UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Maharage yakichemka lazima yaruke ruke tu mara dstv, mara tanesco, mara ttcl, mara posta masta, mara atapangiwa kazi nyingine. Mara kimeo
 
Kuna mamba humu alisaga kunguni.
Msimlaumu samia mengine hayajui. Muwe mnamuambia
 
Akaboreshe huduma za kutuma parcel na mizigo mikubwa. Fuso,Canter na Scania 113 za Posta zitoke wanunue Gari za kisasa za kusafirisha parcel mikoani.

Na customer care waboreshe kwenye kupokea na kutuma parcel, kwa majiji makubwa waweke gari ndogo na pikipiki za kufanya delivery kama wenzao DHL
Hivi Maharage alsomea kitu gani.
Kwenye TV yumo
Kwenye umeme yumo
Kwenye simu yumo
Na Sasa kwenye logistics ndio kabisa.
 
Kwa ajili ya Misa nyingine sio? By the time mnamaliza mkitoka nje unapewa taarifa mandondo atapangiwa kazi nyingine.
yes,
paroko atashangaa sana 🤣
Nahis paroko atamtia moyo atamwambia haya ni majaribu usiogope,
ñjoo uungame kwanza kuna kitu hovyo umefanya pale Tanesco hujaungama, embu ñjoo ungame!!

sasa sijui mandondo atakubali kuungana au atamsingizia mwezi wa kwanza?😜
 
Liwapo kwenye maji boya huwa linaeleaelea likienda huku na kule kutegemeana na mawimbi na upepo, lakini lenyewe huwa halina mwelekeo wala maamuzi.

Ukiona linazama ujue limevutwa kuzamishwa, likiibuka ujue limeachiwa, likianza kwenda kutoka lilipo ujue linapelekwa, likirudi ujue linarudishwa and the story goes on just like that.
Nimekuelewa sana.
 
Aisee..
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Tuna uongozi wa hovyo sana kuwahi kutokea tangu uhuru
 
Back
Top Bottom