Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Uteuzi: January Makamba ateuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Ndugulile, Kalemani, Chamuriho na AG Kilangi watenguliwa, Feleshi ateuliwa

Ni Uteuzi wa Kimkakati zaidi na bahati nzuri wote walioteuliwa ni Watu makini na wachapakazi pia kwani hata Rekodi zao za Kiutendaji hapo kabla zinajieleza na Kuridhisha.

Kurejeshwa kwa Mbarawa nimefurahi na pia kuihamishia Idara ya Maelezo katika Wizara ya Mtaalam Makamba ni Jambo jema kabisa.

Kuondolewa kwa Kalemani ni Uthibitisho rasmi kuwa sasa Mabaki ya Hayati Rais Dkt. Magufuli na yaliyokuwa hayagusu yameshaondolewa na hata Kuvunjwa nguvu ya Kiushawishi ndani ya CCM na Serikali.

Uwaziri wa Dkt. Tax kwa hiyo Wizara Muhimu Kiulinzi na Kiusalama nchini ni Heshima kwa Wanawake na Imani Kubwa Kwao ila kama sijakosea nadhani ndiyo mara ya Kwanza mwa Mwanamke kuteuliwa hapo.

Wote waliotenguliwa walikuwa dhaifu.

Elezea madhaifu yao ,
 
Kwa jicho la tatu unahisi huyu anaweza kumkontrol msukuma au ile "ndio mkuu"[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
Huyu Tax haendi kuwapangia hao wanajeshi la kufanya..huyo anaenda kulink maslahi yao na Serikali,huku pia Wizara iki-solve ishu ndogondogo ambazo zinahusisha jeshi na Wizara nyingine..Ni mwakilishi tu.
 
Rais Samia Suluhu kafanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali kama ifuatavyo

  1. Rais Samia Suluhu amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, anachukua nafasi ya marehemu Elias Kwandikwa
  2. Dkt. Ashatu Kijaji ameteuliwa kuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kuchukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambae uteuzi wake umetenguliwa
  3. January Makamba anachukua nafasi ya Merdard Kalemani wizara ya Nishati
  4. Makame Mbarawa anachukua nafasi ya Chamuriho wizara ya ujenzi na uchukuzi
  5. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali


View attachment 1935268
View attachment 1935270
Yale yale kusafisha choo kwa mkojo.
 
Kunatatizo kubwa Sana Sana kwa taasis, ama madam hajaenea vzr au anaongozwa na watu ambao wanamwendesha kimawazo au anasukumwa na jenda issues,

Sasa unamtoa kwel kalamani et unatengua uteuzi wake, au ndugulile is she seriously?? Hii nchi imekosa kwel watu wakumwambia madam hili hapana unakosea;, kwel wazir wa ulinz unamweka tax??
Kalemani hakuwa anajua anafanya nini. Ni ubabe tu usio na sababu
 
Hatuhitaji kumwaga damu ili kuwapa raia kile wakitakacho. Maccm hayana mapenzi na Tanzania na Watanzania ndiyo sababu yanagomea haya mabadiliko chanya ambayo yataleta mabadiliko makubwa sana nchini.

Miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi lakini bado tuna katiba ya chama kimoja!

Na hali hii ndiyo inayochangia sana nchi yetu kukosa maendeleo ya kweli kwa miaka 60 sasa tangu tupate uhuru.

Ugumu upo kwenye uoga wa kuingia front mkuu, hii waifahamu uzuri.

Siro akitamka tu akavunja miguu watu wanasepa.

Lakini hata huko Ulaya na Marekani watu wanaingia hivyohivyo ila tawala hujiandaa.

Kule Capitol Hill wamejiandaa kwa kupigilia mabango kuzuia entry kwa waandamaji.
 
Wizara zote nyeti wamepewa wanawake, afya ,ulinzi, tamisemi, elimu,[emoji18][emoji18]mwigulu namshauri aachie wizara ya fedha mapema[emoji33][emoji33]
 
Huyo kaharibu kwenye madini siku nyingi tu alikuwa anabebwa sababu ya Jiwe.

Hawa wote walitemwa wamaharibu sana wizara zao walikuwa wanatembelea nyota ya jiwe lakini hamna kitu.

Wapo na wengine soon watapata haki yao.

Na mama yetu Rais. Alifikaje Hapo. Huwa mnakuwa wapumbavu mpaka Mnaacha kufikiria. Siasa Ni mipango. Sio vyote vitakuwa kwa faida yako. Usipende sana mambo mapya bali penda kazi na malengo.


Mana Samia Ni Rais wa JMT. Alipata kuwa Mgombea mwenza wa JPM. Na Sasa ndo Mkuu wetu. So Team ya Kikwete ni ya CCM. Team ya JPM ni CCM na Team ya JPM ndo imetoa Mama yetu. Ana malengo na maono yake. Tumwache afanye kazi. Hapa mitandaoni ni mahali Pa domokaya
 
Mbona mama timu magufuli. Mkuuu JPM Ni marehemu. Rais wetu Ni mama Samia. Kadiri mnavyopenda kuongea kuhusu JPM, Ndivyo mnavyozidi kuonyesha ukubwa Wake. Je. Timu ya kikwete na mkapa na mwinyi Ni ipi? Samia na mwinyi kama ndo kijiti kupeana wamepewa na JPM. Jifunzeni kumove on. Muwe consistency hata kwa ujinga wenu.

Nakumbuka JPM alivyomtumbua mbunge wa Kigamboni, alishambuliwa na hata kwenye Kugombea ubunge kigamboni, watu mliingia moyoni mwa JPM. Mkasema mwanaye Makonda lazima apite! Mkasahau kuwa Makonda cheo chake cha ukuu wa Wilaya alipewa na JMK. Na Hata bunge la katiba aliingia na kina mama Samia. Rais wetu mpendwa wa Sasa. Huwa mnamjua sana JPM hata uko kaburini bado mnadownload mind yake.

Hawa wanasiasa tofauti Yao ndogo sana. Vijana fanyeni kazi. Nani Kawa waziri wakati wewe sio Katibu wa wizara hizo haikusaidii lolote. Huwa mnajifariji sana kwa matatizo ya wengine. Ni Alama ya kufell na kuchanganyikiwa. Jaribuni kuishi maisha yenu. Solange uwaziri Ni kuteuliwa. Kila kitu Ni possible. Love and live your life.
Mkuu hii jF imejaa watu wenye mawazo ya kibodaboda hadi kero.

Huwa najaribu kifikiria ni nini maana ya mtu kuweka maswala ya teams katika uongozi ila huwa sipati majibu kabisa.Huyo makonda aliwekeza na Jk ila utasikia alikuwa ni mtoto wa JPM kwakua tu ni msukuma, wanahubiri ukabila ilihali wao ndo wameutanguliza mbele.
 
Back
Top Bottom