Quite literally, the term "philosophy" means, "
love of wisdom." Kupenda hekima, walioanzisha hill neno walikuwa watu waliopenda kujiweka kama watafutaji wa maarifa.
Walijitofautisha na wajuaji wa kina sage na gurus na rabbis. Tena ungejua hii tabia ya 'ujuaji' kujifanya unajua kila kitu. Au umeshikilia maarifa fulani kwamba ndio kila kitu, ndio tabia mahsusi kabisa iliyopelekea kumkataa nabiy Issa kati ya 'wasomi' waliokuwa wengi na kukubalika na watu wa kawaida.
Kuna maandiko katika biblia yanayoweka kheri kwa wahitaji wa maarifa;
Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Na zipo aya kadhaa zinazosifia tabia ya 'ufilosofi': Samahani bandugu nitakopi aya nzima maana sina hakika nikiwapa reference kama kila mmoja ataenda kweli kusoma:
Mithali 8
1 Je! Hekima halii?
Ufahamu hatoi sauti yake?
2Juu ya mahali palipoinuka karibu na njia,
Penye njia panda, ndipo asimamapo.
3Karibu na malango, mahali pa kuingia mjini,
Mahali pa kuyaingilia malango anapiga kelele.
4Enyi watu, nawaita ninyi;
Na sauti yangu ni kwa wanadamu.
5Enyi wajinga, fahamuni werevu,
Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu.
6 Sikieni, maana nitasema yaliyo mazuri,
Na kufumbua midomo yangu kutakuwa maadili.
7 Maana kinywa changu kitasema kweli,
Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu.
8Maneno yote ya kinywa changu yana haki;
Hapana hata neno lililopotoka au la ukaidi.
9Yote humwelea yule afahamuye,
Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa.
10Pokea mafundisho yangu, wala si fedha,
Na maarifa kuliko dhahabu safi.
11 Maana hekima ni bora kuliko marijani;
Wala vyote vinavyotamanika havilingani nayo.
12Mimi, hekima, nimefanya werevu kuwa kao langu;
Natafuta maarifa na busara. [Watafuta maarifa huitwa filosophers]
13 Kumcha BWANA ni kuchukia uovu;
Kiburi na majivuno, na njia mbovu,
Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
14 Shauri ni langu, na maarifa yaliyo sahihi;
Mimi ni ufahamu, mimi nina nguvu. [Amenikumbusha hitimisho letu na
draga]
15 Kwa msaada wangu wafalme humiliki,
Na wakuu wanahukumu haki.
16Kwa msaada wangu wakuu hutawala,
Na waungwana, naam, waamuzi wote wa dunia.
17 Nawapenda wale wanipendao,
Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
18 Utajiri na heshima ziko kwangu,
Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
19 Matunda yangu hupita dhahabu, naam, dhahabu safi,
Na faida yangu hupita fedha iliyo teule.
20Natembea katika njia ya haki,
Katikati ya mapito ya hukumu.
21Niwarithishe mali wale wanipendao,
Tena nipate kuzijaza hazina zao.
Sehemu ya Busara katika Uumbaji [READ THIS PART CAREFULLY, imebeba madini ya uzi huu. Kama yeyote utang'amua sehemu nilipopingana na maandiko tafadhari nirekebishe]
22 BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yake,
Kabla ya matendo yake ya kale.
23 Nalitukuka tokea milele, tangu awali,
Kabla haijawako dunia.
24Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa,
Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.
25 Kabla milima haijawekwa imara,
Kabla ya vilima nalizaliwa.
26Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde
Wala chanzo cha mavumbi ya dunia;
27Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;
Alipopiga duara katika uso wa bahari;
28Alipofanya imara mawingu yaliyo juu;
Chemchemi za bahari zilipopata nguvu;
29 Alipoipa bahari mpaka wake,
Kwamba maji yake yasiasi amri yake;
Alipoiagiza misingi ya nchi;
30 Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi; [
Umeona!!]
Nikawa furaha yake kila siku;
Nikifurahi daima mbele zake;
31 Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu;
Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.
32 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa;
Maana heri hao wazishikao amri zangu.
33Sikieni mafundisho, mpate hekima,
Wala msiikatae.
34Ana heri mtu yule anisikilizaye,
Akisubiri sikuzote malangoni pangu,
Akmngoja penye vizingiti vya milango yangu.
35 Maana yeye anionaye mimi aona uzima,
Nayafe aaftapata kibali kwa BWANA. [Njia, kweli, uzima ]
36 Bali anikosaye hujidhuru nafsi yake mwenyewe,
Na wao wanichukiao hupenda mauti. [Malipo ya ukaidi, uongo ni mauti]