Utawala wa Rais, Samia Suluhu Hassan unastahili kongole kwa barabara za Mitaa na taa za barabarani

Hayo mambo ya kongole na pongezi ndio uchawa wenyewe. Taa za barabarani ni wajibu wa serikali na ni haki ya wananchi sababu wanalipa Kodi hata kama mradi ni WA mkopo wa IMF.

Kasome notes za mtoto wako za civics jikumbushe rights and responsibilities za citizen.

Hivi ukimpa ujauzito mke wako au mwenza wako unataka tukupongeze? Huo si wajibu wako? Na mkeo au mwenza si haki yake kubeba mimba?
 
Peleka ujumbe, traffic light hazituhusu kama mustakabala mzima wa nchi yaani uchaguzi unatindiganywa!

Nchi inauzwa, wewe unatwambia traffic light? Za nini?
 
Peleka ujumbe, traffic light hazituhusu kama mustakabala mzima wa nchi yaani uchaguzi unatindiganywa!

Nchi inauzwa, wewe unatwambia traffic light? Za nini?
Una hoja nzuri sana Broh! Na huwa nafuatilia nyuzi zako jithidi kitu kidogo tu kuwa "open -minded" usifocus sana kwenye upande mmoja. Hata shetani ana uzuri wake.
 
Basi kama ni wajibu wao tuseme " Wamejitahidi kuwajibika" huoni kama wameonesha sehemu mojawapo ya matumizi ya kodi za Wananchi Mkubwa? Tusibeze kila kitu, wana udhaifu wao sawa, ila tuwe genuine kiasi...
 
Huo mkopo ulisimamiwa na Serikali ipi Broh!... Tusibanange na kubagaza kila jitihada, siyo sawa.
By the way hata Mimi siungi mkono kila jambo ila kwenye mazuri nasema.
Vitu petty sana hivyo! Hivi hii nchi ni ya kutegemea mkopo kuweka taa za barabarani kweli?

Nadhani kabla ya kusifia fikiria kwanza ugumu wa jambo husika. Taa 1 ya barabarani haizidi 1.5 mil. Halafu chukua walau gari 3 tu za serikali (zilizonunuliwa mwaka huu) convert kwenye idadi ya taa uone maajabu ya hii nchi!

Au chukua nusu ya ile pesa CHAFU waliyochangiwa CCM juzi convert kwenye idadi ya taa! Nadhani utarudi uboreshe thread yako.
 
Una hoja nzuri sana Broh! Na huwa nafuatilia nyuzi zako jithidi kitu kidogo tu kuwa "open -minded" usifocus sana kwenye upande mmoja. Hata shetani ana uzuri wake.

Kuwa open minded ni pamoja na kuhitaji majibu Kwa hoja za Polepole kama kipaumbele kabla ya jambo jingine lolote.

Ninakazia:

Polepole kwa ushahidi huu, CCM acheni kutuambia mtafanya nini eti ndani ya siku 100. Jibuni hoja zake, haziepukiki, hizo ndizo za wananchi!

Kama mmetumwa kumsemea mrejesheeni ujumbe huo.
 
Thank you Brethren, Be blessed abundantly!..may your eyes be opened and see reality as the continuum of the same thing I pray,
Amen.
 
Atusaidie na Mwendokasi Kimara-Gerezani/Kivukoni hali ni sio nzuri kabisa. Mfano leo ni kama mabasi hakuna
 
Tatizo naona ni kwamba unajenga hoja ukiwa umefocus upande mwingine na hoja yangu imefocus upande mwingine. Nina hakika ukifocus kwenye polarities zote utaona nilipo. Sikatai kuwa kuna udhaifu,la hasha!..ila naonesha kuna uzuri pia bila kujali ni kiasi gani.
 
Hakuna uzuri hapo mkuu! Huwezi ku jeopardise kodi yangu mwananchi kwenye embezzlement, hanasa na ufisadi serikalini kisha in return ukope pesa ya riba World Bank uje uniwekee TAA za barabarani halafu nikusifu.
Dharau hizo.
 
Well said,
Kuna shida kubwa kwenye matumizi ya fedha za Umma hili sipingi hata kidogo lakini hoja yangu ni kuwa pamoja na yote hayo zipo alama nzuri hata kama ni ndogondogo.

Tofauti inayojitokeza kwenye hoja zetu ipo kwenye mkabala wa kimtazamo "focus approach" tu Mkubwa. Mtu anapochagua mkabala wake wa kimtazamo, mkabala huo hutawala hoja na picha za kiakili za mtu huyo juu ya anachokitazama au kukizungumzia.

Ukitazama chochote kwa mkabala hasi, huwezi kuona jema lolote liwe kubwa au dogo, ila ukitazama kwa mkabala chanya, yapo mazuri utayaona.
Jambo muhimu na ambalo ni mtihani kwetu tulio wengi ni kuwa open- minded na kuona multiple dimensions bila kuathiriwa na focus approach.
 
Huo mkopo ulisimamiwa na Serikali ipi Broh!... Tusibanange na kubagaza kila jitihada, siyo sawa.
By the way hata Mimi siungi mkono kila jambo ila kwenye mazuri nasema.
Kulkua na haja ya mkopo ilihari kampeni za chama znatumia Tzs 86B ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…