshimiwa, Polepole
Ninafahamu kuwa ana hoja makini na inapaswa siyo tu kujibiwa ila kujibiwa kwa umakini na watu makini.

Vipi Broh! Kwenye hakuna barabara za mitaa zenye mataa? Jibu taratibu kama mtu asiye na hisia kali.

Peleka ujumbe, traffic light hazituhusu kama mustakabala mzima wa nchi yaani uchaguzi unatindiganywa!

Nchi inauzwa, wewe unatwambia traffic light? Za nini?
 
Peleka ujumbe, traffic light hazituhusu kama mustakabala mzima wa nchi yaani uchaguzi unatindiganywa!

Nchi inauzwa, wewe unatwambia traffic light? Za nini?
Una hoja nzuri sana Broh! Na huwa nafuatilia nyuzi zako jithidi kitu kidogo tu kuwa "open -minded" usifocus sana kwenye upande mmoja. Hata shetani ana uzuri wake.
 
Hayo mambo ya kongole na pongezi ndio uchawa wenyewe. Taa za barabarani ni wajibu wa serikali na ni haki ya wananchi sababu wanalipa Kodi hata kama mradi ni WA mkopo wa IMF.

Kasome notes za mtoto wako za civics jikumbushe rights and responsibilities za citizen
Basi kama ni wajibu wao tuseme " Wamejitahidi kuwajibika" huoni kama wameonesha sehemu mojawapo ya matumizi ya kodi za Wananchi Mkubwa? Tusibeze kila kitu, wana udhaifu wao sawa, ila tuwe genuine kiasi...
 
Huo mkopo ulisimamiwa na Serikali ipi Broh!... Tusibanange na kubagaza kila jitihada, siyo sawa.
By the way hata Mimi siungi mkono kila jambo ila kwenye mazuri nasema.
Vitu petty sana hivyo! Hivi hii nchi ni ya kutegemea mkopo kuweka taa za barabarani kweli?

Nadhani kabla ya kusifia fikiria kwanza ugumu wa jambo husika. Taa 1 ya barabarani haizidi 1.5 mil. Halafu chukua walau gari 3 tu za serikali (zilizonunuliwa mwaka huu) convert kwenye idadi ya taa uone maajabu ya hii nchi!

Au chukua nusu ya ile pesa CHAFU waliyochangiwa CCM juzi convert kwenye idadi ya taa! Nadhani utarudi uboreshe thread yako.
 
Una hoja nzuri sana Broh! Na huwa nafuatilia nyuzi zako jithidi kitu kidogo tu kuwa "open -minded" usifocus sana kwenye upande mmoja. Hata shetani ana uzuri wake.

Kuwa open minded ni pamoja na kuhitaji majibu Kwa hoja za Polepole kama kipaumbele kabla ya jambo jingine lolote.

Ninakazia:

Polepole kwa ushahidi huu, CCM acheni kutuambia mtafanya nini eti ndani ya siku 100. Jibuni hoja zake, haziepukiki, hizo ndizo za wananchi!

Kama mmetumwa kumsemea mrejesheeni ujumbe huo.
 
Peleka upumbavu wako huko.... unapakwa mafuta wewe?
Wewe una Rolls-Royce ngapi umepewa kuja kujaza maparagraph humu mwanaume mzima? Nyie watu wengine mngefiaga tu kwenye makende ya baba zenu. Kwa yote yanayoibuliwa mmekosa hata aibu? Bure kabisa, mtu mzima hovyo. Pure nonsense, you are a fool
Thank you Brethren, Be blessed abundantly!..may your eyes be opened and see reality as the continuum of the same thing I pray,
Amen.
 
Moja ya jambo zuri linaloipendezesha miji mingi Tanzania ni uwepo wa barabara nzuri za mitaa zenye taa za barabarani. Hakika Utawala huu kwenye suala hili umejitahudi sana kwa sababu mitaa yetu sasa imekuwa na hadhi nzuri pamoja na muonekano maridhawa.

Biashara ndogondogo zinazofanyika usiku pembezoni mwa barabara zimetanamalaki na kuipa mitaa muonekano na sifa ya ofisi ya kijasiriamali. Jambo hili linaiweka Tanzania na mitaa yake katika muonekano endelevu na siyo ule ulioigizwa kama "Darwin nightmares"miaka kadhaa iliyopita.

Jambo hili siyo tu limeipa mitaa muonekano ila limeifanya mitaa kuwa na sifa bora kabisa kuonesha matumizi ya Kofi za Wananchi wa nchi hii. Kumuelimisha mwanamtaa wa Pangarasi, Darafuma na Mang'ombe juu ya kulipa kodi siyo mzigi mzito tena kwa TRA.

Mitaa inaonekana ni mitaa ya nchi inayoendelea kupiga hatua za makusudi kutoka kwenye lindi la uduni. Usalama wa mitaa nyakati za usiku umeimarika kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka kadhaa kabla ya uwepo wa taa hizo.

Ile kauli mbiu ya vijana kutoka vijijini kuja Dar es Salaam kusgabgaa mataa imeanza kuwa chapwa kwa sababu siku hizi kijijini ni kama Dar tu, na hapa Serikali imejitahidi kupunguza wimbi la uhamaji hususani vijana kutoka vijijini kuja mijini "rural- urban migration".

