UTEUZI: Maharage Chande aondolewa TTCL, ateuliwa kuwa Postamasta, Ulanga arudishwa TTCL

Watu na bahati zao,
 
Matunda ya Expo2020 Dubai



Tanzania yapata neema ya Trilioni 17 Dubai EXPO​

https://mtanzania.co.tz/tanzania-yapata-neema-ya-trilioni-17-dubai-expo/#
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika leo Dubai, UAE

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji lililofanyika leo Dubai, UAE.
Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya Dubai EXPO 2020 umezaa matunda baada ya kushuhudiwa utiaji saini wa mikataba 36 ya makubaliano katika sekta mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Sh trilioni 17.
Sekta zitakazonufaika ni pamoja na nishati, kilimo, utalii, miundombinu, usafiri na teknolojia.
Utiaji saini huo ambao umeshuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan umefanyika wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji ambalo pia limeshirikisha viongozi wa taasisi za Serikali, binafsi na wafanyabiashara mbalimbali.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwenye maonesho ya Dubai EXPO 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Godius Kahyarara, amesema mikataba hiyo 36 ina thamani ya Dola bilioni 7.43 ambazo ni sawa na Sh trilioni 17.35.
Miongoni mwa mikataba hiyo umo wa uwekezaji katika umeme, uwekezaji katika Mamlaka ya Bandari (TPA) unaolenga kuondoa msongamano bandarini, kulipa uwezo Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC) katika biashara ya mafuta, kuliongezea uwezo TTCL katika sekta ya ICT ambao pia utahusisha ujenzi wa kiwanda cha simu za mkononi za kisasa.
Aidha katika eneo la kilimo imesainiwa mikataba minne ikiwemo inayolenga kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuongeza teknolojia na upatikanaji wa nyenzo za kilimo ambapo mradi wa chini una thamani ya Dola 500, kufungua soko la bidhaa za Tanzania katika nchi za mashariki ya kati na kufungua fursa za wakulima katika soko la dunia.

Mkataba mwingine ni ule uliosainiwa baina ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar ambao unalenga kukuza utalii wenye thamani ya Dola milioni 100.
Vilevile umo mkataba wa kukuza biashara kati ya Tanzania na Supermarkets za Emirates ambapo wameanza na kahawa na korosho pamoja na ujenzi wa eneo la viwanda Kwala mkoani Pwani.
Mikataba mingine ambayo Rais Samia ameshuhudia utiaji saini wake ni ile inayolenga kufungua masoko ya bidhaa za mboga, matunda na maua (horticulture) kati ya Tanzania na India, kuiongezea uwezo, mtaji na teknolojia Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na uzalishaji wa mbolea kwa kutumia manyoya ya kuku, ngombe na mabaki ya mifugo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Ashatu Kijaji, akizungumza wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwenye maonesho ya Dubai EXPO 2020.
Akihutubia katika kongamano hilo Rais Samia amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na kuwakaribisha wawekezaji zaidi kuja kuwekeza nchini.
“Leo tumeshuhudia utiaji saini wa mikataba 36 ni matumaini yetu itaenda kutekelezwa kwa vitendo, na kama kuna changamoto yoyote kutoka Serikali yangu tafadhali nijulisheni haraka,” amesema Rais Samia.
Tanzania ni kati ya nchi 192 zinazoshiriki maonesho hayo yaliyoanza Oktoba Mosi 2021 yakitarajiwa kumalizika Machi 31 ambapo ushiriki wa Tanzania unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).
Sehemu ya Watanzania waishio Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wakimsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza nao.
EXPO ni maonesho ya dunia yanyofanyika kila baada ya miaka mitano yakisimamiwa na Shirika la Kimataifa lijulikanalo kama Bureau of International Exhabition (BIE) lenye nchi wanachama 195 huku Tanzania ikiwa mwanachama tangu mwaka 1973.
 
Ni upuuzi tu nchi nzima. Kama manyani vile juu ya miti
Huyu mama anahangaika sana kama umeona mtu hafai SI umtoe mazima tu!!
Vetting zero hamna kitu hapa.
Kibaya zaidi mazee yaliochoka akili bado yanawekwa
Duh mbona kamficha sana Chande

Bw. Ulanga nae naona nyota imeng'aa. Katoka Trade Mark Africa kaenda TPSF, hajakaa sana leo kawa balozi. Anaweza kuwa msemaji wa serikali ajaye. Kila la heri kwake.
Ni kuvurugana akili tu, wamemvuruga hadi mleta uzi kaja kuufungulia huku International Forum
 
Mbona yule Waziri Kindamba katoka hapo Ttcl kaenda kuwa Rc Tanga,nae uyo Kindamba ni mtaalamu wa It....Rais wetu katiba inamlinda muache afanye yake
 
Kumuondoa Ulanga TTCL lilikuwa ni kosa la kiufundi...

Sijui kwa nini Samia anaingizwa sana machaka na washauri wake...
Nilishangaa pia, nadhani amepata feedback, Ulanga ni Experienced & Handson engineer, falsafa yake ya uongozi imejikita kwenye uhalisia sio nadharia tu, apewe muda. Kwa muda mfupi aliokuwepo TTCL na mabadiliko aliyoyaleta vinatosha kumtetea. Napenda approach yake ya kukomaa kuifanya TTCL kuongoza kwenye upande wa fixed data, dunia ndipo iliko.
 
Anafanya nini watu wanalia na fiber tu kila siku progress haionekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…