Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Fitina za JK kazini. Kindamba ni team JPM kamheshimu sana kumpa ubalozi.

Pole pole amenyamazishwa kisomi, achague moja aidha asusie cheo aendelee kuongea au akafanye kazi na akae kimya.
 

POLEPOLE KUWA BALOZI MALAWI… kuteuliwa tarehe 14.3.2022 kuapishwa tarehe 15.3.2022 ?​

Kwanini ni dharura hivyo? Msechu wa NHC alifukuzwa na JPM na Samia leo anapewa nafasi ile ile na Samia?​

Mwenye kufahamu Samia anakutupeleka anielewesha tafadhali, mimi ninaona kama tunapotea njia.​

Kwani kutumbuliwa na magufuli ni dhambi
 
Ninavyomjua HP ,Huko kwa Wanyasa Hatakwenda.Yeye siyo wa kupelekwa pelekwa.By the way alisema yeye njaa haiumagi kihivyo.Alifika Dar muda mrefu. na alikuwa na mpango wa kutogombea ubunge baada ya kumaliza muda wake
 

POLEPOLE KUWA BALOZI MALAWI… kuteuliwa tarehe 14.3.2022 kuapishwa tarehe 15.3.2022 ?​

Kwanini ni dharura hivyo? Msechu wa NHC alifukuzwa na JPM na Samia leo anapewa nafasi ile ile na Samia?​

Mwenye kufahamu Samia anakutupeleka anielewesha tafadhali, mimi ninaona kama tunapotea njia.​

Masuala ya kisiasa sio ya kuweka moyoni kama vile ushabiki wa Yanga na Simba, utajikuta unaumiza tu nafsi.
 
mara mwakani anastafishwa ubalozi....kataa wahuni wanamtoa kijanja mnoo 😂
 
Akirudi akalime vitunguu, kijijini kwao hii ni demotionbkubwa sana
 
Rais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Peter Ulanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Ulanga ni Mkurugenzi Mstaafu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF).

Na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali John Julius Mbungo, Mkurugenzi Mstaafu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Meli Tanzania (MSCL).

View attachment 2150380
Nchi inaongozwa na watu wa hivyo,yani mchechu ndio anaweza NHC na wengine hawawezi...jk anaongoza hii serikali nchi inarudi kwenye upigaji
 
Back
Top Bottom