UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

Anaye teuwa anasubiri mwenyewe atenguliwe.

Hii siyo kawaida hata kidogo.

Hawa wanaoteuliwa na kutenguliwa kila siku wanafanya kazi lini?

Teuzi hizi ni za majaribio au kubahatisha, hazina utaratibu wowote unaofuatwa kujua ni wapi wanapostahili kuwepo?

Hii ni ishara muhimu sana kwamba huyu mama hawezi kitu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)...
🤣🤣🤣🤣🤣 Yaani Nape hajamaliza kumkaribisha Jamaa kaliwa kichwa tena,si Bora aache kazi arudie dstv alikokuwa?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

"Serikali kwasasa inafanya mapitio ya sheria ya utumishi wa umma Sura no. 298, sera ya Menejimenti ya ajira ya umma toleo la pili la 2008, kanuni ya utumishi wa umma ya 2022 na miongozo yake inayohusu masuala ya ajira"
~hayo yalisemwa Septemba 04, 2023 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete
 
Watu wanasema ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.
Maneno hayo yamedhihirishwa na Serikali ya Awamu ya sita na kudhihirisha ule usemi wa kuruka ruka kwa maharage ndo Kuiva kwake!.

Baada ya Maharage chande kuliwa kichwa cha Mkurugenzi mtendaji TANESCO na kupewa UKURUGENZI MKUU TTCL leo Mchana ameliwa Tena kichwa na kupelekewa kuwa Postamasta mkuu na kunyang'anywa Medani ya UKURUGENZI MKUU..

HONGERA ENG.PETER ULANGA...
POLEE SANA MAHARAGE NDO MAISHA YALIVYO..
View attachment 2762253
Nchi INA figisu kishenzi
 
Liwapo kwenye maji boya huwa linaeleaelea likienda huku na kule kutegemeana na mawimbi na upepo, lakini lenyewe huwa halina mwelekeo wala maamuzi.

Ukiona linazama ujue limevutwa kuzamishwa, likiibuka ujue limeachiwa, likianza kwenda kutoka lilipo ujue linapelekwa, likirudi ujue linarudishwa and the story goes on just like that.
Kwa hio unasema kwamba Maharage ni ........
 
Huyu maharage atakuwa kampigia Mheshimiwa kujitetea siyo bure.

Sasa posta masta nani ataposti barua tena?

Au kazi ya kupokea barua za kuomba kazi, nazo ipo nini ile , mmmh karongwa
 
Aliyekuwa anamtumia kupiga porojo hapo TANESCO ana "magodfather" anapeta tu.

Mr Beans akija kushtuka kateuliwa u-gateman wa halmashauri ya Namtumbo DC.,😁😁.
 
Back
Top Bottom