Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni wadudu wa aina gani hao?!Hao wadudu shida tupuuu
Hataki habari zake zivuje lakin pia kuwe na smooth handover. Maana ukirudi ofisini asubuhi upo chini ya ulinzi 😀😀Huyu Rais huwa anatengua na kuteua usiku tu?!!!
Kufika augost 2025 walioteuliwa leo watakuwa wameishatenguliwa au kuhamishwa mara mbili au tatu.Hiki ndio anacho weza kufanya mara nyingi KIZIMKAZI pale magogoni. Kuliko jambo lolote. Na anapenda mno kutengu na kuteua.
KAZI ni kipimo Cha utu.
Ila magufuli alipokaa Zaid ya miaka Tano huku akiendelea kutumbua majipu yake ulikua unaimba kwaya tuh za hapa kazi tuh,mkoje wazee Parokia??HAya ndio anayo yaweza, hakuna kingine anacho weza.
Mwaka wa tatu still anaunda Serikali, Ruto ana mwaka mmoja kazini ila alisha achana na teua, tengua, hamisha, mwaka wa tatu Raisi anaunda Serikali.
Huko kwingine alikopelekwa alishindwa kuongoza!? Hana kitu huyo. Ndio walewale TU. Hamisha huku peleka kule performance sifuri.Uongozi ni muongoza njia. Anasimamia utendaji wa taasisi ili kufikia malengo na dira ambayo kimsingi bodi (anayoiongoza) ndio hupendekeza kwa maendeleo na ukuaji wa taasisi husika
Bahati mbaya vipi wakati anaenda kuwa mwenezi.Makala hakika ana bahati mbaya
Mzee kajitete na mashtaka yaliyo juu yako dhidi ya nnya za watu.Angewaacha HATA wale Pasaka JAMAN mama ana suprise
Issue hapo ni Makonda...TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanyau teuzi, utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwa Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe.Ndejembi anachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Makonda alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Anachukua nafasi ya Mhe.John Vianney Mongella ambaye atapangiwa kazi nyingine.
iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Kabla ya uteuzi huu Kanali Mtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazi nyingine.
v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwa Waziri.
vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Sillo anachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji.
ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemeja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes Kisaka Meena ambaye
amehamishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji.
xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. Nicholaus Mkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Habari.
xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mjumbe wa Tume ya
Mipango.
Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri na Naibu Makatibu Wakuuu tafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa 05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
View attachment 2949540
View attachment 2949541
Nguruwe hatuli peke yetu TU sisi mnaotuita wanaharamu kisa TU hatufanani Imani, tunakula pamoja na hao unaowaita ndugu zako katika Imani. Ila usione wivu sana sisi kula nguruwe, hata wewe hujakatazwa, ni shingo Yako ngumu kufuata Mila za mwarabu kwani wazee wako walikuwa wanakula hadi panya.Dah, Wala nguruwe watupu ,ila watu wa dini ya haki na ya Mungu mmoja huwakuti kulalama juu ya uteuzi kuwa wa waabudu masanamu watupu!
Ila ingetokea tofauti ungeona hawa wanaharamu wangemtusi prezidaa
Arusha imelipuka kwa furaha si mchezo
Angestaafu tu au sio ili kutoa fursa kwa vijana.Asha Rose Migiro anarudi tena kufanya nini?
ccm sijui wanatuonaje
Kwato za punda zinang'aa kama zimepigwa kiwi 😃😃😃View attachment 2949558
Tutakosa hizi heka heka
taratiiibuu wanampotezaMakonda kashushwa Cheo
Ila usione wivu sana sisi kula nguruwe, hata wewe hujakatazwa, ni shingo Yako ngumu kufuata Mila za mwarabu.