Utenguzi: Maharage Chande wa Posta, Ulanga wa TTCL na Justina Mashiba wa UCSAF watumbuliwa

Utenguzi: Maharage Chande wa Posta, Ulanga wa TTCL na Justina Mashiba wa UCSAF watumbuliwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu MkuuKiongozi Balozi Dk.t Moses Kusiluka, viongozi waliotenguliwa ni kama ifuatavyo:-

1. Bi Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolph Ulanga, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

2. Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Bw. Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania.

3. Prof. John Nkoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Bi. Justina Tumaini Mashiba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Sharifa B. Nyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

View attachment 3050160
Pia soma; UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL
Only baba yake Magabe ndo imeniuma, I personally know him.
 
Walionywa mapema na wenye akili hawakusikia!

IMG-20240723-WA0205.jpg
 
mtendaji mkuu alikuwa ni kiazi, period
Ila chakujiuliza kwanini wote hao na kwapamoja hapo bado wapo ambao hawakuguswa,kuna nini,walikuwa na bond nzito sanaa au kukataa matokeo ya uamuzi uliofanywa.Vinginevyo nitafananisha na siasa za taifa moja kiuubwa duniani,Baada ya babu kutema bungo wapo viongozi washirika wanufaika wa babu walituma salamu za pongezi,isije kuwa ni kuponzwa na copy&paste?
 
Back
Top Bottom