UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

🤣 Zuhura Yunusi mwambie mama asifanye ukatili huu wa kisaikolojia.

Yaani ndio tumetoka Kanisa kwenye misa ya shukrani kwa uteuzi wa TTCL, kufika nje kuwasha tu simu tunakutana na pdf la Zuhura Yunusi 🤣 tumeng'atuliwa na kuteuliwa tena kwenye taasisi nyingine.

Tutawasiliana na Baba paroko tena kesho
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. John Ulanga kuwa Balozi. Bw. Ulanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Postamasta, Shirika la Posta Tanzania. Kabla ya uteuzi huu Bw. Chande aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Bw. Chande anachukua nafasi ya Bw. Macrice Daniel Mbodo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Aidha, Mhandisi Peter Ulanga ataendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Kasheshe aisee
 
Back
Top Bottom