Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Mungu yu mwema aisee ,Mama piga kazi ,uliona wapi tangia uhuru zaidi ya nusu ya baraza la mawaziri ni kabila moja ,tena mama naona kaamua kuwaacha tu wengine waendelee ,angesafisha wote ,hii nchi ni yetu wote ,Asante saaana Rais wetu mpendwa
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji91]
 
Katika vitu Sukuma gang walikosea ni ishu ya Lodilofa wakadhani wako stronger enough kusimama wenyewe….

Soon Membe anarudi mjini ndipo watajua hawajui…

Then nimenusa nusa mahali ule utatu mtakatifu umeinuka tena… wameamua kusameheana!!
Aisee . . Sukuma Gang chali
 
Mheshimiwa January Yusuf Makamba, hongera sana kwa kuteuliwa kuwa waziri,wizara ya Nishati.
Wizara ya Nishati Ina changamoto nyingi sana ambazo zinatugusa sisi wanyonge.
Shirika la umeme (TANESCO) ni kero.
a).Tunaomba umalize changamoto ya nguzo za umeme na mita kwa wateja wa REA,
b). kanda ya Chanika-wateja wamefanyiwa survey zaidi ya miezi sita, lakini hawajapata huduma kwa ukosefu wa nguzo, nyaya na mita.
c).Lakini ukienda vituo vingine vya Tanesco Kama Buza,unakuta nguzo zimelundikana .

Ushauri:
1). Mheshimiwa Waziri,Shirika ni moja kwa hiyo ni busara wakachangia rasimali
2). Mheshimiwa Waziri kuanzia July 2021 serikali imeanza kukusanywa kodi ya majengo kupitia Luku,ni vema TANESCO wakaharakisha kuweka umeme,ili kuongeza wigo wa walipa Kodi.
3). TANESCO,wawe wanapeleka, Nguzo nyingi kwenye miradi mpya (badala ya kupeleka maeneo yenye umeme (kusubiri matukio ya dharura).
4). Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO aongeze rasilimali Kituo Cha TANESCO Chanika chenye wateja wengi Sana katika jiji la Ilala( mafundi,vitendea kazi).
4). Mheshimiwa Waziri,kuna fomu nyingi za maombi ya umeme , kwenye vituo mbalimbali vya TANESCO,lakini hazijafanyiwa kazi,
5).kwa mfano Kuna wateja walichukua fomu za maombi ya umeme kisarawe May 2020 ,lakini hawakupata huduma,mpaka mwezi May 2021 zile fomu zilipohamishiwa kituo kipya Cha Chanika, lakini mpaka hivi leo bado hawajapata huduma za umeme.(ingia kwenye Data base ya TANESCO,angalia pending applications,utapata majibu).
6). Mheshimiwa Waziri,watendaji wa TANESCO ,wajitafakari,wana majibu yanayo kera na hawana customer care,wana haribu taswira(image) ya taasisi mbele ya wateja wao
 
Dr tax ni reserve ya mulamula trust me

Mula mula akizingua tu TaX huyo .

Huko wizara ya ulinzi Wala hakuna kash Kash yeye atadili na masoja tu .

Wala hamtamsikiasikia kwana kwadikwa mlikua mnamsikia daily au mwinyi.

Mula mula watch out TaX is there to take in
 
Rais Samia Suluhu kafanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali kama ifuatavyo
  1. Rais Samia Suluhu amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, anachukua nafasi ya marehemu Elias Kwandikwa
  2. Dkt. Ashatu Kijaji ameteuliwa kuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kuchukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambae uteuzi wake umetenguliwa
  3. January Makamba anachukua nafasi ya Merdard Kalemani wizara ya Nishati
  4. Makame Mbarawa anachukua nafasi ya Chamuriho wizara ya ujenzi na uchukuzi
  5. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali


Makamba nikati ya vijana makini kidogo ccm imebaki nao,achana na wakina Mwigulu
 
Back
Top Bottom