UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

Thubutu..posho serikalini tamu kwanafasi yake ya ukurugenzi bado hawezi kuukataa halafu private si mpaka aombe kwani anapata tu hivihivi...ila jamaa sijui ana u special gani mpaka apete namna hii
 
Kama humjuwi Maharage Chande Bora ukae kimya tu.

Kwa uwelewa wangu mdogo Maharage Chande ni namba nyingine kama ni kwa Jina la Jamuhuri ama la Maharage yote kwetu ni Siri ila majibu tuta yapata baada ya miaka kadhaa.

Kwahali ilivyo na kile Kina endelea mwenye macho aambiwi Tazama. Ila nawakumbusha nawasalim kwa Jina la Jamuhuri ya Muungano na wote itikieni kazi iyendelee....🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙏
 
Ndio umeandika nini sasa hapa au huyo maharage wako amefanya nini nchi hii Hadi useme ni namba nyingine?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)...
Maharage alikuwa anajitapa kwa kuongea na rais moja kwa moja hata Makamba alimuogopa, na hapo posta wanamtumbua na nasikia account zake zote wameshashikilia soon hata hizo suti atavaa kobaz
 
Maharage chande na yule dogo wa Bandari ni watu waliowekwa kwenye u CEO kwa bahati mbaya.

Hawana sifa utendaji wao ni wakujiumauma. Hata posta alikoenda Maharage hana atakalofanya.

Hafai.
 
Hiyo jeuri wanayo akina Maganga wa CWT pekee!

Hao wenye CV zao waoga wa maisha,ukidindia mamlaka ya uteuzi hata sector binafsi bongo wanaogopa kukuajiri watafuatwafuatwa!
 
Wanaotaka ajira wamejaa we nenda tu private company kama utapata.
Pengo lako linazibika
 
Kwa wasio mfahamu huyu Maharage kabla ya kuja TANESCO alikuwa kiongozi wa Multichoice (ile kampuni inayomiliki DSTV) yaani kwa kifupi alikuwa boss wa wafunga madish wote wa DSTV na wafanyakazi wengine.
Kwahiyo alitoka kuwa mfunga madishi mpaka kuja kukabidhiwa shirika nyeti kama TANESCO? Haishangazi kwanini tumetumbukia kwa mgao wa umeme tena mkali
 
KISA CHA KUFIKIRIKA
Kwenye CV unaweka kuwa juzi nilikuwa mkurugenzi wa shirika A, jana nikahamishiwa shirika B leo nikahamishiwa shirika C kesho ikitokea umetemwa aloo...

Kila HR atakuwa anajiuliza inamaana wewe ulikuwa unajaribu kubebwa hubebeki sasa nikusaidiaje, kama vipi acha CV yako tutakupigia, ukiona kimya usipige simu sawa eeh.

Mwisho.
 
Ukiteuliwa tulia.
Kazi ya mamlaka ya uteuzi ni kuteua kama ipendavyo. Kazi ya mteuliwa ni kuteulika.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)...
Tena alitakiwa awe kwaya masta kabisa. Anatuzimia umeme sisi? Anadharau mpaka mamlaka. Tena anasema anaacha mgao na kuanzisha ratiba. Ratiba na mgao tofauti yake nini?
 
hivi Samia mimi hunioni au kunifikria tu?
Samia kuwa na huruma basi nimekupigania sana.
 
Back
Top Bottom