DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Kashushwa mzee Nafasi ya Katibu uenezi ni Ya kitaifaKashushwa cheo au analetwa serikalini mdogo mdogo.?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kashushwa mzee Nafasi ya Katibu uenezi ni Ya kitaifaKashushwa cheo au analetwa serikalini mdogo mdogo.?
Teh teh teh.😃😃😃..mkakati upi huo tena?...kwani bila Makonda CCM haiwezi kushinda uko Arusha ,?In a sense and technically kashushwa. Ukila na kipofu usimguse mkono. Kwa kumtajataja JPM alikuwa anagusa hadi masikio. Ila upande mwingine kupelekwa Arusha ni mkakati kuelekea 2025. Msije mkamsikia anakuwa Katibu Mkuu CCM...
Kuna wakati kiongozi yapaswa vitendo vyako viongee sana kama mbinu anazotumia Nchimbi, chama kilijaa wapiga pambio bila mipango ya kuzikabili chaguzi.Mm nilijua kaletwa nchimbi basi atafagia mitaka taka yooote.katibu hana kelele ni mtu wa mipango zaidi.niliota ndoto flan naikumbuka mpaka kesho.inakribia kutimia
Makonda ilitakiwa ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya halafu apelekwe Mkoa aliopo Chongolo...TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.
iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.
vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.
ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.
xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.
Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
View attachment 2949540
View attachment 2949541
Hataki kukua kiuongozi kwani umaarufu upo Kwa mtawala pekee tofauti na hapo ni kujichimbia kaburi.Makonda alitaka kujiinua kuliko mkuu wake.
Yeyote asingekubali.
Kumekucha na nini? Makonda hataiweza na haiwezi Arusha. Akija anatakiwa awe mpoleeeee. Aliwaweza nyie wala 🍟 wa Dar ila huku haiwezi ng'ooooooo. Kashindwa Ukatibu uenezi, ataweza ukuu wa mkoa. PtuuuuuuuuArusha kumekuchaaaa 😆
Kilichomuondosha ni kusifia Mjomba Magu mara kwa mara na huku akisisitiza kuwa Dr Samia yupo same page na Mjomba Magu.Makonda wenye chama wameona anawadhalilisha, wameona wampangie kazi nyingine ili aisiendelee kuaibisha chama.
Ruto mbona amefanya uteuzi na utenguzi juzi tu hapa au yule ni Ruto Rais wa Comoro?HAya ndio anayo yaweza, hakuna kingine anacho weza.
Mwaka wa tatu still anaunda Serikali, Ruto ana mwaka mmoja kazini ila alisha achana na teua, tengua, hamisha, mwaka wa tatu Raisi anaunda Serikali.
imagine pesa zinazopotea kwa hii hamisha, teua, tengua, rudisha......ndani ya miaka mitano umeshateua na kutengua mara ngapi?
Nini kimeongezeka? Naona kama ni fashion tu.
Tunadeal na performance based kweli au kuna lingine?
Yule alikiwa mwajiliwa wa seeikalini tangu zamani,,so usipompa kazo anaendelea kula mshahara bureWatu wanabahati sana Dr Mhede amefeli TRA akafeli DART tena kapewa kazi?
Wala hawajaliimagine pesa zinazopotea kwa hii hamisha, teua, tengua, rudisha......
Never outshine your MasterAmemteua Lucas Mwashambwa kuwa chawa kiongozi jamiiforums.
Anyway tukiacha utani, Bashite kuna namna amegusa pasipogusika, na soon anaweza akarudi bench aendelee kuwa best loser!!
Na kwa siasa na style zake ukweli Chadema walikiwa na hali ngumj.Sijajua mama Samia atamuweka nani mtu wa makekekabisa. wananchi wanapokea negative kuteuliwa kwa mkolomije!
Naamini Mh. Mpango hajapenda hii🤔🤭Kiukweli katika waimbaji wote wa zile Pambio huyu Joyce Ndalichako sikuwahi msikia kabisa!! Ukijumlisha na uprofesa na ni mwanamke hahahaha!
What do u mean? Kwamba anaweza kuja na michezo yake ya kufungia bar, sjui shisha. Mara jumamosi ni siku ya usafi?Arusha wing get ready
Depal mlewee tu nyumbani 😅
Kwanini, unadhani?Naamini Mh. Mpango hajapenda hii🤔🤭