Mheshimiwa January Yusuf Makamba, hongera sana kwa kuteuliwa kuwa waziri,wizara ya Nishati.
Wizara ya Nishati Ina changamoto nyingi sana ambazo zinatugusa sisi wanyonge.
Shirika la umeme (TANESCO) ni kero.
a).Tunaomba umalize changamoto ya nguzo za umeme na mita kwa wateja wa REA,
b). kanda ya Chanika-wateja wamefanyiwa survey zaidi ya miezi sita, lakini hawajapata huduma kwa ukosefu wa nguzo, nyaya na mita.
c).Lakini ukienda vituo vingine vya Tanesco Kama Buza,unakuta nguzo zimelundikana .
Ushauri:
1). Mheshimiwa Waziri,Shirika ni moja kwa hiyo ni busara wakachangia rasimali
2). Mheshimiwa Waziri kuanzia July 2021 serikali imeanza kukusanywa kodi ya majengo kupitia Luku,ni vema TANESCO wakaharakisha kuweka umeme,ili kuongeza wigo wa walipa Kodi.
3). TANESCO,wawe wanapeleka, Nguzo nyingi kwenye miradi mpya (badala ya kupeleka maeneo yenye umeme (kusubiri matukio ya dharura).
4). Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO aongeze rasilimali Kituo Cha TANESCO Chanika chenye wateja wengi Sana katika jiji la Ilala( mafundi,vitendea kazi).
4). Mheshimiwa Waziri,kuna fomu nyingi za maombi ya umeme , kwenye vituo mbalimbali vya TANESCO,lakini hazijafanyiwa kazi,
5).kwa mfano Kuna wateja walichukua fomu za maombi ya umeme kisarawe May 2020 ,lakini hawakupata huduma,mpaka mwezi May 2021 zile fomu zilipohamishiwa kituo kipya Cha Chanika, lakini mpaka hivi leo bado hawajapata huduma za umeme.(ingia kwenye Data base ya TANESCO,angalia pending applications,utapata majibu).
6). Mheshimiwa Waziri,watendaji wa TANESCO ,wajitafakari,wana majibu yanayo kera na hawana customer care,wana haribu taswira(image) ya taasisi mbele ya wateja wao