UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

Maharage Chande[emoji38][emoji846]

Kutoka kuwa ED wa TANESCO----->ED wa TTCL(Siku 3) mpaka Postamasta..[/color][/b]

Tusishangae kesho akatenguliwa na ka ujumbe ka "Atapangiwa kazi nyingine".

Kwenye CV yake anaandikaje? Ha haa
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Sasa inaingia Team Mpya ya DB na Kampeni za 2025. Hili taifa litaliwa hadi liliwe
 
Akaboreshe huduma za kutuma parcel na mizigo mikubwa. Fuso,Canter na Scania 113 za Posta zitoke wanunue Gari za kisasa za kusafirisha parcel mikoani.

Na customer care waboreshe kwenye kupokea na kutuma parcel, kwa majiji makubwa waweke gari ndogo na pikipiki za kufanya delivery kama wenzao DHL
 
Kwani hizo nafasi hawezi kupewa mtu asiyekuwa kwenye system?Tanzania hii ya watu 60+mill hayupo msomi anayemzidi au hata wa kufanana nae akapewa hizo nafasi?

Inashangaza sana,anatolewa hapa nawekwa kule anatolewa kule anatupwa pale alimradi awepo ktk circle.kwani hizi teuzi anayezifanya hashauriwi au ndiyo hashauriki?
Inakera Sana hii kitu
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
samia kazi imemshinda anajikongoja
 
Back
Top Bottom