Katika maandiko yangu kadhaa niliwahi kuandika juu ya sera pendelevu ya mijini " urban- bias policy" inavyoibagaza na kuibananga mitaa ya vijijini ila kwenye hili tunaona jitihada za dhati, za kimkakati na za makusudi kabisa za kupunguza upendeleo huo.
Atusaidie na Mwendokasi Kimara-Gerezani/Kivukoni hali ni sio nzuri kabisa. Mfano leo ni kama mabasi hakuna
 
Vitu petty sana hivyo! Hivi hii nchi ni ya kutegemea mkopo kuweka taa za barabarani kweli?

Nadhani kabla ya kusifia fikiria kwanza ugumu wa jambo husika. Taa 1 ya barabarani haizidi 1.5 mil. Halafu chukua walau gari 3 tu za serikali (zilizonunuliwa mwaka huu) convert kwenye idadi ya taa uone maajabu ya hii nchi!

Au chukua nusu ya ile pesa CHAFU waliyochangiwa CCM juzi convert kwenye idadi ya taa! Nadhani utarudi uboreshe thread yako.
Tatizo naona ni kwamba unajenga hoja ukiwa umefocus upande mwingine na hoja yangu imefocus upande mwingine. Nina hakika ukifocus kwenye polarities zote utaona nilipo. Sikatai kuwa kuna udhaifu,la hasha!..ila naonesha kuna uzuri pia bila kujali ni kiasi gani.
 
Hakuna uzuri hapo mkuu! Huwezi ku jeopardise kodi yangu mwananchi kwenye embezzlement, hanasa na ufisadi serikalini kisha in return ukope pesa ya riba World Bank uje uniwekee TAA za barabarani halafu nikusifu.
Dharau hizo.
 
Well said,
Kuna shida kubwa kwenye matumizi ya fedha za Umma hili sipingi hata kidogo lakini hoja yangu ni kuwa pamoja na yote hayo zipo alama nzuri hata kama ni ndogondogo.

Tofauti inayojitokeza kwenye hoja zetu ipo kwenye mkabala wa kimtazamo "focus approach" tu Mkubwa. Mtu anapochagua mkabala wake wa kimtazamo, mkabala huo hutawala hoja na picha za kiakili za mtu huyo juu ya anachokitazama au kukizungumzia.

Ukitazama chochote kwa mkabala hasi, huwezi kuona jema lolote liwe kubwa au dogo, ila ukitazama kwa mkabala chanya, yapo mazuri utayaona.
Jambo muhimu na ambalo ni mtihani kwetu tulio wengi ni kuwa open- minded na kuona multiple dimensions bila kuathiriwa na focus approach.
 
Huo mkopo ulisimamiwa na Serikali ipi Broh!... Tusibanange na kubagaza kila jitihada, siyo sawa.
By the way hata Mimi siungi mkono kila jambo ila kwenye mazuri nasema.
Kulkua na haja ya mkopo ilihari kampeni za chama znatumia Tzs 86B ?
 
Moja ya jambo zuri linaloipendezesha miji mingi Tanzania ni uwepo wa barabara nzuri za mitaa zenye taa za barabarani. Hakika Utawala huu kwenye suala hili umejitahidi sana kwa sababu mitaa yetu sasa imekuwa na hadhi nzuri pamoja na muonekano maridhawa.

Biashara ndogondogo zinazofanyika usiku pembezoni mwa barabara zimetanamalaki na kuipa mitaa muonekano na sifa ya ofisi za kijasiriamali. Jambo hili linaiweka Tanzania na mitaa yake katika muonekano endelevu "sustainable view"na siyo ule ulioigizwa kama "Darwin nightmares"miaka kadhaa iliyopita.

Jambo hili siyo tu limeipa mitaa muonekano ila limeifanya mitaa kuwa na sifa bora kabisa kuonesha matumizi ya kodi za Wananchi wa nchi hii. Kumuelimisha mwanamtaa wa Pangarasi, Darafuma na Mang'ombe juu ya kulipa kodi siyo mzigi mzito tena kwa TRA.

Mitaa inaonekana ni mitaa ya Nchi inayoendelea kupiga hatua za makusudi kutoka kwenye lindi la uduni. Usalama wa mitaa nyakati za usiku umeimarika kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka kadhaa kabla ya uwepo wa taa hizo.

Ile kauli mbiu ya vijana kutoka vijijini kuja Dar es Salaam kushangaa mataa imeanza kuwa chapwa kwa sababu siku hizi kijijini ni kama Dar tu, na hapa Serikali imejitahidi kupunguza wimbi la uhamaji hususani vijana kutoka vijijini kuja mijini "rural- urban migration".

Katika maandiko yangu kadhaa niliwahi kuandika juu ya sera pendelevu ya mijini " urban- bias policy" inavyoibagaza na kuibananga mitaa ya vijijini ila kwenye hili tunaona jitihada za dhati, za kimkakati na za makusudi kabisa za kupunguza upendeleo huo.
IMG-20250901-WA0068.jpg
IMG-20250903-WA0080.jpg
 
Back
Top Bottom