Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Uteuzi na Utenguzi: Paul Makonda ateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ndalichako aondolewa uwaziri

Acheni kujitoa ufahamu. Katibu wa Itikadi siasa na uenezi aliyepita kabla ya Bashite aliishia kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya. Ila yeye kawekwa mkuu wa mkoa wa Arusha kimkakati. Je yeye na Chongolo ambaye alikuwa katibu mkuu wa chama wana tofauti gani? Tena yeye kapewa jiji lenye ngome ya upinzani!?

Hapo ni siasa za CCM za kutafuta kuungwa mkono kaskazini. Kuitoa CCM haitowezekana kwa miaka 30 ijayo. Huo ndio ukweli mchungu. Kwa akili za upinzani kudemka inaonesha hawaijui siasa na watapigwa bao tena.

CCM ni dubwana kubwa sana.
Basi sawa.
 
Eti siasa za ccm kutafuta kuungwa mkono! Unachekesha sana. Bila majeshi ccm inaweza Fanya siasa Gani za kistaarabu. Ghafla umegeuka shehe Yahya, eti miaka 30 ijayo! Wewe inaweza jitabiria miaka Yako 30 ijayo!?
Hahaa Mkuu Jay Jay Nchi hii ina wajinga wengi sana tena wakubwa.

Huyo naye ni mwanajamii forum....jiulize Mwananchi wa kawaida yuko na hali gani ya ujinga.
 
Utapata wapi neno na wakati kila siku unajipendekeza na kujitoa ufahamu kiasi cha kufikia hatua ya kuweka mpaka namba yako ya simu! Ili tu ukimbukwe!! Na bado umeishia kupuuzwa tu na wenye chama chao!

Vipi sasa!! Utaendelea kumsifia tena Paul Makonda kama enzi zile alipokuwa Katibu Mwenezi wa chama chenu? Dogo, mimi kaka yako nakushauri bora ukawekeza tu nguvu zako zote kwenye kilimo cha kahawa hapo Mbozi! ccm ina wenyewe! Na wewe si mmoja wao!
Mkuu Tate Mkuu huyu Lucas Mwashambwa alikuwa mkulima nzuri Sana wa magimbi na parachichi hapa Mbodzi, tangia alianza kuwashabikia wakina Tulia mara Bashite ,Samia n.k ili apate teuzi ndio chanzo chakuua kilimo chake ila kwasasa labda amepata akili nakurudi kukamata jembe
 
Makonda na Chongoro nani alikuwa mkubwa??
Chongoro mkuu wa wilaya
Makonda mkuu wa mkoa sasa nani kashuka hap??
Kumbe unaandika andika TU hata taarifa huna! Punguza ujuaji wakati hujui kitu. Chongolo mkuu wa wilaya wa nyumbani kwenu labda.
 
Hivi unaakili kweli . Kwa hiyo uchaguzi wa 2025 haupo au uko mbele ya muda kwamba CCM amesha shinda uchaguzi wa 2025 unaelewa maana ya neno mkakati??
Bichwa kubwa akili ndogo .
Mkakati Gani ambao unamtegemea Makonda!? Magufuli alivyoiba chaguzi nchi nzima , Makonda alikuwa na cheo Gani!? Huyo Makonda hana huu ukuu unaotaka kumpa. Juzi TU hapa alikuwa nobody kabla ya kukumbukwa.
 
Mimi sina neno wala cha kuandika leo.Maana Mama anatupatia Sapraizi Watanzania Mpaka Unaona Nchi na wananchi wakitetemeka.
Inatakiwa uteuzi wa waziri wa pesa mtaani nao upate waziri,bajeti inapangwa hakuna mafungu,quarter zinapita mafungu hakuna,nini maana yake,Kizimkazi
 
Atakuja kutuambia hataki mtu aje kwenye mkoa wake wa Arusba

Sasa lile ghorofa analojenga ukweni pale njiro litaenda kwa kasi sana
 
Back
Top Bottom